Posts

Showing posts from June, 2014

QUOTES OF THE DAY JUNE 11, 2014

Image
1. Once you replace negative thoughts with positive ones, you'll start having positive results. ~Willie Nelson   2. No matter what you're going through, there's a light at the end of the tunnel and it may seem hard to get to it but you can do it and just keep working towards it and you'll find the positive side of things. ~Demi Lovato  3. Positive anything is better than negative nothing. ~Elbert Hubbard   4. I do believe we're all connected. I do believe in positive energy. I do believe in the power of prayer. I do believe in putting good out into the world. And I believe in taking care of each other. ~Harvey Fierstein  5. Positive thinking will let you do everything better than negative thinking will. `Zig Ziglar

QUOTES OF THE DAY JUNE 10, 2014

1. I think that anybody that smiles automatically looks better. - Diane Lane  2. A smile is the universal welcome. - Max Eastman 3. Remember even though the outside world might be raining, if you keep on smiling the sun will soon show its face and smile back at you. - Anna Lee 4. After every storm the sun will smile; for every problem there is a solution, and the soul's indefeasible duty is to be of good cheer. - William R. Alger 5. A smile is happiness you'll find right under your nose. - Tom Wilson 6. The real man smiles in trouble, gathers strength from distress, and grows brave by reflection. - Thomas Paine 7. Let my soul smile through my heart and my heart smile through my eyes, that I may scatter rich smiles in sad hearts. - Paramahansa Yogananda 8. A smile is the light in your window that tells others that there is a caring, sharing person inside. - Denis Waitley 9. A smile is a curve that sets everything straight. - Phyllis Dille...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: UFARANSA YAICHAPA 8-0 JAMAICA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI

Mshambulizi wa Arsenal Olivier Giroud alifunga bao na kuiongoza ''Le Blues'' kuilaza Jamaica mabao 8-0 katika mechi yao ya mwisho ya kujipima nguvu iliyochezwa siku ya Jumapili. Ufaransa ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 kufikia muda wa mapumziko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi na Karim Benzema wakimpa kocha Didier Deschamps kila sababu ya kutabasamu kabla ya kudundadunda. Matuidi na Benzema walifunga tena katika kipindi cha pili, huku bao lake Giroud na mengine mawili kutoka kwa Griezmann yakitamatisha ushindi wao. Ufaransa 8-0 Jamaica Ufaransa itakabiliana na Honduras, Uswisi na Equador katika kundi E. Kiungo cha kati wa Real Madrid Benzemaa lionyesha mchezo wa kuridhisha huku Ufaransa ikionyesha kwamba inaweza kujikimu bila Franck Ribery ambaye hatahudhuria michezo ya Kombe la Dunia kutoana na jeraha la mgongo. Hugo Lloris anaychezea Tottenham Hotspurs, Patrice Evra wa Manchester United, Mamadou Sakho wa Liverpool na Moussa Sissoko wa Newcastle walicheza mechi h...

QUOTES OF THE DAY JUNE 9, 2014

1. For anything worth having one must pay the price; and the price is always work, patience, love, self-sacrifice - no paper currency, no promises to pay, but the gold of real service. - John Burroughs 2. The key to everything is patience. You get the chicken by hatching the egg, not by smashing it. - Arnold H. Glasow 3. Our real blessings often appear to us in the shape of pains, losses and disappointments; but let us have patience and we soon shall see them in their proper figures. - Joseph Addison 4. Good character is not formed in a week or a month. It is created little by little, day by day. Protracted and patient effort is needed to develop good character. - Heraclitus 5. It is easier to find men who will volunteer to die, than to find those who are willing to endure pain with patience. - Julius Caesar 6. Never cut a tree down in the wintertime. Never make a negative decision in the low time. Never make you...

BADO HALI INATATANISHA BRAZIL KUHUSU USAFIRI: MGOMO BADO UNAENDELEA KWA KASI

Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa muda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya kazi nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja. Mahakam ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita. Maandamano mengi yamekuwa yakulalamikia hali ngumu ya usafiri lakini sasa wafanyikazi wa treni za mijini ziitwazo Metro ndio waliogoma kutaka nyongeza ya mishahara. Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.  Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo? Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

HATIMAYE CAMEROON WAPANDA NDEGE NE KUELEKEA BRAZIL BAADA YA KUONGEZEWA PESA

Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa. Wachezaji hao, almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe. Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12. Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha. Haijabainika vyema ngapi wameongezewa ndio wakakubali safari. Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'. Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

PAPA FRANCIS I AMEWAKUTANISHA MARAIS WA ISRAEL NA PALESTINA

Image
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis I amewakaribisha Rais wa Israel, Shimon Peres, na mwenzake kutoka Palestina, Mahmoud Abbas, katika maombi ya aina ya kipekee katika makao makuu ya Kanisa Katoliki la Vatican. Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya makazi yake kabla ya kuandamana naye, wakiandamana na kiongozi wa Kanisa la Orthodox, Partriarch Artholomew kwa hafla maalumu katika Medani ya Vatican. Akiongea katika hafla hiyo Papa alisema ujasiri na nguvu vinahitjika katika juhudi za kuleta amani. "Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi; Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na nguvu moyoni," Papa alisema Na katika hotuba yake Bwana Peres alisema alitakia vizazi vyote vijavyo amani ya kudumu: "Rafiki wapenzi, Nilikuwa mchanga, na sasa nimezeeka. Nilishuhudia vita, Nili...

ETI LLULU NA NANDO WA BIG BROTHER NI WAPENZII

Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe. Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu. Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo. “Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando. Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa. Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando ...

RAIS MTEULE WA MISRI EL-SISI AAPISHWA NA KUKABIDHIWA MADARAKA

Abdel-Fattah al-Sisi ameapishwa kuwa rais mpya wa Misri katika seherehe iliyofanywa kwenye mahakama makuu ya katiba mjini Cairo. Baada ya kaapishwa, Rais Sisi alikwenda ikulu kwa ajili ya sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kutoka nchi kadha. Kiongozi wa muda, Adly Mansour na Bwana al-Sisi walitia saini waraka wa kukabidhi madaraka kwake rais mpya - kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri. Rais mpya alisema hilo ni tukio la kihistoria. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi alishinda katika uchaguzi wa mwezi uliopita kwa asili-mia-97, ingawa upinzani ulisusia uchaguzi huo. Wafuasi wa Rais al-Sisi walisherehekea katika medani ya Tahrir mjini Cairo. Mfuasi mmoja wa al-Sisi, Fakhri Gamel Abdul Khaleq, alisema anatumai sherehe za leo ndio zitamaliza matatizo yaliyopita: "nampongeza Bwana rais anapoapishwa leo. Mungu ajaalie uwe mwaka wa furaha kwetu na kwa Wamisri wote. Na tunaomba Mungu atunusuru na yale yaliyotokea kabla, na tutakuwa watu wema. Mungu akipenda, kama alivosema rais, tutakuwa...

QUOTES OF THE DAY JUNE 8, 2014

1. Friendship... is not something you learn in school. But if you haven't learned the meaning of friendship, you really haven't learned anything. - Muhammad Ali 2. Don't walk behind me; I may not lead. Don't walk in front of me; I may not follow. Just walk beside me and be my friend. - Albert Camus 3.Walking with a friend in the dark is better than walking alone in the light. - Helen Keller 4. One of the most beautiful qualities of true friendship is to understand and to be understood. - Lucius Annaeus Seneca 5. A friend is someone who gives you total freedom to be yourself. - Jim Morrison 6. Love is the only force capable of transforming an enemy into friend. - Martin Luther King, Jr. 7. Lots of people want to ride with you in the limo, but what you want is someone who will take the bus with you when the limo breaks down. - Oprah Winfrey 8. Let us be grateful to people who make us ha...

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri ,Cairo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Abdel Fatah el Sisi. Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo. Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50. Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi. Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood. Chanzo: BBC

MSIBA: MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

Image
Muigizaji mkongwe hapa nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. Akithibitisha taarifa ya kifo cha Mzee Small, mwanae aitwae Mahmoud amesema mzee wake amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakati akiwa hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu. Mipango inafanyika nyumbani kwao Tabata na kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia tutaendelea kujulishana. Ni pigo lingine tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii na kadhaa majuma yaliyopita. CHANZO: KAJUNASON BLOG

QUOTES OF THE DAY JUNE 7, 2014

1. A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man. - Lana Turner 2. Any girl can be glamorous. All you have to do is stand still and look stupid. - Hedy Lamarr 3. Always remember that you are absolutely unique. Just like everyone else. - Margaret Mead 4. If the facts don't fit the theory, change the facts. Albert Einstein 5. Behind every great man is a woman rolling her eyes. - Jim Carrey 6. My fake plants died because I did not pretend to water them. - Mitch Hedberg 7. A woman's mind is cleaner than a man's: She changes it more often. - Oliver Herford 8. Do not take life too seriously. You will never get out of it alive. - Elbert Hubbard 9. I always wanted to be somebody, but now I realize I should have been more specific. - Lily Tomlin 10. As a child my family's menu consisted of two choices: ...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: MADEREVA WA UMMA WAGOMA NA KUANDAMANA BRAZIL

Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.  Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo. Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi. Awamu nyingine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana.

QUOTES OF THE DAY JUNE 6, 2014

1. Wisdom, compassion, and courage are the three universally recognized moral qualities of men. - Confucius 2. Imagination is more important than knowledge. - Albert Einstein 3. Honesty is the first chapter in the book of wisdom. - Thomas Jefferson 4. A man must be big enough to admit his mistakes, smart enough to profit from them, and strong enough to correct them. - John C. Maxwell 5. A good head and a good heart are always a formidable combination. - Nelson Mandela 6. The only true wisdom is in knowing you know nothing. - Socrates 7. Experience is not what happens to you; it's what you do with what happens to you. - Aldous Huxley 8. By three methods we may learn wisdom: First, by reflection, which is noblest; Second, by imitation, which is easiest; and third by experience, which is the bitterest. - Confucius 9. Discipline is the bridge between goals and accomplishment. - Jim Rohn 10. For beautiful eyes, loo...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: FIFA YATANGAZA IMANI KUHUSU MICHUANO HIYO BRAZIL

Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa amesema kuwa ana imani kuwa kombe la dunia nchini Brazil litakuwa na ufanisi mkubwa. Bwana Sepp Blatter ametoa wito kwa raia wa Brazil wajitolee vilivyo kusaidia kufanikisha mchezo huo mwaka huu. Matamshi ya Bwana Blatter yamekuja huku hofu ikielezewa mjini Sao Paulo juu ya msongamano mkubwa wa watu na magari kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa shirika la reli. Maafisa wakuu wa Fifa wenyewe walikwama katika foleni ndefu ya magari barabarani. Usafiri huo unatarajiwa kutatizika zaidi kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa wafanyikazi hao na serikali.  Orodha kamilifu ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Dunia imetolewa. Majina ya makocha 32 ambao watasimamia mechi za mashindano hayo, pia majina ya wachezaji 736 watakaoshiriki mechi hizo zitakazochezwa kati ya Juni 12 hadi Julai 13 zimetangazwa.. Taarifa zaidi iliyotolewa ni kuwa timu zimepunguza idadi ya wachezaji, majeraha kukaguliwa na hali ya afya ya wachezaji ku...

