Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wameshambulia wanakijiji karibu na mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwaua watu 45.
Walioponea kifo waliambia BBC kwamba washambuliaji hao walijidai kuwa walikuwa wamekuja kuwahubiria wanakijiji kabla ya kuanza kuwafyatulia risasi kiholea.
Wakati huohuo,wakazi pamoja na maafisa wakuu wanasema kuwa watu 200 waliuawa katika mashambulizi tofauti mapema wiki hii.
Mji wa Maiduguri na vitongoji vyake, haujaathirika sana na mashambulizi tangu kutangazwa kwa sheria ya hali ya hatari mwaka mmoja uliopita.
Maeneo ya mashinani ndio sasa hulengwa kwa mashambulizi
Serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na shinikizo ndani ya nchi na kimataifa kuongeza juhudi za kukabiliana na kundi la Boko Haram tangu liwateke nyara wasichana zaidi ya miambili wa shule mwezi Aprili.
Kundi hilo limekuwa likiendesha harakati zake tangu mwaka 2009 katika juhudi za kudai uongozi wa kiisilamu.
Maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi mbali mbali ikiwemo maafisa wa usalama.
'Wanakijiji wahadaiwa'
Washambuliaji waliingia katika kijiji cha Barderi, karibu na chuo kikuu cha Maiduguri viungani mwa mji wa Maiduguri, wakiwaambia watu kuwa walikuwa wamekuja kuwahubiria, lakini baadaye wakaanza kuwashambulia kwa bunduki.
Wapiganaji hao wamewahi kutumia mbinu kama hizi za kijanja kuwahadaa wanakijiji na baadaye kuwashambulia.
Ramani ya Afrika. Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo: 1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia. 2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti. 3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takriba...
Comments
Post a Comment