Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi lisilofahamika la kigaidi.Waziri wa habari nchini humo Lambeart Mende amesema kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya Taifa.Amesema kuwa kulikuwa na matukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara .Mashambulizi haya yametokea wakati Rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchini humo.Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari kwa raia wake kutofanya safari za ndani ya mji wa Kinshaasa hadi hali itakapodhibitiwa Zaidi.
MTU MMOJA AUAWA KATIKA MAPIGANO CAIRO
Mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya wanafunzi wanaokiunga mkono Chama cha Muslim Brotherhood na wakazi jijini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.Maafisa mjini humo wamesema kuwa mwanafunzi mmoja alipoteza maisha baada ya pande hizo mbili kushambuliana kwa risasi katika mji wa Nasr.Tukio hilo limetokea siku moja baada ya Serikali ya Misri kukitaja chama cha Muslim Brotherhood kuwa kundi la kigaidi.Katika tukio jingine, watu watano wamejeruhiwa kwa bomu lililokuwa karibu na basi moja mjini Nasr, bomu hilo lilitegwa na kulipuka wakati basi hilo lilipokuwa likipita karibu na eneo lilipotegwa bomu.Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo.Siku ya alhamisi, takriban wafuasi 16 wa chama cha Muslim Brotherhood walikamatwa wakishutumiwa kujihusisha na kundi hilo linalodaiwa kuwa la kigaidi.Miongoni mwa waliokamatwa ni Mtoto wa Naibu Kiongozi wa Chama hicho.Shirika la Habari la Misri, Mena limesema Watu hao walikamatwa na kushutumiwa kuchochea machafuko na mapigano dhidi ya Jeshi na Polisi.Siku ya jumanne, Watu 16 waliuawa na zaidi ya 100 walijeruhiwa katika shambulio la bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika jengo la usalama mjini Mansoura, Maafisa wameeleza.Serikali imesema kuwa Muslim Brotherhood inahusika na shambulio hilo, madai ambayo yamepingwa vikali na Chama hicho.Kundi lenye uhusiano na Al Qaeda, Ansar Beit al-Maqdis (washindi wa Yerusalemu) walikiri kuhusika na shambulio hilo.
WANAJESHI WAUAWA KWA BOMU SOMALIA
Milipuko imekuwa ikijitokeza mara kwa mara nchini Somalia. Takriban wanajeshi watano na afisa wa jeshi wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu nchini Somalia mashuhuda wameeleza.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo. Sababu ya mlipuko huo haijafahamika majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.
Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo. Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo. Sababu ya mlipuko huo haijafahamika majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.
Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo. Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.
96% WAHITIMU DARASA LA SABA KUJIUNGA SEKONDARI
ASILIMIA 96.15 ya wanafunzi wa darasa la saba waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na kufaulu, ndio waliochaguliwa kujiunga na sekondari za serikali.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwamba jumla ya wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani huo ndio watakaoanza kidato cha kwanza mwakani.Alisema wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na kwamba waliochaguliwa wameongezeka kwa asilimia 31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.Kwa mujibu wa matokeo ya mtihani mwaka huu, alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 244 huku ya wasichana ikiwa ni 241 kati ya alama 250 ambapo mwaka jana alama ya juu ilikuwa 237.“Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana 218,093 na wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938 waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka jana,” alisema Sagini.Kuhusu udanganyifu katika mtihani, Katibu Mkuu alisema takwimu zinaonesha waliofutiwa matokeo kutokana na udanganyifu imepungua mwaka huu kwa kuwa na wadanganyifu 13 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo waliofutiwa walikuwa 219.Alisisitiza msimamo wa Serikali kuwachukulia hatua stahiki watendaji watakaobainika kujihusisha na udanganyifu katika mitihani.“Vitendo hivyo vinatoa taswira mbaya kwa Taifa na kufanya watoto wetu wawe tegemezi zaidi kuliko kujituma na kujibidiisha katika masomo yao,” alisema na kuwataka walimu, wazazi na jamii kwa jumla kujiepusha na vitendo hivyo.Pamoja na kushukuru walimu, walimu wakuu, kamati za shule, waratibu wa elimu kata, viongozi wa halmashauri, sekretarieti za mikoa na wadau wa elimu nchini kwa ushirikiano wao wa kusimamia elimu, aliasa waliochaguliwa kutumia fursa hiyo vizuri.Aliagiza walimu na watendaji wa elimu katika ngazi zote kuongeza bidii katika ufundishaji, usimamizi na ufuatiliaji wa kutoa elimu ili kuinua ubora wa elimu nchini.Alitaka pia ukamilishaji majengo na mazingira ya kupokea wanafunzi wote waliochaguliwa na kuhakikisha wanaandikishwa, wanahudhuria na kubaki shuleni hadi watakapohitimu masomo yao ya sekondari.“Naziagiza halmashauri zilizobakiza wanafunzi 16,482 katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 412 ili kuwezesha wanafunzi hao kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo Machi.Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika Septemba 11 na 12 kwa kutumia teknolojia mpya ya OMR ambapo mitihani ilisahihishwa kwa kompyuta.Jumla ya wanafunzi 867,983 walisajiliwa kufanya mtihani, wasichana wakiwa 455,896 ambapo 844,938 ndio waliofanya mitihani hiyo huku 23,045 wakikosa kuifanya kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za utoro, vifo na ugonjwa.
JIJI LA MBEYA KUKUSANYA BILIONI 64.8 MWAKA WA FEDHA UJAO
JUMLA ya shilingi bilioni 64.8 zinatarajiwa kukusanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mwaka wa fedha 2014/2015.Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Musa Zungiza alipotoa taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kujadili bajeti hiyo.Zungiza alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 11.3 sawa na asilimia 17.5 zitakusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani vya halmashauri wakati michango ya nguvu ya wananchi itakuwa bilioni moja sawa na asilimia 1.5.Kutoka serikali kuu, halmashauri inatararajia kupokea Sh bilioni 37.7 sawa na asilimia 58 kwa ajili ya mishahara ya watumishi, Sh bilioni 3.4 sawa na asilimia tano kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh bilioni 11.4 sawa na asilimia 18 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Zungiza alisema pia halmashauri inatarajia kutumia jumla ya Sh bilioni 64.8 katika mwaka huo wa fedha kwa ajili ya mishahara ya watumishi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida.Hata hivyo, baadhi ya madiwani akiwemo Meya, Athanas Kapunga na Diwani wa Kata ya Sinde, Fanuel Kyanula walihoji hatua ya miradi ambayo ujenzi wake haujakamilika ya Soko la Mwanjelwa na Hosteli iliyopo Sokomatola, kuingizwa katika matarajio ya kuwa sehemu ya vyanzo vya ndani vya mapato.Diwani Kyanula alisema ni kwa takriban miaka mitatu sasa, miradi hiyo imekuwa ikiingizwa katika bajeti kwa matarajio kuwa itakamilika kwa wakati na kuanza kuliingizia jiji fedha, lakini matokeo yake imekuwa ni kuzua hoja za ukaguzi.
AFUNGWA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA KAKA YAKE
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Nzega, Tabora, imemhukumu Juma Lufunga (26) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Joseph Ngomelo alisema Lufunga (26) ametiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali na hivyo kustahili kifungo cha maisha gerezani ili adhabu yake iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za aina hiyo.Alisema vitendo vya ulawiti wa watoto wadogo, vimekuwa vikiongezeka kila kukicha na kusababaisha jamii ishindwe kufanya kazi zingine za maendeleo kwa hofu juu ya watoto wao kwa kuwa watu wazima wamekuwa ni tatizo hasa wanaume.Kabla ya hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo Juma Lufunga akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na yeye kuwa ni mwathirika wa virusi vya Ukimwi, hata hivyo mtuhumiwa huyo alipoombwa vyeti vya uthibitisho hakuweza kuwasilisha mahakamani.Awali, Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 24 mwaka 2012 majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Mwanihara, Lufunga alimlawiti mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.Melito alidai taarifa ya daktari ilithibitisha unyama aliofanyiwa mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.
APIGWA HADI KUFA KATIKA FUMANIZI
MTU mmoja m kulima na mkazi wa eneo la Kumsenga wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, aliyefahamika kwa jina la Yusuph Pascal, ameuawa kwa kupigwa na vitu mbalimbali katika tukio linalodaiwa kuwa ni fumanizi la mapenzi.Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraisser Kashai alisema mjini hapa kwamba mtuhumiwa huyo wa fumanizi, aliuawa mwanzoni mwa wiki hii.Alisema baada ya kifo chake, mume wa mwanamke aliyefumaniwa kwa kushirikiana na watu wengine, waliuchukua mwili wa marehemu na kuutupa eneo la Mnarani mjini Kasulu.Kufuatia tukio hilo, kamanda huyo alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo, wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji ya mkulima huyo.Kashai aliwataja watu waliokamatwa kwenye tukio hilo kuwa ni watu watatu wa familia moja, ambao ni Augustino Adrian, Laurent Adrian na Peter Adrian, ambao ni wamiliki wa nyumba yalipotokea mauaji.Aliwataja wengine waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kuwa Mihosho Hamza, ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa akiwa ni mpangaji katika nyumba yalikotokea mauaji na Raymond Shirima.Akisimulia kuhusu tukio, Mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoa Kigoma, David Kisusi alisema awali marehemu akiwa katika nyumba ambayo mwanamke aliyefumaniwa naye alikuwa akiishi, alivamiwa na watuhumiwa, ambao walimpiga na vitu vizito na kufariki.Alisema baada ya kuona kuwa mtuhumiwa huyo wa fumanizi ameuawa, mume wa mwanamke huyo na watuhumiwa wengine wanne, waliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuutupa eneo la Mnarani ili kupoteza ushahidi.Alisema polisi walipofika eneo ambalo mwili huo wa marehemu ulikuwa umetupwa, walianza uchunguzi wao na kubaini kuwa ulitupwa hapo baada ya kuuawa eneo lingine.Ndipo walipofuatilia michirizi ya damu hadi katika nyumba hiyo na kukuta katika moja ya vyumba hivyo, kuna eneo limemwagiwa mchanga mwingi ili kuficha damu hiyo ya marehemu.
JELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA
Wakazi wawili wa vijiji vya Nyabisaga Kata ya Pemba wilayani Tarime mkoani Mara, Mhoni Chacha Ng’wena (25) na Isack Magawi Meng’anyi (30), wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tarime.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ukiongozwa na Inspekta Usu, George Lutonja kwamba washitakiwa walitenda kosa la unyang’anyi wa silaha.Alisema Mahakama imeridhika na ushahidi, ulioambatana na vielelezo vya mlalamikaji, vilivyokamatwa kwa watuhumiwa hao, vikiwemo baiskeli, simu ya mkononi, viatu na tochi.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Usu Lutonja alidai kuwa washitakiwa hao pamoja Januari 3, mwaka huu saa 12 alfajiri, wakiwa na silaha za jadi za mapanga na marungu walivamia na kuingia ndani ya nyumba ya Selestin Omahe, mkazi wa Sirari na kumshambulia na familia yake na kupora vitu vya ndani, vikiwemo baiskeli aina ya Phoenix, simu ya mkononi, viatu na tochi, vyote vyenye thamani ya Sh 284,000.Alidai baada ya tukio hilo, mlalamikaji Omahe alipiga yowe, kuomba msaada na majirani, ambao walitokea pamoja na polisi, waliokuwa doria eneo hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa kukamata washitakiwa hao wakiwa na mali za mlalamikaji.
Baada ya kukamatwa, washitakiwa walifikishwa kwenye vyombo vya sheria, ambapo upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne na vielelezo, vilivyokamatwa kwa washitakiwa wakati wa tukio hilo. Washitakiwa hao waliomba wasamehewe. Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa. Hakimu Kilimi alisema anawahukumu kwenda jela miaka 30 kila mmoja ili iwe fundisho kwa watu wenye tamaa ya kupora mali za watu.
