MTU MMOJA AMEJITOA MUHANGA NA KUUA WATU 16 KATIKA MSIKITI WA MOHMAND PAKISTAN

Takribani watu 16 wameuawa na wengine 35 kujeruhiwa katika swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Mohmand huko Pakistan.

Duru za habari zinasema kuwa mtu huyo aliyejitoa muhanga ameua watu 16 na wengine 35 kujeruhiwa walipokuwa wakihudhuria swala ya Ijumaa kaskazini mashariki mwa  Pakistan.

Shambulio hilo limetokea katika kijiji cha Anbar Tehsil katika wilaya inayokaliwa na kabila la Mohmand ambapo jeshi la Pakistan limekuwa likipambana na kundi la Taliban.

"Swala ya Ijumaa ilikuwa ikiendelea msikitini hapo wakati ambapo mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua na kuua waumini 16 na kujeruhi wengine 35" kiongozi mmoja wa Mohmand aliliambia shirika la habari la AFP.

Hakujatokea taarifa zozote kuhusu shambulio hilo, lakini kundi la Taliban linashutumiwa kuhusika na shambulio hilo kwa kuwa limekuwa likifanya mashambulio katika maeneo ya mahakama, shule na misikiti.

Jeshi la Pakistan limekuwa likifanya operesheni toka Juni 2014 kuangamiza makundi yote ya kigaidi yaliweka ngome kaskazini mashariki mwa maeneo hayo ili kuepusha vifo vya watu wasio na hatia toka 2004.


Chanzo: Al Jazeera

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017