IN THE NEXT - A POEM BY VENANCE GILBERT


Poem: IN THE NEXT 
Composition: December 19, 2014 
First published on the blog: December 29, 2014


The system has turned to uplift us,
From nothing to something mammoth,
Look at them brother, look them twice more,
They have our consent in authority,
Having our consent to share our sufferings,
For self into their bellies,
Look brother, feel pitty for ourselves,
The cultural similarity is credited,
Now brother tell them involved,
Go into details to them,
In the next to put their money where their mouth are,
Let them experience a miss in the next,
To re-drink the milk of human kindness.



All rights reserved.
Venance Gilbert © 2014.



IF YOU HAVE ANYTHING TO COMMENT DON'T HESITATE TO CONTACT ME THROUGH:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert
Mobile: 0753400208
Email: venancegilbert@gmail.com.



VENANCE BLOG WISHES YOU A HAPPY NEW YEAR 2015!!

KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA


Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.

Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.

Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.


KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 TANGU JANGA LA TSUNAMI MWAKA 2004


Mataifa yaliyoathirika na janga la Tsunami yameandaa ibada za kuwakumbuka watu 220,000 waliouawa wakati mawimbi makali yalipoyapiga maeneo ya pwani ya Bahari Hindi mwongo mmoja uliopita.

Mnamo Desemba 26 mwaka wa 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.3 katika upande wa magharibi wa Indonesia lilianzisha msururu wa mawimbi makali ambayo yaliupiga mwambao wa mataifa 14 ikiwa ni pamoja na Indonesia, Thailand, Sri Lanka na Somalia.

Miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha yao ni maelfu ya watalii waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Krismasi katika eneo hilo, na kulipeleka janga la maafa ya asilia ambayo hayakuwa yametarajiwa hadi majumbani kote ulimwenguni.

Maelfu ya watu wameimba wimbo wa taifa wa Indonesia kama mwanzo wa kumbukumbu ya janga hilo, kwenye ibada iliyoandaliwa Banda Aceh - mji mkuu wa mkoa ulio karibu na kitovu cha tetemeko la arshi ambalo lilisababisha mawimbi hayo makali.

Mapema leo misikiti pia iliandaa maombi kite katika mkoa huo, wakati watu wakiyatembelea makaburi ya pamoja – ya karibu Waindonesia 170,000 waliopoteza maisha yao.

Kusini mwa Thailand, ambako nusu ya watu 5,300 waliokufa walikuwa watalii wa kigeni, umati wa wageni walio likizoni walikusanyika katika uwanja wa makumbusho katika kijiji kidogo cha wavuvi cha Ban Nam Khem, katika kumbukumbu ya janga hilo kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni.

Mataifa yaliyoathirika na maafa hayo yalikabiliwa na juhudi za kutafuta msaada, wakati miili ya watu ikiendelea kutapakaa kila mahali au kujazana kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti.
Ulimwengu ulimwaga fedha nyingi na watalaamu wa huduma za misaada na ujenzi, huku zaidi ya kiasi cha dola bilioni 13.5 zikikusanywa katika miezi iliyofuata baada ya janga hilo.

Karibu msaada wa kiasi cha dola bilioni 7 ulitumika katika ujenzi mpya wa zaidi ya nyumba 140,000 kote Aceh, barabara za umbali wa maelfu ya kilomita, na shule mpya pamoja na hospitali. Maelfu ya watoto pia ni miongoni mwa waliouawa.
Lakini janga hilo pia lilimaliza mgogoro uliodumu miongo mingi wa kutaka kujitenga eneo la Aceh, huku mkataba wa amani baina ya waasi na serikali ya Jakarta ukisainiwa chini ya mwaka mmoja baadaye.

Nchini Sri Lanka, ambako watu 31,000 waliuawa, maandalizi yanafanyika ili kuandaa kumbukumbu katika eneo la barabara ya reli ambako mawimbi yalilipiga treni ya abiria, na kuwauwan watu 1,500.

Mnamo mwaka wa 2011, mfumo wa kuonya kuhusu janga la Tsunami uliundwa, wakati nchi mbalimbali za eneo hilo zikiwezeka kiasi kikubwa cha fedha katika mifumo ya kujikinga na majanga.


Chanzo: DW 


BOTI YAZAMA NA WATU 36 JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO



Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36.
Maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika.


Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye mji wa Isangi ambapo mashua hiyo ilikuwa ikielekea nyumba kadha za serikali zinaripotiwa kuchomwa.



Chanzo: BBC Swahili







WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert
Simu: +255712586027/753400208 
Email: venancegilbert@gmail.com

VENANCE BLOG INAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS 2014

VENANCE BLOG inapenda kuwatakia heri ya Christmas kwa mwaka huu 2014 tusherekee kwa amani na upendo huku tukimtanguliza Mungu katika kila jambo kwani yeye ndo muweza wa yote. Heri ya Krismas na pia Heri ya Mwaka mpya 2015!!







WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert
Simu: +255712586027/+255753400208 
Email: venancegilbert@gmail.com

VIDEO MPYA: BRACKETS-ALIVE FT DIAMOND & TIWA ICHEKI HAPA NA KUDOWNLOAD


Alive -“Hii ni hadithi ya kweli ya Vast Bracket, safari yake hadi alivyopona kansa mwaka 2013. Huu ni wimbo wa shukrani kwa kumfanya mshindi aliyeishinda kansa.”



Hayo ni maneno yanayoonekana mwanzoni mwa video ya wimbo mpya ya kundi la Bracket kutoka Nigeria iliyotoka wiki hii, ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz na Tiwa Savage.


Kipindi Vast anaumwa kansa

Memba wa kundi hilo aitwaye Vast, mwaka 2013 alikuwa akipigania uhai wake baada ya kuugua kansa ya damu ambayo baadae alifanikiwa kupona, ndio sababu ya kundi hilo kuamua kurekodi wimbo huu ‘Alive’ kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kumuwezesha msanii huyo kupona.


Vast ni yule ambaye anaimba vesre ya kwanza na kwenye video anaonekana yupo hospitali.


Video hii hapa


Vast aliwahi kuelezea jinsi alivyougua hadi kupona katika mahojiano mbalimbali aliyofanyiwa 2013:

“It all started when we went on an American tour and I started feeling feverish. I found myself taking my bath with hot water even on a very hot day. That was when I started noticing something was wrong. I noticed that whenever I drank alcohol, the fever would come in an aggressive way. I eventually went to a hospital in London. The doctor told me not to worry that everything would be fine. He said to start the treatment, they would have to do something that would allow them take something from my spine. It was a very painful procedure.”

“There was a time that I felt I would die. My only fear was that I was not close to God. I was afraid that if I died, I would not make it to heaven. We musicians have a particular lifestyle. You may plan to be upright, but when you go into entertainment business, it would change you. I was regretting that I was not close to God. I did not want to go to hell. I felt so happy that I survived,”.

“After the treatment, I did two other tests and the doctors confirmed that I was okay. After three months, I am meant to go for a PET scan. I could remember that before the treatment, we had a meeting and agreed that we had to bring £50,000. After the seventh chemotherapy session, the whole money finished. They had to send more £8,000 into the account I was using. The last time I went to withdraw money, what was left there was £120. So I used about £58,000,”

What kind of cancer did you have?

“I had Lymphoma. It is a blood cancer. When I asked the doctor what could the cancer of the blood, he said, nobody knows the cause for now. According to him, it’s like a situation where a dark complexion couple making a baby and the baby turns out to be an albino and if you are asked to explain why, you cannot tell.

I must say that when I was hospitalised, my partner was doing a good job. He would call the producer and they would make a beat and send it to me. He even made the chorus. I picked one of the songs when I came back and hit the studio. We did one of the tracks, it was fantastic. We did another song and it was good as well, all within two days.”

What have you learnt from your experience?

“I learnt that life is very precious. No matter what you do and wherever you are, don’t look down on anybody because you don’t know who will help you tomorrow. Another thing is that you don’t have to be scared of death. You have to face the challenge. Live a normal life. If you are scared of death, you will die. At a point, when I got very scared, the sickness came in full force, but when I started picking courage, it subsided and I recovered.”


KUREJESHWA KWA ADHABU YA KIFO AFGHANSTAN KWAWAPA WASIWASI AMNESTY

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametangaza kurejeshwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, kwa watakaokutwa na hatia ya ugaidi ingawa Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linapinga sheria hiyo.

Pakistan imetoa uamuzi wa kurejesha sheria ya kunyonga watakaokutwa na hatia ya ugaidi. Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif, siku moja baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Taliban na kusababisha vifo vya watu 150, wakiwemo wanafunzi 135. Mashambulizi hayo yalitokea tarehe (16.12.2014), katika shule inayomilikiwa na jeshi ilioko mjini Peshawar.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kurejeshwa kwa adhabu ya kifo, hakutaisaidia Pakistan kupambana na Ugaidi.

