SIMBA YAPATA VIKOSI VIWILI TISHIO
SIMBA ipo Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi, lakini kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola mapema wiki hii alionyesha sura ya vikosi viwili vya ushindi katika michuano hiyo. Katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.
Matola alipanga vikosi viwili na kuwachezesha kwa ushindani kwa muda usiopungua dakika 50. Kikosi cha kwanza ambacho kinaonekana ndicho kitakachotumika katika Kombe la Mapinduzi kiliundwa na Ivo Mapunda, Nassor Said ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Amissi Tambwe, Awadh Juma na Haruna Chanongo.Kikosi cha pili kiliwajumuisha, Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’, Salum Omar, Hassan Khatib, Gilbert Kaze, Abdulhalim Humud, Uhuru Seleman, Amri Kiemba, Betram Mombeki, Said Ndemla na Edward Christopher.
Wakati mazoezi hayo yakiendelea Berko alitoka baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Abdul Hashim, pia Redondo alipelekwa kikosi cha pili akibadilishana na Kiemba. Hii inaonyesha bado Redondo na Kiemba wanaweza kuingia kikosi cha kwanza kwa kutegemea zaidi majaliwa ya Henry Joseph ambaye hakushiriki mazoezi hayo.
Henry yupo kikosi cha kwanza tangu awali.Kikosi cha pili kinaonekana kujaza vijana wengi ambao walipandishwa kutoka timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) ambao waliibana Yanga mwaka jana na kutoka sare ya mabao 3-3. Hata hivyo, ili kikosi hicho kiendelee kufanya kazi itategemea na hali za wachezaji kiafya na kimchezo kabla ya mchezo wowote ule pamoja na nidhamu. Matola hakuwa tayari kukubali au kukataa kuhusu kikosi hicho cha kwanza alichokipanga mazoezini.
Chanzo: Mwanaspoti
Comments
Post a Comment