LEO SEPTEMBA 11 KATIKA HISTORIA

Leo ni tarehe 11 Septemba, siku ya 255 katika mwaka 2016, zimesalia siku 111 kumaliza mwaka huu 2016.

MATUKIO

1740 - Daktari mweusi aliyetibu meno alitajwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Pennsylvania 

1777 - Mapigano ya vita ya Brandywine yalianza huko Pennsylvania ambapo General George Washington na vikosi vyake walishindwa na General Sir William Howe wa Uingereza

1915 - Mkutano wa Zimmerwald uliitishwa kurejesha amani wakati wa vita ya kwanza ya Dunia.

1940 - Adof Hitler alituma vikosi vyake Mashariki mwa Romania katika vita ya pili ya dunia.

1944 - Vikosi vya Marekani viliingia Luxembourg.

1974 - Haile Selassie I aliondolewa madarakani huko Ethiopia.

1997 - Scotland ilipiga kura ya kuwa na Bunge lake kamili baada ya miaka 290 ya Muungano na England.

Jengo la Kituo cha Biashara Duniani (WTC) lililolipuliwa Septemba 11, 2001 na kundi la Al-Qaeda.

2001 - Mnamo majira ya saa 2 na
 dakika 45 asubuhi ikiwa siku ya Jumanne, ndege mbili za abiria za Marekani Boeing 767 zilitekwa angani na kugonga katika jengo la Kituo cha Biashara duniani (WTC) ambapo watu wengi waliuawa. Inasidikika kuwa tukio hilo la ugaidi liliungwa mkono na magaidi wa Kiislamu kutoka Saudi Arabia na kundi la Al Qaeda ilililokuwa chini ya Osama bin Laden kwa kipindi hicho.

2005 - Israel iliwaondoa wananchi wake na vikosi vyake vya jeshi katika mapiagano dhidi ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.

2007 - Urusi ilifanya jaribio la kulipua bomu la Nano lililoitwa "Father of Bombs" yaani Baba la Mabomu yote ambalo lilikuwa ni bomu lisilo la nyuklia kuwahi kutengenezwa.

2012 - Ofisi za Ubalozi wa Mareani nchini Libya katika mji wa Benghazi zilichomwa moto na kupelekea vifo vya watu 4 akiwemo balozi wa Marekani nchini Libya, Christopher Stevens


KUZALIWA

1700 - Mshairi wa Scotland, James Thomson.

1877 - Mwanasayansi James Jeans.

1862 - Mwandishi wa Marekani O. Henry (William Sydney Porter) alizaliwa.

1939 - Charles M. Chuck Geschke muanzilishi wa Adobe System Inc.

1965 - Rais wa Syria Bashal al-Assad. Yupo madarakani tangu mwaka 2000.

1977 - Rapa Ludacris.
Rapa Ludacris alizaliwa mwaka 1977.


VIFO

1971 - Nikita Khrushchev moja kati ya viongozi wa kisoshalist alifariki akiwa na miaka 77 katika kipindi cha vita baridi.

NUKUU

"Kama mtu ameishi katika vita, umaskini na upendo, ameishi maisha kamili" - O. Henry.


KWA MSAADA WA MTANDAO.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA