Aidha TCU inakumbusha kwamba wale waliokwisha omba na hawakupangiwa kwa kukosa sifa stahiki za vyuo walivyopangiwa hawatatakiwa kulipia tena.
Pia wadahiliwa wapya wanatakiwa kulipia kiasi cha fedha za kitanzania Tsh. Elfu Hamsini (50,000/=) kama gharama za udahili. Fedha hii huwa hairudishwi.
Vilevile TCU inakumbusha kwamba kozi ambazo zimejaa tayari hazitaonekana kwenye mfumo wa Udahili (CAS).
Aidha TCU inawakumbusha waombaji kuwa mwisho wa kutuma maombi ya udahili ni Septemba 23 na hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza kwa wale watakaoshindw kuomba vyuo katika muda huo ulioongezwa.
0 comments:
Post a Comment