HEZBOLLAH YATAJA SABABU YA KUUAWA KIONGOZI WAO
Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia la Hezbollah nchini Lebanon limetaja sababu ya kifo cha kiongozi wake wa ngazi ya juu wa kijeshi, Mustafa Badreddine kuwa kimetokana na makombora ya mizinga liliofanyika karibu na uwanja wa ndege wa Damascus nchini Syria.
Hezbollah lilitangaza kifo cha Badreddine hapo jana na alifanyiwa mazishi ya kijeshi siku hiyo hiyo katika eneo la ngome la kundi hilo huko kusini mwa Beirut. Taarifa ya kundi hilo imesema mashambulizi hayo yamefanywa na kundi linaloitwa Takfiri.
Takfiri ni neno linalotumiwa na kundi hilo la Kisunni kwa kuonesha msimamo mkali, kundi lenye kujihami na silaha, lililo na itikadi kali.
Badreddine alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Hezbollah walioshutumiwa mwaka 2005 kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri.
Chanzo: Deutsche Welle (DW)
Comments
Post a Comment