LEO SEPTEMBA 12 KATIKA HISTORIA

Tarehe kama ya leo Septemba 12, 1973 muigizaji wa Marekani, Paul Walker alizaliwa huko Glendale, Califonia.Alifariki Novemba 30, 2013.
Leo ni tarehe 12 Septemba, siku ya 256 katika mwaka 2016, zimesalia siku 110 kuukamilisha mwaka 2016.

MATUKIO

Leo kuna matukio mengi sana hata hivyo tuyaangalie kama ifuatavyo:

1217 - Mfalme wa Ufaransa Prince Louis na Mfalme wa Uingerza Henry III walisaini mkataba wa amani.

1624 - Meli ya kwanza kupita chini ya maji ilijaribiwa katika Mto Thames kwa ajili ya kutumiwa na Mfalme James I huko Uingereza.

1662 - John Flamsteed aliona nusu ya kupatwa kwa jua na ikampelekea kuvutiwa na elimu ya anga (unajimu)

1703 - Jeshi la Uingereza chini ya Archiduke Charles wa Austria waliwasili nchini Ureno.

1722 - Vikosi vya Urusi viliteka Baku na Derbent huko Persia ambayo kwa sasa ni Iran.

1751 - Amsterdam ilikataa kuanzisha makazi ya Wayahudi.

1753 - Mnajimu wa Ufaransa Charles Messier bila kutarajia aligundua gesi ya miamba (crab nebula) na akaanza utafiti wake (Messier Catalogue)

1848 - Uswisi iliunganisha mataifa yake kupata taifa moja la Uswisi.

1878 - Mfalme Leopold II wa Ubelgiji alifungua Mkutano wa Kongo.

1885 - Rekodi ya kwanza ya magoli 35 katika mechi ya ligi daraja la kwanza iliwekwa.

1890 - Cecil Rhodes alifika Harare, Zimbabwe kwa wakati ule ikiitwa Fort Salisbury.

1909 - Waarabu walivamia Gedara Palestina.

1919 - Adolf Hitler aliungana na Chama cha Wafanyakazi wa Ujerumani akiwa mwanachama wa saba lakini hakukubaliana na lengo la chama hicho badala yake alisisitiza Utaifa (Harakati za nchi binafsi) na kusisitiza chuki dhidi ya Wayahudi.

1922 - Mwanariadha Paavo Nurmi aliweka rekodi ya dunia kwa kukimbia umbali wa mita 5000 sawa na kilomita 5 kwa daika 14:35.4

1928 - Kimbunga Hurricane kiliua watu 6,000.

1934 - Estonia, Lativia & walisaini mkataba wa Baltic Entente dhidi ya Muungano wa nchi za Kisovieti.

1941 - Meli ya kwanza ya kijerumani katika vita ya pili ya Dunia ilitekwa na meli za Marekani.

1943 - Taifa la Skorzeny lilimuachia Benito Nussolini huko Gran Sasso.

1944 - Vikosi vya Marekani viliingia nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza.

1950 - Serikali ya Ubelgiji iliwafukuza wafanyakazi wote wa kikomunisti.

1956 - Wanafunzi weusi waliruhusiwa kusoma shule ya Ckay Ky huko Marekani.

1958 - Marekani ilifanya jaribio lake la Nyuklia katika uwanja wa majaribio wa Nevada.

1958 - Muhandisi Jack Kilby alifanya jaribio la sakiti ya kompyuta aliyogundua kwa msimamizi wake.

1959 - Muungano wa nchi za kisovieti (USSR) ulituma chombo Luna 2 kwenda kwenye mwezi.

1961 - Urusi ilifanya jaribio lake la nyuklia huko Novaya Zemlya.

1971 - Urusi ilituma chombo chake kwenye mwezi Luna 16.

1973 - Urusi ilifanya tena jaribio la Nyuklia huko Novaya Zemlya.

1974 - Mfalme Haile Sellasie alipinduliwa nchini Ethiopia.

1978 - Fidel Castro alitembelea Addis Ababa Ethiopia.

1979 - Indonesia ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa 8.1 katika kipimo cha Richter.

1984 - Ethiopia iliunda Jamhuri ya Kisoshalisti.

1987 - Ethiopia ilianza kufuata utawala wa Katiba.

1992 - Mae Jemison alikuwa mwanamke wa kwanza Mmarwkani mweusi kwenda angani.

1999 - Indonesia ilisema itaruhusu walinzi wa amani Mashariki mwa Timor.

2005 - Israel iliondosha majeshi na vikosi vyake kutoka ukanda wa Gaza.

2007 - Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alitangaza nia yake ya kujiuzulu wadhifa huo.

2007 - Rais wa zamani wa Ufilipino Joseph Estrada kwa kosa na wizi wa fedha za serikali.

2010 - Lady Gaga na Eminem walichukua tuzo za MTV Video Music.

2012 - Kampuni ya Apple ilitangaza na kuonesha simu zao iPhone 5 na iOS 6.

2015 - Watalii 12 waliuawa bila kukusudia na Jeshi la Misri Magahribi mwa Jangwa la Misri wakidhaniwa kuwa ni waasi.




KUZALIWA

1575 -  Mtafiti wa Uingereza Henry Hudson.

1913 - Mwanaridha Jesse Owen.

1973 - Muigizaji Paul Walker.

1977 - Muigizaji Connor Frante.

1978 - Muigizaji Benjamin McKenzie.

1981 - Muigizaji na Mwanamuziki Jennifer Hudson.



IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017