MAZUNGUMZO YA AMANI KUHUSU SUDAN KUSINI YAANZA ADDIS ABABA
Mazungumzo ya kupatanisha pande mbili zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita, yameanza mjini Addis Ababa Ethiopia.Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya mambo ya nje nchini Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika Mashariki wananuia kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota kwa takriban wiki tatu.Hata hivyo mazungumzo ya ana kwa ana yangali kuanza kati ya pende zinazozozana yangali kuanza.Waakilishi kutoka pande zinazozozana wanakutana na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa vingozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa ana.Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais Salva Kiir na yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais Riek MacharWakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita.
Chanzo: BBC Swahili
Comments
Post a Comment