KATY PERRY AMESEMA ATAFANYA COLLABO NA TAYLOR SWIFT KAMA ATAOMBA MSAMAHA
Katy Perry na Taylor Swift wakiwa Berley Hilton Hotel Januari 30, 2010 |
Katy Perry na Taylor Swift kufanya collabo?
Collabo hiyo inaweza kutokea lakini kwa sharti moja tu kutoka kwa Katy Perry, kama Taylor Swift atakubali kumuomba msamaha.Hili linakuja baada ya shabiki mmoja wa Katy Perry kuuliza katika mtandao wa Twitter kama Katy Perry anaweza kufanya collabo na Swift, Perry akajibu kwa kifupi "hakika, kama ataomba msamaha"
Mgogoro kati ya mastaa hawa wawili wa Pop ulianza mwaka 2014 kufuatia Swift kumteta Katy katika Mtandao wa The Rolling Stone kuwa wimbo wake "Bad blood" ulikuwa unamhusu Swift.
"Alifanya kitu kibaya sana" alisema Swift. "Ilikuwa kama hivyo. Tumekuwa maadui. Na sababu haikuwa mwanaume. Ni kazi tu. Alijaribu hata kuvuruga tamasha langu. Alijaribu hata kuwapa hela vijana waje kunitoa jukwaani"
JE, KATY PERRY AMETHIBITISHA KUWA WIMBO WA 'BAD BLOOD' UNAMHUSU SWIFT?
Mtandao wa The Internet ulisema kwamba Katy Perry ndiye mwenye makosa, kufuatia baadhi ya madansa wa Swift kuondoka kwenye tour ya Swift kufuatia mpango ulofanywa na Katy Perry.Muda mfupi baada ya Mahojiano na The Rolling Stone yaliyokuwa ya moja kwa moja, Katy alitweet katika mtandao wa Twitter "Kaa tayari kwa kipindi cha Regina George kuhusu nguo za kondoo".
Baadaye kwenye mahojiano mwaka 2015 na Billboard Perry alisema "kama kuna mtu atajaribu kuniharibia sifa yangu, mtamsikia tu"
Chanzo: Billboard
Comments
Post a Comment