KESI YA UMILIKI WA NYIMBO ZA BOB MARLEY YAMALIZIKA
Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.
Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.
Comments
Post a Comment