MFAHAMU KARL MARX KWA UFUPI: DUNIA INAMKUMBUKA LEO

Karl Mark alikuwa ni mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Ujerumani aliyeandika vitabu vya The Communist Manifesto na Das Capital vitabu ambavyo vilikuwa vikipingana na mfumo wa kibepari na kuunda mfumo wa Ukomunisti ama Ujamaa kama alivyoutafsiri hayati Mwalimu JK Nyerere.

Karl Marx alizaliwa Mei 5, 1818. Alianza kuchunguza nadharia za kijamii alipokuwa Chuo Kikuu na wenzie waliounda kikundi chao kilichoitwa Young Hegelians. Hiki kilikuwa ni kikundi kilichokuwa kinaamini katika falsafa za mwalimu wao aliyeitwa Hegel. Marx alikuwa mwandishi wa habari na machapisho yake kuhusu Ukomunisti vilipelekea yeye kufukuzwa Ujerumani na Ufaransa. Mwaka 1848 alichapisha kitabu chake cha The Communist Manifesto akiwa na Friedrich Engels ambacho kilipelekea kufukuzwa Ujerumani na kukimbilia London, Uingereza, huko pia aliandika kitabu cha Das Kapital ambako ndiko alikoishi mpaka alipoiaga dunia.

Karl Marx alikuwa ni miongoni mwa watoto 9 wa Heinrich Marx na Henrietta Marx huko Trier Prussia ya zamani (kwa sasa Ujerumani) Baba yake alikuwa mwanasheria aliyefanikiwa sana na alikuwa mwanaharakati aliyependa mabadiliko nchini Prussia. Japokuwa wazazi wake walikuwa na asili ya Kiyahudi, baba yake Marx alihamia katika Ukristu mwaka 1816 alipokuwa na umri wa miaka 3.

Marx alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida. Alisomea nyumbani hadi alipokuwa na umri wa miaka 12 na kisha alipelekwa Jesuit High School alikosoma kwa muda wa miaka 5 kuanzia 1830 hadi 1835.

Mwaka 1835 Marx alijiunga na Chuo Kikuu cha Bonn. Chuo hiki kilikuwa na Itikadi za kuipinga serikali. Marx alijiunga na maisha ya uanafunzi katika chuo hiki. Katika semista mbili chuoni hapo, alifungwa kwa ulevi na kuvuruga amani chuoni hapo, kuwa na madeni lakini pia kushiriki katika falsafa zilizokinzana na chuo. Mwisho wa mwaka baba yake Marx alimsisitiza kuwa serious na masomo katika Chuo Kikuu cha Berlin.

Katika Chuo Kikuu Berlin alisomea fani ya sheria na falsafa ambako alikutana na falsafa za mwalimu wake George Hegel ambaye alikuwa profesa katika chuo hicho mpaka alipofariki mwaka 1895. Baadaye Marx alijiunga na kikundi cha Young Hegelians ambacho pia kulikuwa na Bruno Bauer na Ludwig Feuerbach ambao walikosoa kuanzishwa kwa siku za kisiasa na kidini nchini humo. Kuna mengi yalijiri Marx alipokuwa Berlin.
Tokeo la picha la marx and bruno bauer
Bruno Bauer
Marx hakutulia wala kuishia hapo. Mwaka 1841 alitunukiwa Shahada yake ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Jena lakini harakati zake za kisiasa zilipelekea yeye kutokuaminiwa na kuwa mwalimu katika chuo chochote nchini Ujerumani. Alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari na mwaka 1842 alikuwa Mhariri wa Rheinische Zeitung ambalo lilikuwa ni gazeti la wanaharakati wa usawa huko Cologne, Ujerumani. Mwaka mmoja baadaye serikali ililifuta gazeti hilo kuanzia April 1, 1843. Marx aliacha kazi hapo Machi 18. Miezi mitatu baadaye alimuoa Jenny von Westephalen  na Oktoba walihamia Paris, Ufaransa.
Tokeo la picha la karl marx and his family
Marx akiwa na mkewe Jenny von Westephalen
Mji wa Paris ulikuwa ni kitovu cha harakati za kisiasa barani Ulaya mwaka 1843. Huko Marx akiwa na Arnold Ruge, walianzisha gazeti la uchambuzi wa kisiasa lilioitwa Deutsch-Franzosische Jahrbucher (German-French Annals) jambo moja tu ndilo lilikuwa likichapishwa katika gazeti hili kabla Marx na Ruge hawajatofautiana kiitikadi hadi kupelekea gazeti hilo kupotea kwenye ramani lakini Agosti 1844, gazeti hilo liliwaleta pamoja Marx na Friedrich Engels kama mwandishi mshiriki ambaye alikuwa msaidizi wake na rafiki yake hadi kifo. Pamoja, wawili hao walianza kuandika makala za kukosoa mawazo ya Bruno Bauer ambaye alikuwa ni mshiriki katika kikundi cha Young Hegelians. Mwaka 1845 Marx na Engels walichapisha makala yao iliyojulikana kama The Holy Family.


Baadaye katika mwaka huo, Marx alihamia Ubeligiji baada ya kufukuzwa nchini Ufaransa ambako aliandika katika gazeti la Vorwarts! ambalo lilikuwa na itikadi ambazo baadaye zingepelekea kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kikomunisti. Alipokuwa Ubeligiji, Marx alipokelewa na Moses Hess, na baadaye aliachana kabisa na siasa za Young Hegelians. Alipokuwa nchini humo aliandika The German Ideology ambako ndiko alipoandika nadharia yake inayojulikana kama Historical Materialism. Marx hakupata mtu wa kuruhusu kuchapisha makala yake. The German Ideology na Theses on Feuerbach hayakuchapisha makala hiyo hadi alipofariki. Nadharia hii inawataka watu kushiriki kwa vitendo kupinga uonevu.


Tokeo la picha la Karl marx and engels
Karl Marx & Friedrich Engels
Mwanzoni mwa mwaka 1846, Mark alianzisha Communist Correspondence Committee katika juhudi zake za kuunganisha ukomunisti barani Ulaya. Waingereza walivutiwa na sera zake na kuitisha mkutano na kuunda shirikisho lao Communist League na mwaka 1847 katika mkutano wao mkuu uliofanyika London, shirikisho hilo liliwaomba Marx na Engels kuandika Manifest der Kommunistischen Partei (Manifesto of the Communist Party)

The Communist Manifesto ni miongoni mwa kazi maarufu za Marx ambayo ilichapishwa mwaka 1848 na baadaye mwaka 1849 Marx alifukuzwa nchini Ubeligiji. Alikwenda Ufaransa ambako alianzisha vuguvugu la Mapinduzi nchini humo ambako pia alifukuzwa. Prussia ilikataa kumpokea Marx na hivyo alihamia London japokuwa Uingerza ilikataa kumpa uraia nchini humo hadi kifo chake.

Marx alipokuwa London alisaidia kuundwa kwa shirikisho la wanataaluma wa Ujerumani German Workers' Educational Society lakini pia Shirikisho la Kikomunisti The Communist League. Aliendelea kufanya kazi kama mwandishi japokuwa safari hii alizuiwa na baadhi ya itikadi zake. Alifanya kazi katika The New York Daily Tribune kwa miaka 10 kuanzia 1852-1862 lakini hakulipwa , aliishi kwa kusaidiwa na rafiki yake Engels.

Marx aliutazama mfumo wa kibepari zaidi na mwaka 1867 alichapisha toleo la kwanza la kitabu chake Das Kapital. Baadaye alitumia muda wake kupitia chapisho hilo na akawa akilifanyia masahihisho na kuongeza baadhi ya vitu. Matoleo mawili yaliyofuata baadaye ambayo hata hakuyakamilisha yaliunganishwa na kuchapishwa na Engels.

Marx alifariki kwa ugonjwa wa mapafu unaojulikana kitaalamu kama pleurisy alipokuwa London Machi 14, 1883. Katika kaburi lake kuna maandishi ya kitabu chake The Communist Manifesto yenye maana wafanyakazi wote waungane.



MAKALA HII IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO INAWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUDA WOWOTE PANAPOHITAJIKA.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017