RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri ,Cairo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Abdel Fatah el Sisi. Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo. Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50. Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi. Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood. Chanzo: BBC

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

VALENTINE DAY'S QUOTES

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018