KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ENGLAND YATOKA SARE NA ECUADOR 2-2

Katika mechi za kirafiki kwa maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, England ilitoka sare ya 2 - 2, dhidi ya Ecuador katika mechi iliyochezwa huko Miami.

Timu ya England iliongozwa na Frank Lampard. Raheem Sterling ambaye huchezea klabu ya Liverpool, alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United. Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki itakayofuata. 

Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda mapumziko. 

Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

BEYONCÉ FT JAY Z-DRUNK IN LOVE SONG LYRICS

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI (AWAMU YA PILI)

ABIRIA 52 WALIOKWAMA KATIKA MELI HUKO ANTAKTIKA WAOKOLEWA

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA