Skip to main content

HALI BADO NI TETE NCHINI BURUNDI

HALI ya Burundi imezidi kuwa tete huku makundi mawili hasimu ya wanajeshi, yamekuwa yakipigana, kila moja likitaka kutawala jiji la Bujumbura.

Mapigano hayo ni kati ya wanajeshi wanaomtii Rais Pierre Nkurunziza, ambao wanapambana na wanajeshi wanaompinga, ambao wanamuunga mkono mwanajeshi aliyetangaza mapinduzi, Meja Jenerali Godefroid Niyombare.

Ofisa Mwandamizi wa Jeshi nchini humo, alisema wanajeshi wanaomtii Rais Nkurunziza wamefanikiwa kudhibiti na kurejesha maeneo muhimu ya jiji hilo chini ya utawala wa Serikali, ukiwamo uwanja wa ndege.

Hata hivyo, viongozi wa wanajeshi wanaompinga Rais huyo, wameendelea kudai kuwa wameipindua Serikali ya nchi hiyo.

Hali ya machafuko nchini humo, ilianza baada ya kiongozi huyo kutangaza kuwa ana nia ya kuwania tena kipindi cha tatu cha urais, jambo ambalo wapinzani nchini humo wamedai ni kinyume cha Katiba.

Kwa mujibu wa mashuhuda nchini humo, milio ya risasi na mabomu imekuwa ikisikika usiku kucha kuanzia juzi katika mapigano baina ya vikosi vinavyomtii Rais na vile vinavyotaka mapinduzi, lakini hadi sasa haijafahamika nani aliyefanikiwa kulidhibiti jiji hilo.

“Hatujaweza kulala kutokana na hofu tuliyonayo, milio ya milipuko na risasi imekuwa ikisikika kila sehemu, watu anaogopa kwa kweli,” mmoja wa mashuhuda aliwaambia waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari ndani ya kikosi kinachomtii Rais Nkurunziza, jeshi hilo limeweza kurejesha maeneo muhimu chini ya Serikali kama vile Ikulu, Redio na Televisheni ya Taifa na uwanja wa ndege.

Mitaa ya jiji hilo imejaa askari na polisi wanaomtii Rais na hadi majira ya jioni uwanja wa ndege, ulifunguliwa tayari kwa kutoa huduma za usafiri.

Hata hivyo, bado mapigano yanaendelea eneo ambapo televisheni na redio za taifa zipo, huku vikosi vinavyotaka mapinduzi vikijaribu kuingia ndani ya vituo hivyo vya habari.

Kila kikundi kinataka kudhibiti vituo hivyo vya utangazaji wa taifa, kwa kuwa ndio vyombo vya habari pekee vyenye uwezo wa kusikika hadi nje ya jiji hilo la Bujumbura.

Tayari Mkuu wa Majeshi na Rais Nkurunziza wametangaza na kudai kuwa jaribio la kupindua nchi hiyo, limeshindikana.

Hata hivyo, kauli hizo zimekuwa zikipingwa na viongozi wanaotaka mapinduzi nchini humo, na mmoja wao alisema kuwa wamefanikiwa kudhibiti takribani mji wote wa Bujumbura.

Msemaji wa kundi hilo la waasi, Venon Ndabaneze, alisema askari wanaotawanywa katika jiji hilo, wote wako upande unaotaka mapinduzi na si wanaomtii Rais Nkurunziza.

Juzi, Meja Jenerali Godefroid Niyombare, aliyekuwa Mkuu wa Usalama, alitangaza kumpindua Rais Nkurunziza akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, hali iliyozua shangwe kwenye mitaa mbalimbali jijini humo.

Niyombare alifukuzwa kazi na Rais Nkurunzinza Februari mwaka huu. Majengo ya kituo cha binafsi cha Televisheni Renaisance ya Burundi, iliyotumiwa na Meja Jenerali Niyombare, yameripotiwa kuharibiwa vibaya usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Innocent Muhozi, moja ya ofisi zake ilichomwa moto usiku huo na kusababisha kila kilichokuwepo ndani kuteketea.

Jenerali Niyombare, alitoa tangazo hilo, saa chache tu baada ya Rais huyo kupanda ndege kwenda Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliojadili suala hilo la Burundi.

Hata hivyo, iliripotiwa kuwa baada ya tangazo la kupinduliwa kwake, Nkurunziza, alirejea Burundi bila kuhudhuria mkutano huo, lakini alipofika Bujumbura alilazimika kurejea Dar es Salaam baada ya Uwanja wa Ndege wa Bujumbura kufungwa.

Habari zilizopatikana kutoka BBC baadaye jana jioni zilidai wanajeshi watano walikuwa wameuawa, silaha nzito zilikuwa zikitumika, mirindimo ya risasi ilisikika kila kona na waandamanaji walilazimika kujifungia ndani.

Ofisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa kutoka Ikulu ya Dar es Salaam, alipozungumza na AFP, alikiri kuwa Rais Nkurunziza bado yupo Tanzania, jijini Dar es Salaam, lakini haifahamiki ni sehemu gani alipo.

Nkurunzinza yuko wapi?

Suala sehemu alipo Rais Nkurunziza baada ya kufanyika ribio la kumpindua nchini kwake, limeendelea kuwa tete baada ya Tanzania kusema haijui alipo.

Hatua hiyo imetokana na tetesi kuwa Rais huyo yupo nchini baada ya kuhudhuria mazungumzo ya kutafuta amani kwa marais wa nchi za Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam na baadaye kutangazwa nchi hiyo kupinduliwa na kueleza kushindwa kurejea nchini mwake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo.

Awali , alipoulizwa alipo Rais huyo, alisema hawezi kujibu swali hilo lakini baadaye alisema hajui huku akiondoka na kucheka.

Membe alisema baada ya tamko la viongozi wa nchi za Afrika Mashariki, kulaani jaribio la kufanya mapinduzi katika nchi hiyo zaidi ya hayo Baraza la Mawaziri lililokutana kwa siku mbili Jumanne na Jumatano, litakutana tena Jumatatu wiki ijayo na kufanya tathmini ya hali halisi ya Burundi kwa siku tatu hizi mpaka Jumatatu.

“Kwa sasa sitaweza kuzungumza jambo jingine lolote kuanzia sasa mpaka Jumatatu jioni baada ya kikao cha baraza la mawaziri wenzangu, ambapo tutajua mambo ya kuzungumza.”

“Naomba kuwatahadharisha Watanzania kuwa hali ni tete Burundi lolote unalosema wewe na kudhani dogo linaweza kugharimu maisha ya mtu naomba mnielewe na mkae mkielewa haya mengine tutazungumza siku hiyo ya Jumatatu,” alisisitiza.

Alisema wananchi wa Burundi wako katika matatizo na vizuri kuvuta subira, badala ya kuendelea kuzungumza, kwani uhai wa mtu unaweza kuwa matatani.

Membe alipoulizwa alipo Rais wa Burundi, kwani inasemekana alirudi nchini Tanzania baada ya ndege yake kushindwa kutua nchini kwake , alisema yeye hajui.

Alisema hali ya Burundi ni tete na sababu hiyo, walikutana kutafuta ufumbuzi wa kudumu na wananchi waache kufanya ghasia na badala yake watulie na kuchagua viongozi wao kwa amani.

Alisema imeelezwa kuwa jaribio la jana la baadhi ya askari kutaka kuipindua Burundi, lililaaniwa na viongozi wote wa Afrika. Alisema Afrika haitaki nchi yoyote, kwa sababu zozote, kuhalalisha kuchukua madaraka kwa njia ya mtutu wa bunduki.

Wakimbizi wafa kwa kipindupinduKigoma

Wakati hali ya utawala nchini Burundi ikiwa tete , wakimbizi wa nchi hiyo waliopo mkoani Kigoma, wameanza kupatwa na majanga mengine baada ya kuripotiwa watu wanne kufa kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Leonald Subi alisema mjini Kigoma kwamba watu wawili walikufa wakiwa tayari wanaumwa ugonjwa huo na kufariki hapa nchini.

Alisema watu wawili wengine, walipatwa na ugonjwa huo wakisubiri msaada wa kibinadamu katika kijiji cha Kagunga wilaya Kigoma, mwambao wa Kaskazini wa Ziwa Tanganyika.

Subi alisema kuwa kwa sasa hali ya upatikaji wa huduma za kibinadamu, ikiwemo chakula, maji, mahala pa kujihifadhi na huduma ya choo ni mbaya sana kutoka na idadi kubwa ya wakimbizi hao kuwepo kijijini hapo kwa kipindi kifupi na hivyo kijiji hicho kuzidiwa katika kuwapatia huduma watu hao.



Chanzo: Habari Leo

Comments

Popular posts from this blog

DOWNLOAD AUDIO KUTOKA UPRISE MUSIC: JVP SQUAD-HUSTLE ZA KITAA

Ngoma imefanywa Uprise Music na producer Fragger. Ngoma inaitwa Hustle za Mtaa imefanywa na JVP Squad ndani kasimama Ng'itu the Hustler na Fizzo. Sikiliza na kudownload kisha toa maoni yako hapa.  BOFYA HAPA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD  

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi. Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!! Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj.  WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert  Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

LIST OF APPLICANTS SELECTED TO JOIN THE NATIONAL INSTITUTE OF TRANSPORT (NIT) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

To access the names of selected undergraduates click  HERE

SHAIRI: HEKO LIBERIA

Picha kwa hisani ya Freepik Shairi hili linakuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka huu nchini Liberia. Katika hali isiyo ya kawaida George Weah aliyekuwa akitetea nafasi yake ali kubali kusindwa na mpinzani wake Joseph Boakai katika Uchaguzi huo pasipo mvutano na migogoro kama ilivyozoeleka katika mataifa mengi ya bara hili . Kama mshairi niliwiwa kuandika ili kupongeza kitendo hiki cha uungwana kukubali kukabidhi madaraka pasipo mvutano ambao mara nyingi hupelekea umwagaji damu. Karibu katika shairi letu kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Shairi: Heko Liberia Mtunzi: Venance Gilbert Mpate Mwaka: 19 Novemba 2023 HEKO LIBERIA Heko Liberia naisifu yenu demokrasia, Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia, Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia, Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia, Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia, Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia, Mpinzani akashika dola imani ikaendelea, Heko Liberia naisifu yenu demokrasia. Mtawala aku...

DEADMEN SPEAKS: A POEM

Image generated with OpenArt AI tool It has been longtime since I published my poems on this platform, today I'm humbly inviting you to our section of poems. As you enjoy reciting this creativity, please don't forget to leave your comment after this post or writing via my contacts after this poem. Poem: Deadmen Speaks Poet: Venance Gilbert Composition: July 30, 2023 DEADMEN SPEAKS: A POEM BY VENANCE GILBERT I heard deadmen tells no tale but these ones do They are burdened with a lots Weak folks who talks nothing just talking in mind in the streets I say so because one of them is me I speak for deadmen. Six years with no stable duties to perform while responsibilities have taken-off This week this job next week none and I have to survive regardless But how without money How can I count money without job? I speak for deadmen. While I'm enjoying my jobless survival Executive wants to collect from my pocket I have to pay tariff to buy light tariff to withdraw my hard-earned sav...

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika. Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo: 1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia. 2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti. 3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takriba...

NExT-GPT: MFUMO WA LUGHA WA AKILI BANDIA UNAOKUPA MAJIBU KWA MAANDISHI, PICHA, SAUTI NA PICHA MJONGEO

Picha hii imetengenezwa kwa Akili Bandia na Decrypt. Katika uwanda mpana wa teknolojia unaotawaliwa na makampuni makubwa kama OpenAI na Google, NExT-GPT ambao ni mfumo huria wa lugha pana ya Akili Bandia (AI) [Large Language M odel (LLM)] unaweza kuwa na kile kinachohitajika ili kushindana na miamba hii miwili katika teknolojia. ChatGPT imeusisimua ulimwengu kwa uwezo wake wa kuelewa maswali katika lugha asilia na kutoa majibu kama ya binadamu. Lakini wakati Akili Bandia inaendelea kusonga mbele kwa kasi ya umeme, watu wametaka kuwepo na maendeleo zaidi. Zama za maandishi pekee zimekwisha sasa mifumo ya lugha ya Akili Bandia imeanza kuwa mingi kuleta ushindani. NExT-GPT imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha taifa cha Singapore (NUS) na Chuo Kikuu cha Tsinghua. Inaweza kuchakata na kutoa majibu kwa kuchanganya maandishi, picha, sauti na picha mjongeo (video). Hii inaruhusu majibizano ya asili zaidi kuliko miundo ya maandishi pekee kama ilivyo kwenye ChatGPT. T...

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa  FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa  Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

Chuo cha Mipango ama Institute of Rural Development Planning kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za shahada (Bachelor Degree) chuoni hapo mwa mwaka wa masomo 2016/207. BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO IMPORTANT NOTICES TO SELECTED STUDENTS The selected candidates must report at the Institute’s main campus Miyuji area on Monday 17 th October, 2016 ready for orientation program. Joining instructions can be downloaded from the website www.irdp.ac.tz and can also be collected from the main campus admission office. Tuition fees for Bachelor Degree courses 850,000/= Registration fee is 50,000/=, Students organization fee 20,000/= sports and games is 10,000/= and NACTE Quality Assurance Fee 20,000/=. Students are required to pay atleast half of the tuition fee and 100,000/= for registration, students organization, sports and games and NACTE Quality Assurance Fee. The payment should be made through CRDB Bank account no. 01J1082678600 before 1...

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI...