VIFAHAMU VITABU 20 VYA KWANZA KUANDIKWA KATIKA MFULULIZO WA WAANDISHI AFRIKA

1. Things Fall Apart-Chinua Achebe
2. Burning Grass-Cyprian Ekwensi
3. No Longer at Ease-Chinua Achebe
4. Zambia Shall Be Free-Kenneth Kaunda
 5. People of the City-Cyprian Ekwensi
 6. Mine Boy-Peter Abrahams
 7. Weep Not Child-Ngugi Wa Thiong'o
8. A book of African Verse-kimehaririwa na John Reed & Clive Wake
 9. Modern African Prose-kimehaririwa na Richard Rive
10. Equiano's Travels-Olaudah Equiano
11. One Man, One Matchet-T. M. Aluko
12. The African-William Conton
13. Mission to Kala-Mongo Beti
14. Quartel-kimeandikwa na Richard Rive, Alex La Guma, Alf Wannenburgh & James Matthews
15. Origin of East Africa-kimehaririwa na David Cook
16. Arrow of God-Chinua Achebe
17. The River Between-Ngugi Wa Thiong'o
18. The Imprisonment of Obatala-Obotunde Ijimere
 19. Lokotown-Cyprian Ekwensi
 20. Child of Two World-Mugo Gatheru

KIGOGO WA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND

Stori: Shakoor Jongo
Yule kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni 48 ziliteketea.“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwaKajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.Baada ya kujazwa data, Risasi Jumamosi lilijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond: “Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One.





 Chanzo: Global Publishers Ltd

VITAMBULISHO VYA URAIA KUVUKIA MIPAKA KENYA, RWANDA NA UGANDA

Wananchi wa mataifa ya Rwanda, Uganda na Kenya wamepokea kwa shangwe kuanza kwa mpango wa kutumiwa kwa vitambulisho vya uraia kama cheti cha kuwaruhusu kuvuka mpaka na kuingia moja wapo wa nchi hizo.Mpango huu wa kutumia vitambulisho vya uraia kama hati ya kusafiria katika nchi hizo tatu umeanza kutumiwa rasmi tarahe Mosi Januari 2014, kufuatia makubaliano kati ya viongozi wa mataifa hayo.Mpango wenyewe unatokana na makubaliano kati ya viongozi wa nchi tatu waliofikia wakati wa mkutano uliofanyika nchini Uganda mwezi Juni mwaka jana.Pia mpango huu unalenga kurahisisha usafiri wa watu wa jumuiya katika mataifa wanachama kama awamu ya pili ya ushirikiano kati ya mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.Hata hivyo siku moja tu baada ya kuanzishwa kwa mpango wa kutumia vitambulisho vya uraia kama hati ya kuwaruhusu raia wa nchini tatu, Uganda, Kenya na Rwanda kuvuka mpaka na kuingia mojawapo ya nchi hizo sasa inaonekana mpango huo huenda ukawanufaisha watu wachache peke yake.Sio raia wote wa Uganda , Kenya au Rwanda wanafahamu hayo . Watu wengi nchini Rwanda bado waliwasili katika mipaka ya nchi hiyo wakiwa wamejihami kwa Pasipoti zao ili waweze kuruhusiwa kuvuka mpaka na kuingia katika nchi jirani. Hali ni vivyo hivyo nchini Uganda.Hata hivyo baadhi ya watu wanahisi ingekuwa vyema kama mpango huu pia ungewanufaisha raia wa Burundi na Tanzania.Kwa sasa ni raia wa Rwanda na Kenya peke yao ambao wana vitambulisho vya kitaifa ikimaanisha kuwa raia wa Uganda watalazimika kutumia kadi zao za kupigia kura hadi taifa hilo litakapoanza kutoa vitambulisho vya uraia.

MAZUNGUMZO YA AMANI KUHUSU SUDAN KUSINI YAANZA ADDIS ABABA

Mazungumzo ya kupatanisha pande mbili zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita, yameanza mjini Addis Ababa Ethiopia.Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje nchini Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika Mashariki wananuia kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota kwa takriban wiki tatu.Hata hivyo mazungumzo ya ana kwa ana yangali kuanza kati ya pende zinazozozana yangali kuanza.Waakilishi kutoka pande zinazozozana wanakutana na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa vingozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa ana.Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais Salva Kiir na yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais Riek MacharWakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita. Chanzo: BBC Swahili

MADAGASCAR YAPATA RAIS MPYA

Maafisa nchini Madagascar wanasema kuwa matokeo ya mwanzo mwanzo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Disemba, yanaonyesha mshindi kuwa waziri wa zamani wa fedha Hery Rajaonarimampianina.Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Hery Rajaonarimampianina alishinda asilimia hamsini na tatu (53%) ya kura zilizopigwa.Mshindani wake, Jean Louis Robinson anasema kuwa uchaguzi ulikumbwa na wizi wa kura na sasa anasema sharti shughuli ya kuhesabu kura irejelewe.Uchaguzi huo ulikuwa mpango wa kurejesha utulivu kwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika miaka minne iliyopita.Bwana Rajaonarimampianina alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, Rais wa zamani Andry Rajoelina. Chanzo: BBC Swahili

DIAMOND AISIFIA NGOZI YA WEMA ASEMA INA MVUTO NA INANG'ARA KULIKO KITU CHOCHOTE

Kweli hii ni 2014! Diamond aisifia ngozi ya Wema, adai ina mvuto na ina mng’aro kuliko kitu chochote.!“Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani, ameacha kabisa kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla.”Hiyo ni kauli ya staa aliyetikisa mwaka 2013 bwana Diamond Platnumz aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti maarufu la michezo nchini hivi karibuni. Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na Wema ipo mbioni kutimia.“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.” alisema Diamond.




Chanzo: Bongo Movies

ACHINJWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MKAZI wa Kijiji cha Kakese-Mkwajuni, wilayani Mpanda, Shoma Salum (78) ameuawa kwa kuchinjwa kwa kile kinachodaiwa ni kutokana na imani za kishirikina.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema mauaji hayo yalifanyika Desemba 29 , mwaka jana saa 2:30.Alikutwa nyumbani kwake mwili ukiwa na majeraha makubwa sikioni na kichwani. Mwanamke huyo inadaiwa alikuwa mganga wa kienyeji na mfinyanzi maarufu wa vyungu.Kwa mujibu wa Kamanda, siku moja kabla ya tukio, akiwa kwenye shughuli hizo, jirani na nyumbani kwake, walifika vijana wawili waliotajwa ni Shigela Majinja (25) na Mhoja Shilinde (18). Inadaiwa vijana hao ambao ni wakazi wa kijijini hapo.Walifika kwa kwa mama huyo wakijifanya kuwa ni wateja wake, ambapo walikuwa wakiulizia bei ya vyungu. Pia, walimwomba awasaidie kuwapatia tiba ya kienyeji .“Ndipo vijana hao walipoanza kumhoji juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutaka kujua mahali , alikokuwa akiishi na chumba alichokuwa akilala na alikuwa akilala na nani. Inadaiwa aliwajibu vijana hao kwa ufasaha bila kuwa na shaka nao huku mazungumzo hayo yakiwa yanasikilizwa kwa siri na Tausi Mlitoni, ambaye naye alikuwa karibu na eneo hilo ,” alisema Kamanda.Kwa mujibu wa Kamanda, Desemba 29 saa 2:30 asubuhi mke wa Lameck Mboka, aitwaye Zamda Militone, baada ya kuona mama mkwe amechelewa kuamka, alienda na kujaribu kufungua mlango wa chumba chake.Lakini, alibaini kuwa kilikuwa kimefungwa kwa nje. Kidavashari alisema Zamda alipofungua mlango huo wa chumba cha mama mkwe wake na kuingia ndani , alimkuta mama akiwa ameuawa.Kamanda alisema watu watatu wanashikiliwa kwa mahojiano, nao ni Majija, Shilinde na Masanja Ngasa (31), wote wakazi wa kijijini hapo. Watuhumiwa wengine wanne wanaendelea kusakwa baada ya kukimbia kusikojulikana. Chanzo: Habari Leo

EYMAEL: NIPENI YANGA NIIUE AL-AHLY

KOCHA Luc Eymael ambaye tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Yanga, ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa anaijua vizuri Klabu ya Al-Ahly ya Misri na endapo watampatia kibarua hicho, atawasaidia kuwang’oa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya mtandao, Eymael ambaye ni raia wa Ubelgiji, alisema amefanya mazungumzo ya awali na mmoja wa viongozi wa Yanga kupitia barua pepe, ambapo alisema kama klabu hiyo itampatia ajira hiyo hana wasiwasi na uwezo wake katika kuwang’oa Al-Ahly ambao Yanga inatarajia kukutana nao raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itaanza michuano hiyo dhidi ya timu ya Comoronize ya Visiwa vya Comoro inayotajwa kuwa ni dhaifu na baada ya hapo itakuwa na kibarua kizito dhidi ya wababe hao wa Misri. Eymael aliyezaliwa miaka 54 iliyopita katika mji mdogo wa Tongeren, Ubelgiji alisema hajajua Yanga inaundwa na nyota wenye uwezo kiasi gani lakini anachoweza kuwaambia viongozi wa klabu hiyo ni kwamba anazijua timu nyingi hasa Wamisri hao ambao tayari wameshapata pigo kubwa kwa kuondokewa na nyota wao wawili muhimu akiwemo mkongwe Mohamed Aboutrika aliyetangaza kutundika daluga Desemba mwaka jana.

Eymael alisema tayari mezani kwake amepokea ofa mbili kutoka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Algeria za CS Constantine na CR Belouizdad na amepanga kuzitupilia mbali kama Yanga watachangamka kuharakisha mazungumzo naye ya kumpa nafasi iliyoachwa na Ernest Brandts. Alisema kama Yanga watakuwa na nia ya kweli katika kumpa kibarua hicho anawapa mpaka mwisho wa wiki hii na kama hawatamtafuta katika muda huo ataingia katika mazungumzo ya kujiunga na Costantine ambayo inamtafuta kila wakati kupitia mwenyekiti wa klabu hiyo.

CS Constantine inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 48, katika ligi inayoongozwa na ES Setif yenye pointi 59, wakati Belouizdad inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 41, ambapo klabu zote zinamuwinda Mbelgiji huyo.

“Nilivyofuatilia Yanga ni timu nzuri, unajua nilikuwa Kenya na AFC Leopards na hadi sasa wananihitaji, sijui uwezo wa wachezaji wa Yanga na kuhusu akili zao na mbinu lakini kama watakuwa na ubora hakuna shida katika kushindana na hao Al Ahly,” alisema Eymael.

“Kama Yanga wana nia ya kweli waambie wanitafute mpaka kufikia mwisho wa wiki hii, wakichelewa baada ya muda huo nitaingia katika mazungumzo na hawa Constantine ambao wapo katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Algeria. Huenda mambo yakamnyookea Eymael kwa kuwa mpango wa Yanga kumpa ajira Bobby Williamson, kocha wa Gor Mahia umegonga mwamba baada ya kocha huyo kugoma kuja Tanzania na kubaki Kenya ingawa viongozi wa Yanga wamedai kuwa hawakati tamaa hadi kieleweke. Akizungumza na Mwanaspoti Bobby raia wa Scotland, alisema amezungumza na mwenyekiti wa Gor Mahia mara baada ya kusikia Yanga wanamhitaji.

Chanzo: Mwanaspoti

SIMBA YAPATA VIKOSI VIWILI TISHIO

SIMBA ipo Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi, lakini kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola mapema wiki hii alionyesha sura ya vikosi viwili vya ushindi katika michuano hiyo. Katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam. 

Matola alipanga vikosi viwili na kuwachezesha kwa ushindani kwa muda usiopungua dakika 50. Kikosi cha kwanza ambacho kinaonekana ndicho kitakachotumika katika Kombe la Mapinduzi kiliundwa na Ivo Mapunda, Nassor Said ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Amissi Tambwe, Awadh Juma na Haruna Chanongo.Kikosi cha pili kiliwajumuisha, Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’, Salum Omar, Hassan Khatib, Gilbert Kaze, Abdulhalim Humud, Uhuru Seleman, Amri Kiemba, Betram Mombeki, Said Ndemla na Edward Christopher.

Wakati mazoezi hayo yakiendelea Berko alitoka baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Abdul Hashim, pia Redondo alipelekwa kikosi cha pili akibadilishana na Kiemba. Hii inaonyesha bado Redondo na Kiemba wanaweza kuingia kikosi cha kwanza kwa kutegemea zaidi majaliwa ya Henry Joseph ambaye hakushiriki mazoezi hayo. 

Henry yupo kikosi cha kwanza tangu awali.Kikosi cha pili kinaonekana kujaza vijana wengi ambao walipandishwa kutoka timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) ambao waliibana Yanga mwaka jana na kutoka sare ya mabao 3-3. Hata hivyo, ili kikosi hicho kiendelee kufanya kazi itategemea na hali za wachezaji kiafya na kimchezo kabla ya mchezo wowote ule pamoja na nidhamu. Matola hakuwa tayari kukubali au kukataa kuhusu kikosi hicho cha kwanza alichokipanga mazoezini. 


Chanzo: Mwanaspoti

ABIRIA 52 WALIOKWAMA KATIKA MELI HUKO ANTAKTIKA WAOKOLEWA

Waokoaji kutoka Australia wamefanikiwa kuwaokoa abiria 52 waliokuwa wamekwama katika meli ya Akademic Shokalskiy huko barani Antaktika toka tarehe 24 Desemba mwaka jana 2013 na helkopta inayomilikiwa na raia wa China aitwaye Xu Long. Meli hiyo ilikwama kutokana mlundikano wa barafu katika injini zake. Barafu hiyo ilisafirishwa na upepo mkali umbali wa netiko maili 1,500 kutoka katika mji wa Hobart jimbo la Australia. Kazi ya kuokoa abiria hao ilichukua dakika 45 kwa kila Wafanyakazi wa meli hiyo wanataraji kubaki katika meli hiyo kwa muda wa wiki moja mpaka pale barafu itakapoyeyuka. Aidha abiria hao waliokuwa wakisafiri kuelekea Tasmania hawatasafiri tena mpaka pale hali itakapokuwa shwari katikati ya mwezi huu.


Jinsi barafu ilivyokuwa imeganga
Jinsi barafu ilivyokuwa imeganga

IRAQ SECURITY FORCES FIGHT MILITANTS IN ANBAR PROVINCE

Special forces in Iraq are fighting Jihadist militants who have reportedly taken over swathes of two cities.The clashes with fighters from the Al Qaeda linked Islamic State of Iraq and the Levant (ISIS) are taking place in Fallujah and Ramadi.

Both cities are in the province of Anbar where Sunni militant activity has been on the rise.On Monday the security forces broke up a long-running Sunni anti-government protest camp in Ramadi. A senior police officer was quoted as saying ISIS fighters had seized at least 10 police stations and had freed a number of prisoners.

ISIS fighters have posted videos of themselves burning government vehicles, setting up checkpoints and issuing challenges to the authority of the Shia Prime Minister, Nouri Maliki. Sunni tribal fighters have also taken to the streets, with reports that some are fighting on the government side. As well as the breaking up of the protest camp, the arrest of a Sunni MP at the weekend also raised tensions. Sunni Arabs in Iraq claim they have been targeted and politically marginalised by Mr Maliki's government, a charge the prime minister denies.

Source: BBC

WAZIRI MGIMWA AFARIKI

RAIS Jakaya Kikwete amepokea kwa mshituko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Kalenga kupitia CCM.

Rais katika taarifa ya Ikulu jana, alisema Taifa limepoteza Waziri huyo katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa, ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Kalenga. Kifo cha Mgimwa kilitangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali. Katika tangazo lake, Balozi Sefue alisema Waziri Mgimwa aliaga dunia jana saa 5.20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi- Clinic, Pretoria, Afrika Kusini ambako alilazwa kwa muda kidogo.

Balozi Sefue alisema maandalizi ya kurudisha nyumbani mwili wa marehemu yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na taarifa zaidi zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea. Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na familia ya Mgimwa, Rais Kikwete alisema: “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshituko na huzuni yangu kubwa kutokana na taarifa za kifo cha Mgimwa.

“Binafsi nilimtembelea mara mbili hospitalini alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”Rais Kikwete aliongeza: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu. “Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wanafamilia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” alisema Rais Kikwete.

Rais pia aliwatumia rambirambi wananchi wa Kalenga akisema wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao. Kifo cha Mgimwa kinafanya wizara tano sasa kukosa mawaziri baada ya wengine wanne kuondoka, kutokana na sakata la ujangili kwa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, kukiuka haki za binadamu kwa baadhi ya raia kuuawa na wengine kupata ulemavu huku mifugo pia ikiuawa. Wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki alijiuzulu, mawaziri wengine watatu walitenguliwa vyeo vyao, ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.

Wasifu wake Mgimwa alizaliwa Kalenga Januari 20, 1950 na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Wasa kati ya mwaka 1961 na 1967 kabla ya kujiunga na Seminari ya Tosa kati ya mwaka 1966 na 1967. Baada ya hapo alijiunga na Seminari ya Tosamaganga kati ya mwaka 1968 na 1969 kisha Seminari ya Mafinga kati ya mwaka 1970 na 1971. Mwaka 1975 alijiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) hadi mwaka 1978 ambapo alipata Stashahada ya Juu katika masuala ya benki.Alirudi IFM mwaka 1983 na kusoma hadi mwaka 1984 na kutoka na Stashahada ya Uzamili katika fedha na mwaka 1989 alijiunga na Chuo cha Uongozi Mzumbe kusomea Shahada ya Uzamili katika fedha, ambayo aliipata mwaka 1991.

Kuhusu ajira, Mgimwa alifanya kazi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 2000, akishika nafasi za Mhasibu mwaka 1980 hadi 1981; mwaka 1981 hadi 1989 alikuwa mhadhiri katika Chuo cha NBC na mwaka 1996 hadi 1997 alikuwa Meneja katika benki hiyo. Kuanzia mwaka 1997 hadi 2000 alikuwa Mkurugenzi wa NBC kabla ya kuwa Mkuu wa Chuo cha Benki Mwanza kati ya mwaka 2000 na 2010, alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Kalenga, akichukua nafasi ya Stephen Galinoma.

Mei 7 mwaka juzi aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Fedha, akichukua nafasi ya Mustafa Mkulo.Ndani ya CCM Mgimwa kati ya mwaka 2008 na 2010 alikuwa Mlezi wa Kata ya Wasa, mwaka 1994 hadi 1995 alikuwa Kamanda Msaidizi wa Vijana wa CCM wakati mwaka 1991 hadi 1994 alipata kuwa Diwani wa Kata ya Gangilonga. Katika uhai wake aliandika machapisho mengi kuhusu masuala ya benki na fedha. Wakati huo huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtumia Rais Jakaya Kikwete salaam za rambirambi, kutokana na kifo hicho cha Waziri Mgimwa.

Aidha, kimetuma salaam kwa familia na uongozi wa CCM, kutokana na msiba huo wa kuondokewa na mmoja wa wanachama na mbunge.Taarifa iliyotolewa jana, ilisema chama hicho kimepokea kwa mshituko na majonzi makubwa taarifa za kifo hicho.“Kwa masikitiko makubwa, CHADEMA kinatuma salaam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na msaidizi wake wa karibu na mtumishi mwenzake serikalini,” ilisema taarifa ya chama.

Chanzo: Habari Leo

HERI YA MWAKA MPYA 2014

Venance Blog inawakutakia HERI YA MWAKA MPYA 2014 sherehekea kwa amani na utulivu kama ujuavyo ndo mwanzo wa mwaka hivyo unachotakiwa kufanya usilewe sana kama ni mtumiaji wa vileo eti kisa unafurahia kuumaliza mwaka 2013 na kukaribisha mwaka 2014 pia usitumie pesa hovyo kwani mwezi huu huwa mgumu sana. Mwisho nakutakia mafanikio mema katika mwaka huu 2014, uwe mwaka wa neema kwako na Mungu akutangulie katika kila jambo.. HERI YA MWAKA MPYA!!

KILA LA HERI KUUMALIZA MWAKA 2013 NA KUUANZA MWAKA 2014

Venance Blog inawatakieni kila la heri katika kuumaliza mwaka huu 2013 na kuuanza mwaka mpya 2014. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetulinda toka Januari 1 mpaka leo hii Desemba 31 muda na wakati kama huu, tumuombe pia atualie uzima tuweze kuufikia mwaka mpya 2014 tukiwa wazima wa afya ili pia tuendelee na ujenzi wa taifa letu Tanzania. Kwa hayo machache, Venance Blog inakutakia kila la heri na maandalizi mema ya kuupokea mwaka mpya, tusherehekee kwa amani na utulivu bila kuvuja sheria zilizowekwa... KARIBU 2014 KWA HERI 2013!!!

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yake.Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapyaAmeyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake. Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.Jaji Warioba amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi 38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano.Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja.Hata hivyo Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania BaraMalalamiko matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya Muungano,kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.Tanzania bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru , ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara.