Skip to main content

WALIOKUFA KATIKA TETEMEKO WAFIKIA 16

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kuaga miili ya waliokufa katika tetemeko la ardhi mkoani Kagera.


Maafa zaidi yameripotiwa katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea juzi mkoani Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 16, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule yameanguka.

Tukio hilo limemfanya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kulazimika kufanya ziara ya ghafla ya kuwatembelea waathirika wa tetemeko hilo, ambalo limedaiwa kusababisha tafrani pia katika nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki za Kenya na Rwanda.

Katika hatua nyingine, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo eneo la Tengeru, mkoani Arusha kimeeleza mpango wa kuanza kufunga vifaa vitakavyotoa ishara ya matukio ya matetemeko ya ardhi kabla majanga hayo kutokea.

Katika mradi huo maalumu chini ya Kitengo cha Utafiti wa Miamba na Volcano, chuo hicho kitashirikiana na taasisi mbalimbali za elimu ya juu zilizopo Ulaya na Marekani, hasa Chuo Kikuu cha Glasgow kilichopo Scotland, kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Burton Mwamila. Ziara ya Waziri Mkuu

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu jana katika Uwanja wa Kaitaba ulioko mjini Bukoba ambapo umeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuaga miili ya watu waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema tukio hilo ni la kwanza kutokea mkoani humo na kwamba limeleta madhara makubwa kwa wananchi na kuacha majonzi makubwa.

Kijuu alisema mpaka taarifa inaandaliwa watu 16 waliripotiwa kupoteza maisha na kusababisha majeruhi 253, huku 170 wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo na 83 wakitibiwa na kuruhusiwa.

Alisema pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 840 za makazi kuanguka, nyumba 1,264 kupata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka.

Alisema tetemeko hilo lenye ukubwa wa alama 5.7 uliopimwa kwa kipimo cha Ritcher cha kisayansi cha kupima matetemeko, limeleta madhara makubwa ambapo Serikali ya Mkoa inaendelea kutathmini kwa kina athari zaidi zilizosababishwa na tetemeko hilo na pia uharibifu uliojitokeza kisha kupeleka katika Ofisi ya Waziri Mkuu waone jinsi ya kusaidia.

Alisema hatua zilizochukuliwa na mkoa mpaka sasa ni kuwaokoa na kuwapeleka watu hospitali kwa ajili ya matibabu na kuwapatia makazi ya muda baadhi ya wananchi wenye nyumba zilizoathirika, wakati mipango mingine ikiandaliwa.

Taarifa hiyo ya Mkuu wa Mkoa, ilimfanya Waziri Mkuu kueleza masikitiko yake na serikali kutokana na janga hilo na kutoa salamu za pole kwa wananchi waliopatwa na madhara na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa na pia maeneo yote yaliyoathirika.

"Leo si siku nzuri kwetu, nimekuja kumwakilisha Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anawapa pole sana wana Kagera wote na Watanzania kwa ujumla. Pia Makamu wa Rais anawapa pole kwa msiba huu mkubwa, lengo la safari yangu ni kuja kuwapa pole, tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea Tanzania, tumekuwa tukisikia kutoka mataifa ya nje lakini leo limetupata nchini kwetu," alisema Majaliwa.

Aliwasihi na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu, kuonesha umoja na ushirikiano, lakini pia kujitokeza kuwafariji wenzao wakati wote wa majonzi, huku akisema Watanzania kwa miaka mingi wamekuwa wakishuhudia mitikisiko midogo, lakini juzi tumeshuhudia mtikisiko mkubwa kabisa ambao umeleta madhara makubwa kwetu.

"Mpaka sasa hatuna uhakika mtikisiko huu utakuwa endelevu kwa kiasi gani, nataka niwahakikishie Watanzania wote, Serikali tunafanya mawasiliano na taasisi zenye uwezo wa kubaini mtikisiko huu ili tuweze kujua jambo hili litakuwa endelevu kwa kiasi gani na kuona dalili na ukubwa wake utakuwaje ili tujipange katika kutoa elimu lakini pia tahadhari pindi jambo kama hili linapoweza kutokea au tunapoona viashiria au dalili za jambo hili," alisema Waziri Mkuu.

Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa katika taarifa yake alimweleza kwamba tathmini inaendelea na kwamba ameiagiza Kamati ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kufika mkoani Kagera mara moja na kuzunguka mkoa mzima kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa kwa lengo la kufanya tathmini ya jumla.

Alisema baada ya tathmini hiyo, utaratibu utafuatwa kwani serikali haiwezi kuwatupa mkono wananchi hao, pia alitumia fursa hiyo kuwaambia wafiwa kuwa Watanzania nchini kote wako pamoja nao katika janga hilo.

