HATIMAYE CAMEROON WAPANDA NDEGE NE KUELEKEA BRAZIL BAADA YA KUONGEZEWA PESA

Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa. Wachezaji hao, almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe. Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.

Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha. Haijabainika vyema ngapi wameongezewa ndio wakakubali safari.

Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'. Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

BEYONCÉ FT JAY Z-DRUNK IN LOVE SONG LYRICS

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI (AWAMU YA PILI)

ABIRIA 52 WALIOKWAMA KATIKA MELI HUKO ANTAKTIKA WAOKOLEWA

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA