KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: UFARANSA YAICHAPA 8-0 JAMAICA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI
Mshambulizi wa Arsenal Olivier Giroud alifunga bao na kuiongoza ''Le Blues'' kuilaza Jamaica mabao 8-0 katika mechi yao ya mwisho ya kujipima nguvu iliyochezwa siku ya Jumapili.
Ufaransa ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 kufikia muda wa mapumziko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi na Karim Benzema wakimpa kocha Didier Deschamps kila sababu ya kutabasamu kabla ya kudundadunda.
Matuidi na Benzema walifunga tena katika kipindi cha pili, huku bao lake Giroud na mengine mawili kutoka kwa Griezmann yakitamatisha ushindi wao.
Ufaransa 8-0 Jamaica
Ufaransa itakabiliana na Honduras, Uswisi na Equador katika kundi E.
Kiungo cha kati wa Real Madrid Benzemaa lionyesha mchezo wa kuridhisha huku Ufaransa ikionyesha kwamba inaweza kujikimu bila Franck Ribery ambaye hatahudhuria michezo ya Kombe la Dunia kutoana na jeraha la mgongo.
Hugo Lloris anaychezea Tottenham Hotspurs, Patrice Evra wa Manchester United, Mamadou Sakho wa Liverpool na Moussa Sissoko wa Newcastle walicheza mechi hiyo.
Hapo baadae, beki wa Asenal na Loic Remy wa Queens Park Rangers waliingia kama wachezaji wa ziada.
Comments
Post a Comment