WAHUBIRI INJILI WAGEUKA KUWA WASHAMBULIAJI NIGERIA

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wameshambulia wanakijiji karibu na mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwaua watu 45. Walioponea kifo waliambia BBC kwamba washambuliaji hao walijidai kuwa walikuwa wamekuja kuwahubiria wanakijiji kabla ya kuanza kuwafyatulia risasi kiholea. Wakati huohuo,wakazi pamoja na maafisa wakuu wanasema kuwa watu 200 waliuawa katika mashambulizi tofauti mapema wiki hii. Mji wa Maiduguri na vitongoji vyake, haujaathirika sana na mashambulizi tangu kutangazwa kwa sheria ya hali ya hatari mwaka mmoja uliopita. Maeneo ya mashinani ndio sasa hulengwa kwa mashambulizi Serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na shinikizo ndani ya nchi na kimataifa kuongeza juhudi za kukabiliana na kundi la Boko Haram tangu liwateke nyara wasichana zaidi ya miambili wa shule mwezi Aprili. Kundi hilo limekuwa likiendesha harakati zake tangu mwaka 2009 katika juhudi za kudai uongozi wa kiisilamu. Maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi mbali m...

QUOTES OF THE DAY JUNE 5, 2014

1. Success is not final, failure is not fatal: it is the courage to continue that counts. - Winston Churchill 2. Coming together is a beginning; keeping together is progress; working together is success. - Henry Ford 3. Success consists of going from failure to failure without loss of enthusiasm. - Winston Churchill 4. In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. - Bill Cosby 5. The price of success is hard work, dedication to the job at hand, and the determination that whether we win or lose, we have applied the best of ourselves to the task at hand. - Vince Lombardi 6. Always be yourself, express yourself, have faith in yourself, do not go out and look for a successful personality and duplicate it. - Bruce Lee 7. Try not to become a man of success, but rather try to become a man of value. - Albert Einstein 8. Take up one idea. Make that one idea your life - think of it, dream of it, liv...

MUME WA FROLA MBASHA ASEMA NI VIGUMU SANA NDOA YAO KUFIKIA MUAFAKA TENA

BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi. Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke. Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara. “Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo. TUJIUNGE NA MBA...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ENGLAND YATOKA SARE NA ECUADOR 2-2

Katika mechi za kirafiki kwa maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, England ilitoka sare ya 2 - 2, dhidi ya Ecuador katika mechi iliyochezwa huko Miami. Timu ya England iliongozwa na Frank Lampard. Raheem Sterling ambaye huchezea klabu ya Liverpool, alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United. Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki itakayofuata.  Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda mapumziko.  Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.

RAIS MTEULE WA MISRI KUAPISHWA JUMAPILI

Abdel Fatah al-Sisi ambaye amempinduwa kiongozi wa kwanza aliechaguliwa kwa njia ya demokrasia nchini Misri ataapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Jumapili baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais wiki iliopita. Tume ya uchaguzi hapo juzi imesema Sisi alishinda kwa asilimia 96.91 ya kura sawa na asilimia 47.5, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kumpinduwa Mohamed Mursi wa itikadi kali za Kiislamu. Ushindi wake huo mkubwa dhidi ya mpinzani pekee kiongozi wa sera za mrengo wa shoto Hamdeen Sabahi ulikuwa haukutiliwa mashaka kabisa kutokana na kupongezwa na watu wengi kwa jemedari huyo mkuu mstaafu kukomesha utawala wa mwaka mmoja wa Mursi uliowagawa wananchi miezi kumi na moja iliopita. Sisi ataapishwa saa moja na nusu asubuhi hapo Jumapili katika baraza kuu la Mahakama Kuu ya Kikatiba.Sherehe za kuapishwa kwake zitahudhuriwa na rais wa kipindi cha mpito Adly Mansour, Waziri Mkuu Ibrahim Mahlab na baraza lake la mawaziri,Imamu Mkuu Ahmed al- Tayeb wa Taasisi kuu ya Kiislamu nchini h...

KESI YA UMILIKI WA NYIMBO ZA BOB MARLEY YAMALIZIKA

Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London. Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao. Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena. Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992. Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo. Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.

DICAPRIO' JACK WA TITANIC' NA PARIS HILTON WASUSIA KUONEKANA KATIKA KIPINDI CHA KIM KADARSHIAN

Muigizaji maarufu nchini Marekani, Leonard DiCaprio au maarufu kama 'Jack' aliyeigiza katika muvi ya Titanic, amekata kurekodiwa na kipindi cha Kim Kadarshian 'Keeping Up With the Kadarshians' walipokuwa katika pati ya majira ya joto Jumapil mchana. "Leo hakutaka kurekodiwa kwa ajili ya kipindi cha Kim na hakuwasili mpaka pale shughuli za kurekodi zilipokwisha" alisema mpasha habari mmoja. Pia, Paris Hilton ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Kim, naye hakupenda kuonekana katika kipindi hicho ambaye naye ameanzisha fani yake kama DJ.

KOCHA NOOIJ ASEMA HATOPANGUA KIKOSI CHA TAIFA STARS

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’, Mholanzi Mart Nooij amesema kamwe hatakifanyia marekebisho kikosi chake kilichotinga raundi ya pili ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa Afrika kwa kuifunga Zimbabwe jumla ya mabao 3-2. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salam, Stars ilipata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji wao Zimbabwe Jumapili iliyopita Jijini Harare na kukata tiketi ya kucheza raundi hiyo ya pili na sasa itakutana na Msumbiji Julai 18. Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Harare juzi usiku, kocha huyo alisema: “Mechi na Zimbabwe ilikuwa nzuri na ngumu kwetu, lakini nawapongeza vijana wangu walicheza kwa kujituma na kupata matokeo ambayo yametupeleka hatua nyingine, tuna muda mrefu kabla ya kucheza mechi inayofuata nitatumia muda huu kukirekebisha kikosi changu lakini siwezi kukibadilisha,” alisema Nooij. Akiuzungumzia mchezo wao unaofuata dhidi ya Msumbiji aliyowahi kuifundis...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: BLATTER AWASILI BRAZIL NA KUKUTANA NA RAIS WA NCHI HIYO, DILMA ROUSSEFF

Rais wa FIFA, Joseph S. Blatter amekutana na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff huko Palacio do Planalto, Brasilia. Kwa msisimko wa kihistoria wa kombe hilo ambalo litatolewa kwa bibngwa wa dunia, kombe hilo limetolewa na Blatter na Cafu aliyekuwa nahodha wakati Brazil ilipotwaa kombe hilo mwaka 2002.  "Nilishasema kabla ya kuja Brazil, kwa mara ya kwanza itakuwa ni kuonana na Rais wa nchi hii. Hii yote ni kwa heshima na taadhima" alisema Blatter kabla ya kuanza kwa sherehe ambapo Rais Rousseff aliinua juu kombe la dunia ambalo huguswa na Marais na mabingwa pekee. "Ni matumaini yangu na Wabrazil wenzangu zaidi ya milion 200, wanategemea hapo tarehe 13 Julai zaidi ya watu 23 wataweza kuligusa kombe hili" alisema Rousseff.Siku 10 kabla ya michuano kuanza. Rais Dilma alishaitisha mkutano huko Brazil na wakuu wa majimbo kujadili juu ya mechi ya maandalizi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia huko Palacio do Planato katika dimba la Arena de Sao Paulo. Baada ya...

QUOTES OF THE DAY JUNE 1, 2014

Education is what survives when what has been learned has been forgotten. - B. F. Skinner Love Quote of the Day: I love you the more in that I believe you had liked me for my own sake and for nothing else. -John Keats Art Quote of the Day: Every child is an artist. The problem is how to remain an artist once we grow up. -Pablo Picasso Nature Quote of the Day: If the skies fall, one may hope to catch larks. -Francois Rabelais Funny Quote of the Day: Only two things are infinite, the universe and human stupidity, and I'm not sure about the former. -Albert Einstein