TCU IMEFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA AWAMU YA PILI



Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imefungua tena dirisha la udahiri kwa Wanafunzi wanaoomba kuchaguliwa katika kozi mbalimbali za Shahada ya Kwanza mwaka huu wa masomo 2016/2017. Linasomeka hivi:

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe
31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba
udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali
mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe
12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
• Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
• Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
• Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana
na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
• Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na
matokeo yao yameshatoka,
• Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
• Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo
vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za
kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016.




Unaweza kusoma zaidi kwa KUBOFYA HAPA

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MFAHAMU KARL MARX KWA UFUPI: DUNIA INAMKUMBUKA LEO

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018