WATU 10 WAMEKUFA KATIKA AJALI YA MOTO KIWANDANI HUKO BANGLADESH

Takribani watu 10 wamekufa katika mlipuko mkubwa wa moto huko Bangladesh kufuatia kulipuka kwa kontena la kuchemshia maji ya moto.

 Polisi wamesema kuwa takribani watu 100 walikuwa ndani ya kiwanda hicho chenye jengo la ghorofa 4 ambapo mlipuko ulisikika katika mji wa Tongi.

Takribani watu 30 wamejeruhiwa  kutokana na moto huo kusambaa kwa haraka katika jengo hilo.

Huduma za dharura zinadai kuwa moto bado unaendelea kuwaka na inasemekana idadi ya watu kufariki katika ajali hiyo inaweza kuongezeka.

"Mpaka sasa tumepata uhakika wa watu 10 kufariki. Lakini bado idadi inaweza kuongezeka kwa sababu moto bado ni mkali kushindwa kuzimwa." Inspekta wa Polisi Sirajul Islam aliiambia AFP.

Kumekuwa na majanga mengi ya moto viwandani nchini Bangladesh kufuatia kutokuwa na usalama wa kuzuia majanga hayo katika nchi hiyo.


Canzo: BBC

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

LIST OF UNDERGRADUATES SELECTED TO JOIN TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

VIFAA VYA KUWATAMBUA WENYE UGONJWA WA EBOLA VYAINGIZWA NCHINI

TAZAMA HAPA MAGOLI 10 BORA YA KOMBE LA DUNIA 2018