Chanzo: Habari Leo
WATU SABA WAFARIKI PWANI NA NJOMBE KATIKA MATUKIO TOFAUTI
WATU saba wamekufa katika mikoa ya Njombe na Pwani katika ajali za gari na mtoto kutumbukia kwenye ndoo.Kutoka Njombe, mtoto wa mwaka mmoja, Pendo Mbena amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alisema mtoto huyo alikufa juzi saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Igoma wilayani Njombe.Akielezea tukio hilo, Ngonyani alisema Upendo alikufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo iliyokuwa jikoni baada ya kuachwa na mama yake, Agness Mbena (28) aliyekwenda kuchota maji.Katika tukio lingine, Ngonyani alisema mtoto wa miaka mitatu, Kelvin Kyando, mkazi wa Mtalawe amekufa baada ya kugongwa na pikipiki.Alisema ajali hiyo ilitokea mtaa wa Posta, Njombe Mjini baada ya pikipiki yenye namba za usajili T 112 CLX aina ya Fekon, mali ya Kelvin Chaula (21) kumgonga mtembea kwa miguu, mwanafunzi, Anthon Bruno (12) aliyekuwa amembeba Kelvin.“Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa pikipiki. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mwendesha pikipiki kwani hakuweza kuchukua tahadhari kwani aneo hili lilikuwa na watoto wengi waliokuwa karibu na barabara,” alisema.Mkoani Pwani, watu wanne wamekufa katika matukio mawili tofauti, wakiwemo watu watatu waliopoteza maisha kwa ajali ya gari.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilitokea saa tano usiku eneo la Vigwaza, wilayani Bagamoyo baada ya Fuso lenye namba za usajili T 775 CHX kugongana na lori lenye namba za usajili T 627 ANA/T 386 ACE.Alitaja waliopoteza maisha kuwa ni dereva Kalista Mwigeni (23), mkazi wa Ilula Iringa, Gerald Muhanga (umri wake kati ya miaka 23-25) utingo wa Fuso, na Deseselia Daudi (50) mkulima wa Morogoro aliyekuwa abiria kwenye lori.Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Noah Msalu (40), mkazi wa Iringa aliyekuwa amekodisha Fuso na Alani Philipo (60), mkazi wa Kipawa jijini Dar es Salaam ambaye ni dereva wa lori Katika tukio lingine, Matei alisema siku ya Jumanne saa 12 asubuhi, Mgaza Mbulu (61) mkazi wa Kijiji cha Kibindu, alikutwa amejinyonga juu ya mti kwa kutumia kamba.Alisema mwili wa marehemu ambaye alikuwa akiishi kijijini hapo bila ndugu wa karibu, ulikabidhiwa kwa viongozi wa kijiji baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari. “Marehemu hakuacha ujumbe wowote wa kueleza sababu za kujitoa maisha na upelelezi unaendelea,” alisema.
WALAJI WA NGURUWE KUPATA KIFAFA

Akizungumza na gazeti la Habari Leo hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo. Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.
“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.
Aidha, alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu. Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao. Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule.
Chanzo: Habari Leo
CHRISTMAS PHOTOS
QUOTES OF THE DAY/QUOTES FOR CHRISTMAS 2013
1. He who has not Christmas in his heart will never find it under a tree. -Roy L. Smith
2. Christmas is not a time nor a season, but a state of mind. To cherish peace and goodwill, to be plenteous in mercy, is to have the real spirit of Christmas. -Calvin Coolidge
3. Christmas, my child, is love in action. Every time we love, every time we give, it's Christmas. -Dale Evans
4. Christmas waves a magic wand over this world, and behold, everything is softer and more beautiful. -Norman Vicent Peale
5. We consider Christmas as the encounter, the great encounter, the historical encounter, the decisive encounter, between God and mankind. He who has faith knows this truly; let him rejoice. -Pope Paul VI
6. Christmas... is not an external event at all, but a piece of one's home that one carries in one's heart. -Freya Stark
7. It's true, Christmas can feel like a lot of work, particularly for mothers. But when you look back on all the Christmases in your life, you'll find you've created family traditions and lasting memories. Those memories, good and bad, are really what help to keep a family together over the long haul. -Caroline Kennedy
8. Christmas isn't a season. It's a feeling. -Edna Ferber
9. Christmas in Bethlehem. The ancient dream: a cold, clear night made brilliant by a glorious star, the smell of incense, shepherds and wise men falling to their knees in adoration of the sweet baby, the incarnation of perfect love. -Lucinda Franks
10. I'm sure most of us remember being a kid and you have all of this endless time where two weeks before Christmas feels like ten years. I used to go to bed to try and go to sleep to try and make it go faster. -Andrea Arnold
11. Christmas is a time of year that's so romantic. -Katharine McPhee
12. Christmas makes me happy no matter what time of year it comes around. -Bryan White
13. There's nothing sadder in this world than to awake Christmas morning and not be a child. -Emma Bombeck
14. Christmas is a holiday that persecutes the lonely, the frayed, and the rejected. -Jimmy Cannon
15. I just think that it's strong and it's important that we recognize what the Christmas season is about; it's about the birth of our Savior, and there's a lot of pressure today to be politically correct ,but people are realizing, too, that you have to be open to express your faith what you want believe. -Joel Osteen
16. I've always loved Christmas and that's not really gone away from me from being a child to now. It's always a magical time and I'm unashamed in my love for Christmas. -Martin Freeman
17. I like indoor Christmas trees. And I like people who decorate their homes with lights and all that crap. I think it's a healthy outlet for them. If they weren't covering their lawns with twinkling lights, they'd be doing something that was really, really. -Lewis Black
18. You can't allow the forces of political correction to shut you up. I mean, why are people afraid to say, 'Merry Christmas?' Give me a break. If people don't like it, yeah, they can go do something else. -Ben Carson
19. Christmas and the holidays are the season of giving. It's a time when people are more kind and open-hearted. -Gisele Bundchen
20. If you pray enough for things, I am proof that they can happen. I feel like a kid on Christmas day now, every day. It's something I have wanted for a long time and I am as happy as anyone to be here. It is great to be back at my first love. -Robbie Fowler
SALAAMU ZA SIKUKUU YA KRISMASI
Venance Blog inawatakieni HERI YA KRISMAS. Mpendwa msomaji wa blog hii, leo Wakristu duniani kote wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwokozi wao, Yesu Kristu aliyezaliwa takribani miaka 2000 iliyopita. Venance Blog inakukumbusha katika sikukuu hii kama ni mnywaji usilewe sana na pia ukumbuke ugonjwa hatari wa UKIMWI hasa siku kama hii ya leo kuwa makini sana, pia tuwasaidie watoto wetu au wadogo zetu kuvuka mabarabara salama huko mitaani kwetu. Krismasi ni siku ya furaha na kuoneshana upendo, hivyo tupendane wote kwa pamoja.
HERI YA KRISMAS NA KRISMAS YENYE FURAHA SHEREHEKEA KWA AMANI NA UPENDO!!!
CHRISTMAS GREETINGS

Venance Blog is grateful to wish you a MERRY CHRISTMAS. Venance Blog wishes you a nice celebration, one thing to remember is to keep our national peace and avoiding other evils, if you drink don't take too much remember there is HIV/AIDS so be careful help the children to cross the road along the streets because its a day for happiness and loving each other..
MERRY CHRISTMAS & HAPPY CHRISTMAS!!!
MAANDALIZI MEMA YA SIKUKUU YA KRISMAS
Kwanza namshukuru Mungu toka tukiwa wadogo mpaka sasa anaendelea kutulinda. Uongozi mzima wa Venance Blog tunawatakieni maandalizi mema ya Krismas hapo kesho, wale wa kanisani tukafurahi kwani bwana atazaliwa. Msali salama katika misa za mkesha kubwa zaidi kudumisha amani na usalama kuanzia leo mpaka sikuku itakapoisha. MAANDALIZI MEMA YA KRISMAS!!!