Akielezea mkasa huo, majeruhi Happines Apolinary ambaye ni mkazi wa kata ya Buyekera aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa kuumia kichwani na mgongoni, alisema alishtuka kusikia mtikisiko mkubwa wakati akiwa ndani ya nyumba yake na ghafla aliangukiwa na kuta na kumsababishia majeraha. Pamoja na kueleza kuumia vibaya kutokana na tukio hilo, Happines aliwashukuru wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa huduma nzuri waliyompatia tangu juzi alipofikishwa hospitalini hapo.

Majeruhi mwingine, Paulina Spilian aliyelazwa hospitalini hapo akiwa amejeruhiwa miguu alisema akiwa ndani ya nyumba yake ghafla alisikia mtikisiko mkubwa ulioambatana na kishindo cha kuanguka kwa kuta za nyumba na akiwa katika harakati za kutaka kukimbia nje aliangukiwa na ukuta miguuni.

Majeruhi huyo aliiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwajengea nyumba na pia kuwapa elimu kuhusiana na matukio kama hayo ili waweze kujiokoa baada ya kuona dalili au viashiria tofauti na ilivyotokea juzi.

Advela Respicius ambaye ni mama wa marehemu, Verdiana Respicius aliyekufa baada ya kufunikwa na kifusi cha nyumba, akizungumza kwa niaba ya familia za wafiwa wa tukio hilo, alitoa shukrani kwa serikali kwa kutoa majeneza, sanda na usafiri wa kuwapeleka marehemu hao mpaka vijijini kwa ajili ya maziko.

Vifaa vya kutabiri kufungwa Wakati hofu ikiwa bado imetawala kutokana na tukio hilo hasa kutokana na wananchi wa Kagera kueleza kutofahamu lolote kabla ya kutokea kwa tetemeko kutokana na kutopewa taarifa zozote na mamlaka za serikali, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo eneo la Tengeru, mkoani Arusha kimesema kinatarajia kuanza kufunga vifaa vitakavyotoa ishara ya matukio ya matetemeko ya ardhi kabla majanga hayo kutokea.

Katika mradi huo maalumu chini ya Kitengo cha Utafiti wa Miamba na Volcano, chuo hicho kitashirikiana na taasisi mbalimbali za elimu ya juu zilizopo Ulaya na Marekani, lakini hasa Chuo Kikuu cha Glasgow kilichopo Scotland, kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Burton Mwamila.

Katika mradi huo wa kwanza nchini unaolenga kutoa utabiri wa matukio ya matetemeko na ulipukaji wa volcano nchini, vifaa maalumu vitakavyokuwa vinapima uwezekano wa kutokea majanga hayo, vitafungwa katika maeneo nyeti kama milima, vilima na sehemu ambazo huwa na volcano hai.

Mtaalamu wa miamba ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya 'Eco Science' inayoshughulika na utafiti wa miamba pamoja na milipuko ya volcano, Dk Ben Beeckmans amefafanua kuwa 'Mlima wa Mungu' (Oldonyo Lengai) uliopo eneo la Ngaresero, wilayani Ngorongoro ndio chanzo kikubwa cha matetemeko ya ardhi katika eneo lote la Afrika Mashariki. Mlima huo wenye volkano hai pia umekuwa ukilipuka mara kwa mara na tukio la mwisho lilirekodiwa mwaka 2007.

Vifaa hivyo vya kutabiri matetemeko ya ardhi vitafungwa kuzunguka eneo la mlima huo, Ziwa Natron, Mlima Meru na hata Mlima Kilimanjaro pamoja na maeneo mengine nchini.

Lakini hatua hiyo si kwamba imetokana na matukio ya tetemeko yaliyoyakumba maeneo mengi ya nchi juzi bali ni mpango uliobuniwa na wataalamu mapema mwaka huu na kwamba kilichobaki ni utekelezaji tu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Karimu Meshaki alisema atatoa taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya mpango huo wiki hii.

Hivi karibuni Serikali ilijenga maabara kubwa kabisa ya utafiti wa kisayansi katika Chuo cha Nelson Mandela, Arusha ambayo ilizinduliwa miezi miwili iliyopita.

Serikali ya India pia ilitoa mchango wake kwa kukipatia chuo hicho kompyuta kubwa na yenye uwezo mkubwa zaidi nchini ijulikanayo kama 'Param Kilimanjaro,' ambayo pamoja na shughuli nyingine pia inatarajiwa kutumika katika tafiti za miamba, gesi asilia na pia kwenye huu mradi mpya wa kufuatilia matukio ya tetemeko la ardhi na milipuko ya volkano.



Chanzo: Habarileo

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa  FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa  Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika. Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo: 1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia. 2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti. 3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takriba...

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi. Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!! Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj.  WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert  Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI...

FRIENDSHIP QUOTES OF THE DAY MAY 26, 2018

Today I invite you to read these quotes of the day. Enjoy your day. 1.  One of the most beautiful qualities of true friendship is to understand and to be understood. ~Lucius Annaeus Seneca. 2.  Walking with a friend in the dark is better than walking alone in the light. ~Helen Keller. 3.  There is nothing on this earth more to be prized than true friendship. ~Thomas Aquinas. 4.  My best friend is the one who brings out the best in me. ~Henry Ford. 5.  It is one of the blessings of old friends that you can afford to be stupid with them. ~Ralph Waldo Emerson. 6.  The strong bond of friendship is not always a balanced equation; friendship is not always about giving and taking in equal shares. Instead, friendship is grounded in a feeling that you know exactly who will be there for you when you need something, no matter what or when. ~Simon Sinek. 7.  A friend is someone who gives you total freedom to be yourself. ~Jim Mo...

IDADI YA WATU WALIOFARIKI UGANDA YAFIKIA 33

Moto mkubwa uliowaka baada yaajali mbaya ya barabarani iliohusisha lori la mafuta, umewauwa takriban watu 33 mjini kampala Uganda. Watu wengine 30 wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia tukiohilo. Maafisa wa polisi wanasema kuwa kati ya waliofariki ni raia waliokuwa wanakimbilia eneo hilo la mkasa kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka kwa lori hilo. maafisa wa serikali walikuwa katika harakati za kutambua mili ya waliofariki baada ya wengi wao kuchomeka vibaya. Idara ya polisi imesema kuwa waliofariki waliteketea kiasi cha kutotambulika na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua miili ya waliokufa.

VITAMBULISHO VYA URAIA KUVUKIA MIPAKA KENYA, RWANDA NA UGANDA

Wananchi wa mataifa ya Rwanda, Uganda na Kenya wamepokea kwa shangwe kuanza kwa mpango wa kutumiwa kwa vitambulisho vya uraia kama cheti cha kuwaruhusu kuvuka mpaka na kuingia moja wapo wa nchi hizo.Mpango huu wa kutumia vitambulisho vya uraia kama hati ya kusafiria katika nchi hizo tatu umeanza kutumiwa rasmi tarahe Mosi Januari 2014, kufuatia makubaliano kati ya viongozi wa mataifa hayo.Mpango wenyewe unatokana na makubaliano kati ya viongozi wa nchi tatu waliofikia wakati wa mkutano uliofanyika nchini Uganda mwezi Juni mwaka jana.Pia mpango huu unalenga kurahisisha usafiri wa watu wa jumuiya katika mataifa wanachama kama awamu ya pili ya ushirikiano kati ya mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.Hata hivyo siku moja tu baada ya kuanzishwa kwa mpango wa kutumia vitambulisho vya uraia kama hati ya kuwaruhusu raia wa nchini tatu, Uganda, Kenya na Rwanda kuvuka mpaka na kuingia mojawapo ya nchi hizo sasa inaonekana mpango huo huenda ukawanufaisha watu wachache peke yake.Sio ...

CHANGES QUOTES OF THE DAY MAY 23, 2018

Hello dear reader, welcome once again. Today I have gathered the quotes concerning changes in life. I should not write more since I am not not the speaker in this category, take your time to dive in and become intellectual with full equipped knowledge from the great men of history Remember, someday it might be you. Do not rely on inspiration from friends while you are needy, VENANCE BLOG is here for you. Welcome all the time by searching Quotes. Now proceed. 1. Every great dream begins with a dreamer. Always remember, you have within you the strength, the patience, and the passion to reach for the stars to change the world. ~Harriet Tubman. 2. Change your thoughts and you change your world. ~Norman Vincent Peale. 3.  If you don't like something, change it. If you can't change it, change your attitude. ~Maya Angelou 4.  Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that...

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

Uhali gani msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG? Nakukaribisha katika darasa jipya la kufahamu mambo kadha wa kadha kama yanavyokuwa yakipigiwa kura na watu kutoka vyanzo tofauti kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, watu wenye ushawishi, majarida n.k. Basi kwa kuanza leo nakuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea. Vigezo vilivyotumika husemwa na mtandao husika unaotoa orodha hiyo. Ili kurahisisha kazi hii, mimi kama Blogger ntakuletea orodha hizi kila siku kwa lugha ya Kiswahili. Na tuanze sasa, tunaanzia Korea Kusini kuangalia waigizaji wa kiume wenye mvuto kwa mwaka 2017: # 10. Lee Byung-Hun Lee Byung-Hyun ni muimbaji, mwanamitindo na muigizaji kutokea Korea ya Kusini. Anamiliki kampuni yake ya BH Entertainment. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maigizo katika Chuo Kikuu Chung Ang. Anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kikorea na Kimandarin lakini pia ni mfuasi wa dini ya Budha. Alizaliwa Julai 12, 1972 katika jimbo la Gyeonggi Korea ya Kusini. Alianz...