LEO SEPTEMBA 10 KATIKA HISTORIA

George Washington, Rais wa Kwanza wa Marekani
Leo ni tarehe 10 Septemba siku ya 254 katika mwaka 2016, zimesalia siku 112 kuumaliza mwaka huu 2016.

TUANGALIE MATUKIO MUHIMU YALIYOTOKEA TAREHE KAMA YA LEO


210 K.K - Mtawala wa kwanza wa Dola ya Qin (Qin Dynasty) ya nchini China alifariki.

1776 - George Washington aliomba mpelelezi wa siri wa kujitolea, Nathan Hale akajitolea.

1993 - Israel ilisaini mkataba wa utambuzi na PLO.


1919 - Jiji la New York lilimkaribisha nyumbani Jenerali John J. Peshing na wanajeshi wengine 25,000 waliolitumikia jeshi la Marekanj katika vita ya kwanza ya Dunia katika divisheni ya kwanza.

1939 - Canada ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani.

1945 - Vidkun Quisling alihukumiwa kifo kwa kushirikiana na jeshi la Ujerumani Nazi nchini Norway. Aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 1945.

1963 - Wanafunzi weusi 20 (negro) waliruhusiwa kusoma katika shule za serikali za Alabama kufuatia makubaliano kati ya Serikali kuu na Gavana George C. Wallace.

1974 - Guinea-Bissau ilipata uhuru wake kamili kutoka kwa Ureno.

1979 - Wanaharakati wanne wa Puerto Rico walihukumiwa kwenda jela kwa kosa la kufanya shambulizi katika Bunge la Wawakilishi nchini Marekani mwaka 1953 na jaribio la kutaka kumuua Rais wa Marekani, Harry S. Truman mwaka 1950. Waliachiwa baadae kwa msaha kutoka kwa Rais Jimmy Carter.

2008 - Jaribio lililoitwa Hadron Collider ambalo ni jaribio kunwa kiwahi kufanyika katika historia ya binadamu lilifanywa huko Geneva, Uswisi.


KUZALIWA

1638 - Malikia Maria Theresa akiwa mke wa Mfalme Lous XIV wa Hispania maarufu kama "Maria Theresa wa Hispania" alizaliwa huko El Escorial nchini Hispania.

1928 - Mwanafalsafa wa Canada, Jean Vanier alizaliwa.

1931 - Muigizaji wa Matekani Philip Baker Hall alizaliwa.

1940 - Mwanamuziki wa Marekani Roy Ayers alizaliwa.

1953 - Muigizaji wa kike wa Marekani Amy Irving alizaliwa.

1957 - Mwanamuziki wa Uingereza Siobhan Fahey alizaliwa.

1958 - First lady wa Canada Margaret Trudeau alizaliwa.

1960 - Muigizaji wa Uingereza Colin Firth alizaliwa.

1968 - Muongozajj wa filamu wa Uingereza Guy Ritchie alizaliwa.

1974 - Muigizaji wa Marekani Ryan Phillippe alizaliwa.

1979 - Muigizaji wa Marekani Jacob Young alizaliwa.


KWA MSAADA WA MTANDAO

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA