RAIS MTEULE WA MISRI EL-SISI AAPISHWA NA KUKABIDHIWA MADARAKA

Abdel-Fattah al-Sisi ameapishwa kuwa rais mpya wa Misri katika seherehe iliyofanywa kwenye mahakama makuu ya katiba mjini Cairo. Baada ya kaapishwa, Rais Sisi alikwenda ikulu kwa ajili ya sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kutoka nchi kadha. Kiongozi wa muda, Adly Mansour na Bwana al-Sisi walitia saini waraka wa kukabidhi madaraka kwake rais mpya - kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri. Rais mpya alisema hilo ni tukio la kihistoria. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi alishinda katika uchaguzi wa mwezi uliopita kwa asili-mia-97, ingawa upinzani ulisusia uchaguzi huo. Wafuasi wa Rais al-Sisi walisherehekea katika medani ya Tahrir mjini Cairo. Mfuasi mmoja wa al-Sisi, Fakhri Gamel Abdul Khaleq, alisema anatumai sherehe za leo ndio zitamaliza matatizo yaliyopita: "nampongeza Bwana rais anapoapishwa leo. Mungu ajaalie uwe mwaka wa furaha kwetu na kwa Wamisri wote. Na tunaomba Mungu atunusuru na yale yaliyotokea kabla, na tutakuwa watu wema. Mungu akipenda, kama alivosema rais, tutakuwa mfano mzuri wa ustaarabu".

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU