VIDEO: HII NDIYO MAANA HALISI YA SEPTEMBA 11 HUKO MAREKANI

Mnamo mwaka 2001 ndege mbili za abiria za chini Marekani zilitekwa angani na magaidi wanaodhaniwa kuwa ni Al-Qaeda. Ndege hizo mbili aina ya Boeing 767 ziligonga katika majengo pacha ya Kituo cha Biashara Duniani (WTC) lililoko katika jiji la New York nchini Marekani. Hili lilikuwa ni shambulio kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na magaidi wa Al-Qaeda ambao kwa kipindi hicho kundi hilo lilikuwa likiongozwa na Osama bin Laden ambaye aliuawa miaka ya hivi karibuni na wanajeshi wa jeshi la Marekani (wanavyodai wao Marekani). 

Pia kundi la Al Qaeda lilikuwa limelenga kuteketeza jengo la Idara ya Ulinzi ya Marekani, The Pentagon ambako ndiyo makao makuu ya Idara ya Ulinzi ya nci ya Marekani. Lakini pia ililengwa Ikulu ya Marekani 'The White House'.

Watu wapatao 2,996 pamoja na watekelezaji wa tukio hilo wakiwa 19 waliuawa. Watu zaidi ya 6,000 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Pia tukio hilo lilisababisha uharibifu wa mali hasa majengo na miundo mbinu uliofikia dola bilioni 10. Jumla kuu ya uharibifu ilikadiriwa kuwa dola za kimarekani trilioni 3. 

Katika kutekeleza tukio hilo la ugaidi magaidi 19 walihusika ambapo 15 walikuwa ni raia wa Saudi Arabia, 2 kutoka Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), 1 kutoka Misri na 1 kutoka Lebanon.

Historia ya Al Qaeda inarudi nyuma katika mwaka 1979 ambapo Muungano wa Kisoviet uliivamia Afghanistan. Osama alisafiri hadi Afghanistan na kuunda kikundi cha kiarabu cha wajahideen kupingana na Wasoviet. Osama aliendelea kuwa kinyume na Wamarekani na mwaka 1996 alitoa tamko lililotaka majeshi ya Marekani kuondoka Saudia Arabia

Shambulio hili lilkuwa kama ifuatavyo:
  • Ndege ya Shirika la Marekani (American Airlines Flight 11) aina ya Boeing 767 iliondoka Logan airpot ikiwa na crew ya watu 11 pamoja na abiria 76 (watekaji 5 hawakuhesabiwa) ndege hiyo iligeuzwa ruti ikiwa angani na kugonga katika kituo cha biashara Duniani saa 8:46 am saa za Marekani.
  • Ndege ya pili ya Marekani (American Airlines Flight 77) Boeing 757 iliondoka Washington Dulles Airport kuelekea Los Angels, California ikiwa na crew ya watu 6 na abiria 53 (watekaji wameondolewa katika hesabu hiyo). Watekaji walifanikiwa kuiteka na kugonga jengo la ulinzi la Marekani The Pentagon saa 9:37 am saa za Marekani.
  • Ndege ya tatu (United Airlines Flight 93) Boing 757 iliondoka  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa New York ikielekea San Fransisco kabla ya kutekwa angani na kugonga Stonycreek Township  karibu na Shanksville, Pennsylvania saa 10:03 am saa za Marekani. Abiria walikuwa 33 na crew ya watu 7 huku watekaji wakiwa 4.
  • Ndege nyingine American Airline Flight 11 Boeing 767 ilikuwa na abiria 51 crew ya watu 9 na watekaji 5 iliondoka Los Angels na kutekwa angani hadi WTC saa 9:03 am dakika chache mara baada ya Shambulio la awali.



Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo



WTC kabla ya shambulio


WTC kabla ya shambulio



WTC kabla ya shambulio



Nimekuwekea video pia ambapo unaweza kutazama tukio hilo





Makala hii imeandaliwa kwa Msaada wa Mtandao (Wikipedia, Britannica na YouTube)

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017