Azimio hilo lilipitishwa bila ya pingamizi tarehe (17.12.2014), katika mkutano uliojumuisha vyama vyote vya siasa vya nchi hiyo. Pakistan imesema kuwa kurejesha kwa sheria ya kunyonga walio na hatia ya ugaidi ni hatua muhimu, kwani katu haiwezi kuonyesha huruma yoyote kwa wale wanaohusika na matendo ya ugaidi na kuua watu wasio na hatia.

“Nimetangaza kurejeshwa kwa sheria ya adhabu ya kifo leo, na taifa zima liko pamoja na sisi,” alisema Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif.

Tangu tangazo hilo kutolewa na serikali ya Pakistan, watu wanne tayari wameshanyongwa katika jimbo la Punjab. Watu hao walikutwa na hatia za kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Rais wa zamani Jenerali Pervez Musharraf, mwaka 2003 na Jenerali wa Makao Makuu ya Jeshi la Pakistan mwaka 2009.

Hata hivyo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuanza tena kunyonga watu baada ya sheria hiyo kusimamishwa mwaka 2008 sio suluhisho ya kuzuia matatizo ya ugaidi.

“Hii ni hatua ya kijinga. Serikali inataka kuficha kushindwa kukabiliana na suala la msingi lililooneshwa na mashambulizi ya Peshawar, yaani ukosefu wa ulinzi madhubuti kwa raia wa maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Pakistan," alisema Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International wa Asia-Pacific David Griffiths katika taarifa yake.
Aliongeza kwa kusema, adhabu ya kifo inakiuka haki za kibinaadamu. Hali hii inatupa wasiwasi mkubwa , kwani itasababisha ukiukwaji wa sheria mbalimbali za kimataifa wakiendelea kutekeleza mpango wao.

Lakini serikali kwa upande wake imejitetea kwa kusema kuwa nchi hio ipo katika wakati mgumu wa kupambana na ugaidi, hivyo hakuna njia nyengine bali kurejesha sheria ya kunyonga, huku makundi ya kidini pamoja na ya kisiasa yakikubaliana na uwamuzi huwo wa serikali.

"kunyongwa kwa magaidi wawili tarehe 19 Disemba ilikuwa ni ushindi kwa sheria ya nchi," Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf aliliambia shirika la habari la IPS, na kuongeza " Hatimaye serikali imewatendea haki magaidi."

Pakistan ina wafungwa 8000 ambao wamekuwa wakisubiri adhabu ya kifo tangu mwaka 2008. 17 kati yao walifungwa kwa mashtaka ya ugaidi, na adhabu yao ya kifo kwa kunyongwa itatekelezwa katika siku saba zijazo.

"Kutokana na hali ilivyo nchini humo, maisha ya watu wengi yapo hatarini. Serikali ya Pakistan inalazimika kufuta tena sheria ya adhabu ya kifo," alionya Griffiths wa shirika la Amnesty International.


MMAREKANI MWEUSI AWAUA ASKARI WAWILI WA MAREKANI NA BASTOLA NA KISHA KUJIUA MWENYEWE

Mtu mmoja nchini Marekani amewaua askari wawili waliokuwa kaka patrol wakiwa wamevalia nguo za kazi. Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwalenda askari hao na kuwafatulia risasi na baadae kujiua mwenyewe. 

Hii ni bastola iliyokutwa eneo la tukio.


Inasemekana kuwa mwanaume huyo aliwahi kumjeruhi mpenzi wake wa zamani kwa kumfyatulia risasi iliyomsababishia majeraha.


Áidha inasemekana pia kuwa kabla hajatenda tukio hilo aliandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe ambao si mzuri kwa polisi. Pia aliweka picha ya bastola hyo katika akaunti yake ya Instagram na kuañdika kuwa hiyo ndio itakuwa post yake ya mwisho.

Aidha mtu huyo ambaye ni Mmarekani mweusi ametajwa kwa jina la Ismaail Brinsley miaka 28 na maofisa hao kuwa ni Liu Wenjin na Raphael Ramos.

Mauàji hayo yametokea kufuatia kuwepo na mauaji ya watu weusi Marekani wanaouawa na maaskari weupe wa Marekani na kutochukuliwa hatua zozote na nchi hiyo..

Rais Obama wa Marekàni aliye katika jimbo la Hawaii kwa mapumziko ya sikukuu amelaani tukio hilo.



ChanzO: BBC NEWS




WASILIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert
Simu: 0712586027/0743400208
Email: venancegilbert@gmail.com




ICHEKI KWA MARA YA KWANZA VIDEO YA ALI KIBA - "MWANA"


Alikiba - Mwana (Official Music Video)
Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’ imeachiwa leo hii Ijumaa ya 19 Decemba 2014. 
Ali Kiba Alithibitisha kuwa video imekamilika na kusema Video imetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town.

Vituo vitakavyo rusha hii video 
Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks.

Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv.

Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTVUganda.

Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto.

Tanzania itachezwa kwenye kituo cha CloudsTV.

Hii ndio Video Halisi ya Mwana itazame.

DOWNLOAD WIMBO MPYA WA BRACKETS FT DIAMOND PLATNUMZ NA TIWA SEVAGE HAPA

Wakati Davido wa Nigeria akimponda sana Diamond Platnumz, kuwa hana fadhila, wasanii kutoka Nigeria Brackets wamakuja na ujio mpya wa Wimbo wao uitwao Alive ukiwa kama gospel fulani, wakiwa wanamshukuru Mwenyezi Mungu. Mwanadada Tiwa Savage pia amehusika humu ndani. Diamond a.k.a. Chibu Dangote kama kawaida kawakilisha kwa lugha yetu ya KISWAHILI.

 
ILI KUDOWNLOAD WIMBO HUU BONYEZA HAPA




WASILIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

UMOJA WA MATAIFA WAOMBA MSAADA KWA AJILI YA SYRIA

Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha Dola bilioni 8.4 kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura wa kibinaadamu kwa takribani watu milioni 18 wa Syria na kuzunguka ukanda huo unaokumbwa na mzozo.
Ombi hilo limetolewa jana na maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Berlin, Ujerumani kwenye mkutano wa wafadhili na wamesema msaada huo unahitajika haraka nchini Syria, na katika nchi na jamii zinazopambana kuwahifadhi wakimbizi wa Syria.
Kwa mara ya kwanza ombi hilo la Umoja wa Mataifa, linahusisha msaada wa chakula cha kuwapa nguvu na kurudisha afya, malazi, msaada mwingine wa kibinaadamu pamoja na msaada wa maendeleo.
Maafisa wa umoja huo wamesema Dola bilioni 2.9 zinahitajika ili kuwasaidia watu milioni 12.2 walioko ndani ya Syria kwa mwaka 2015, na Dola bilioni 5.5 zinahitajika kwa ajili ya Wasyria walioomba hifadhi ya ukimbizi kwenye nchi jirani na zaidi ya watu milioni moja katika jamii zinazowahudumia.
Kiasi hicho cha fedha kilichoombwa mjini Berlin, ni kikubwa zaidi ya kile kilichoombwa mjini Geneva, mwanzoni mwa mwezi huu, msaada ambao haukujumuisha fedha kwa ajili ya nchi jirani. Hata hivyo, umoja huo umeshapata nusu tu ya kiwango kilichoombwa mwaka huu 2014.
Mahitaji ya kibinaadamu yanaongezeka
Kamishna Mkuu wa Shirika linalowahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR, Antonio Gutteres ameonya kuwa wakimbizi na watu wasio na makaazi ndani ya Syria hawana akiba na nchi zinazowahifadhi ziko katika wakati mgumu, hivyo utaratibu mpya wa misaada unahitajika.
''Mahitaji ya kibinaadamu duniani yanaongezeka, na yanaongezeka kwa kasi. Na ni wazi kwamba fedha zilizopo kwa ajili ya kutimiza mahitaji hayo, haziongezeki kulingana na kukua kwa kasi ya mahitaji,'' alisema Gutteres.
Naye Mkuu wa shughuli za kibinadamu na misaada ya dharura ya Umoja wa Mataifa, Valerie Amos amesema Syria imetoka katika taifa la watu wenye kipato cha kati na kutumbukia kwenye nchi inayopambana na umaskini mkubwa. Amesema watu walioathirika na mzozo wanahitaji chakula, malazi, maji, dawa na ulinzi, lakini pia wanahitaji msaada wa kujenga upya maisha yao, kupata elimu na huduma za afya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amesema mzozo wa kibinaadamu nchini Syria na kwenye nchi jirani unatoa kitisho kwa utulivu wa ukanda wote. Amesema huo ni mwito wa mshikamano kwa mataifa yote na nchi yake iko tayari kutoa sehemu yake.
Mwezi Oktoba, Ujerumani ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria, ambapo wajumbe waliahidi kuongeza msaada wa kifedha wa muda mrefu katika nchi kama vile Lebanon na Jordan, ambazo zinakabiliana na mamilioni ya wakimbizi wa Syria wanaoingia kwa kasi kwenye nchi hizo.
Kiasi watu 200,000 wamekufa na karibu nusu ya idadi ya wakaazi wa Syria hawana makaazi kutokana na mgogoro ulioanza kwa maandamano ya kuipinga serikali ya Rais Bashar al-Assad mwaka 2011 na kugeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.




Chanzo: Deustche Welle (DW)












WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

BAISKELI YA DHAHABU YATENGENEZWA BEI YAKE INASHINDA FERARI


Kampuni ya Goldgenie iliyopo nchini Uingereza inayojihusisha na kutengezeza vitu vya kifahari, imezindua baiskeli yake mpya ya dhahabu yenye thamani ya dola 390,000 ambayo ni bei ghali hata kuliko gari jipya la Ferrari.



Gia za baikeli hiyo zimetengezwa kwa dhahabu pamoja na mikono na vyuma vyake vyote ambapo kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.



Mkurugenzi wakampuni iliyotengeza baiskeli hiyo anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo. Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkurugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.



“Baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.” Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,” aliongeza kusema mkurugenzi huyo.



Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.













WASLIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG
Source: Bongo5 via BBC

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM


Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi.



Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!!




Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj. 






WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert 



Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

HUENDA TANZANIA IKAKOSA MSAADA KUTOKA MAREKANI KWA SABABU YA RUSHWA

Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo.
Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.
Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.
Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Novemba mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.
Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
Juhudi za BBC kumtafuta Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress,aweze kuzungumzia juu ya ripoti hiyo ziligonga mwamba kutokana na sababu za kiprotokali.


Chanzo: BBC

VIDEO MPYA: NIKKI II FT BEN POL-SITAKI KAZI ITAZAME HAPA

Nikki wa pili ameachia video ya wimbo wake Sitaki kazi alomshirikisha Ben Pol. Kitu kimoja Nikki alitakiwa afanye kuchoma vyeti kama alivyoimba hata asingechoma vyeti halisi ilitakiwa afanye hivyo. Video hii hapa chini:




LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK

NIFUATE TWITTER

NIFUATE INSTAGRAM



Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

MTANDAO WA INSTAGRAM WAFIKISHA WATUMIAJI MILION 300


Mtandao wa Instagram leo umefikisha jumla ya watumiaji milioni 300 dunia nzima huku kukiwa na picha na video zaidi ya milioni 70 ambazo zinawekwa kila siku katika mtandao huo. Uongozi wa mtandao huo umeahidi kutatua tatizo la akaunti za watu maarufu ambazo hu-hakiwa na watu na kuahidi kuzifuta akaunti hizo hivyo kutoa taarifa kwamba watu wasishangae kuona idadi ya watu wanaowafuata kupungua.



WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert  





Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

VIDEO MPYA: AY FT MS TRINITY & LA'MYIA ICHEKI HAPA

Mwanamuziki Ambwene Yesaya a.k.a. A.Y. kutoka hapa hapa Bongo land Tz ameachia video ya wimbo wake uitwao Touch me alowashirikisha Sean Kingston na Ms Trinity. Pata nafasi ya kuangalia video hiyo hapa chini ama fuatisha KIUNGO HIKI kuingalia katika akaunti yake ya Youtube. Video hii hapa chini;





EXCLUSIVE: DAVIDO ATOA VIDEO YA WIMBO WAKE 'OWO NI KOKO' ITAZAME HAPA

 
Mwanamuziki kutoka Nigeria, Davido ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Owo ni Koko. 





WASILIANA NAMI KWA:
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert










KWA HISANNI YA DJ CHOKA MUSIC

RAIA NCHINI MISRI WAANDAMANA KUPINGA HUKUMU YA MUBARAK


Polisi nchini Misri wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi ya mauaji dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.

Zaidi ya watu 2000 walikusanyika katika viunga vya Tahrir mahala ambapo ndipo zilipozaliwa harakati za mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 2011.

Awali Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo kwa sasa anatumikia pia kifungo cha miaka mitatu kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa sasa Hosni Mubarack anashikiliwa katika hospitali ya jeshi ambako pia anapatiwa matibabu.

Waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani Habib al-Adly na wenzake sita walihukumiwa kifungo cha maisha 2012, inakadiriwa takriban watu 800 waliuawa wakati wa harakati za kumuondoa kiongozi huyo Februari 11.2011.


Chanzo: BBC

JENIFER LOPEZ NDANI YA BIKINI

Mwanamuziki Jennifer Lopez Ameshare Picha Kwenye Instagram Profile yake Ambayo Inamuonyesha Akiwa Ndani ya Bikini akiwa na Umri wa Miaka 45 Sasa...

CHINA YATOA DOLA BILIONI 85 KUPAMBANA NA EBOLA KATIKA NCHI TATU ZA AFRIKA




SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imetangaza kuwa, kwa mara ya nne katika kipindi kifupi inapeleka msaada wa dawa, vifaa na mahitaji mengine ya tiba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 85 kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa nchi tatu za Afrika Magharibi, ambazo zinapambana na ugonjwa huo, ambao mpaka sasa umeua zaidi ya watu 4,000.

Aidha, China imetangaza kuwa itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba katika nchi ya Liberia, kama sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo. Msaada huo mwingine wa China umetangazwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, XI Jinping katika mazungumzo yake rasmi na Rais Jakaya Kikwete.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye The Great Hall of the People mjini Beijing, ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya Rais Kikwete, Rais Jinping alisema: “Hali katika Afrika sasa ni ya utulivu lakini yapo matishio ya mara kwa mara mengine ya ndani ya Afrika na mengine ya nje na mojawapo ya matishio hayo ni ugonjwa wa ebola.”

Aliongeza Rais Jinping: “Mpaka sasa, China imetuma misaada ya dawa na rasilimali nyingine mara tatu kwa nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zinakabiliana na ugonjwa wa ebola. Napenda kutangaza China, imeamua kupeleka msaada mwingine wenye thamani ya RMB 500 ikiwa ni fedha taslim, wataalamu wa afya, wataalamu wengine na rasilimali nyingine.”

Alisema “China pia itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba ili kiweze kusaidia nchi zote tatu ambazo zinakumbwa na ugonjwa huo wa ebola Liberia, Guinea na Sierra Leone. Tunaungana na wananchi wa nchi hizo tatu katika kukubaliana na tishio hili kubwa ambalo kwa hakika linahitaji ushirikiano wa dunia nzima.”




Chanzo: Habari Leo

ANCELOTTI: SIPENDEZWI NA UHUSIANO WA MORINHOU KWA RONALDO


The Real Madrid boss insists that he does not know, or care, whether the former Blancos manager and the Portugal international have an off-field friendship or not

Real Madrid coach Carlo Ancelotti says he is not interested in Jose Mourinho's relationship with Cristiano Ronaldo.

The Portuguese manager, who previously bossed Madrid but is now in charge at Premier League giants Chelsea, revealed on Thursday that he and Ronaldo do not keep in touch following the 51-year-old's departure from the Spanish capital in the summer of 2013.

But Ancelotti says the matter is not one that concerns him.

"Mourinho is a great coach who can coach anywhere," the 55-year-old said.

"I don't know what his relationship with Cristiano is like, nor am I interested. It is a personal relationship and has nothing to do with Real Madrid.

"I don't know if Mourinho wants to [ever] come back [to Madrid]," he added.

The Italian trainer also discussed criticism of his team following their poor start to La Liga this term - having taken only three points from their first three games.

"I don't understand the lack of confidence in this team, four months ago we won the European Cup and we may win it again," he continued. "Madrid will fight for all competitions until the end.

"We are not thinking about the distance we are behind Barcelona or Atletico Madrid, we need to improve our tactical and physical levels.

"Due to the World Cup we had an odd pre-season, some players arrived back late. That's a problem for all teams.

"We have to improve and show consistency. We've lacked that but I think we'll improve."




Source: Goal.com

VAN GAAL: MADRID HAWATOMUUZA RONALDO

The Dutchman admits he would welcome the arrival of the Portugal international but believes the European champions would not be prepared to sell the player

Louis van Gaal admits Manchester United would explore the possibility of signing Cristiano Ronaldo but insists it is unlikely that Real Madrid will sell the forward.

Reports have suggested that the Portugal international, who signed a five-year contract extension with Madrid last September, will push for a move back to Old Trafford at the end of the season.

But while the United boss maintains his side would be strengthened by the return of Ronaldo, he believes the European champions are not prepared to allow the 29-year-old to leave.

“It’s always a discussion in the papers. I don’t think the media shall buy Ronaldo,” said Van Gaal.

“When it is possible, it is what I have always said with Falcao, players like Ronaldo give a lot extra to selection, to the team, but I don't think Real Madrid shall sell him.”

Earlier this month, Ronaldo admitted that he would be keen to return to Old Trafford, but insisted he was happy at Madrid.

"I love Manchester. Everyone knows that - I have said it many times. Manchester is in my heart," said the Portugal international.

"I left many good friends there, the supporters are amazing and I wish I can come back one day."




Source: Goal.com

QUOTES OF THE DAY SEPTEMBER 19, 2014

1. You cannot create experience. You must undergo it.
Albert Camus

2. We are not human beings having a spiritual experience. We are spiritual beings having a human experience.
Pierre Teilhard de Chardin

3. Human beings, who are almost unique in having the ability to learn from the experience of others, are also remarkable for their apparent disinclination to do so.
Douglas Adams

4. Experience is the teacher of all things.
Julius Caesar

5. People grow through experience if they meet life honestly and courageously. This is how character is built.
Eleanor Roosevelt

6. Man learns through experience, and the spiritual path is full of different kinds of experiences. He will encounter many difficulties and obstacles, and they are the very experiences he needs to encourage and complete the cleansing process.
Sai Baba

7. A mind that is stretched by a new experience can never go back to its old dimensions.
Oliver Wendell Holmes, Jr.

8. If you want to know the taste of a pear, you must change the pear by eating it yourself. If you want to know the theory and methods of revolution, you must take part in revolution. All genuine knowledge originates in direct experience.
Mao Zedong

9. Our wisdom comes from our experience, and our experience comes from our foolishness.
Sacha Guitry

10. There are many truths of which the full meaning cannot be realized until personal experience has brought it home.
John Stuart Mill





Source: BrainyQuotes

SCOTLAND HAITAJITENGA NA UINGEREZA, KURA YA HAPANA YAAMUA


Scotland imefanya uamuzi wa mwisho kuwa itaendelea kubaki sehemu ya Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland kujitenga kuwa taifa huru.

Maeneo 31 kati ya 32 wamepiga kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura 1,914,187 dhidi ya  kura 1,539,920.

Ushindi huo ni asilimia 55 dhidi ya asilimia 45 waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.

Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.




Chanzo: BBC

QUOTES OF THE DAY SEPTEMBER 16


1. Happiness is like a kiss. You must share it to enjoy it. ~Bernard Meltzer

2. There is only one way to happiness and that is to cease worrying about things which are beyond the power of our will. ~Epictetus

3. Our greatest happiness does not depend on the condition of life in which chance has placed us, but is always the result of a good conscience, good health, occupation, and freedom in all just pursuits. ~Thomas Jefferson

4. Achievement of your happiness is the only moral purpose of your life, and that happiness, not pain or mindless self-indulgence, is the proof of your moral integrity, since it is the proof and the result of your loyalty to the achievement of your values. ~Ayn Rand

5. Try to make at least one person happy every day. If you cannot do a kind deed, speak a kind word. If you cannot speak a kind word, think a kind thought. Count up, if you can, the treasure of happiness that you would dispense in a week, in a year, in a lifetime! ~Lawrence G. Lovasik

6. Happiness cannot be traveled to, owned, earned, worn or consumed. Happiness is the spiritual experience of living every minute with love, grace, and gratitude. ~Denis Waitley

7. Be happy with what you have and are, be generous with both, and you won't have to hunt for happiness. ~William E. Gladstone

8. Happiness is when what you think, what you say, and what you do are in harmony. ~Mahatma Gandhi

9. Happiness is not something ready made. It comes from your own actions. ~Dalai Lama

10. Be happy for this moment. This moment is your life. ~Omar Khayyam






Source: BrainyQuotes

KAMA BADO HUJAIONA VIDEO YA PROFESA J-KIPI SIJASIKIA, ICHEKI HAPA

Imetengenezaewa na Adam Juma Next Level, kuna wasanii kibao humo ndani wa filam pamoja na bongo fleva kama vile Dude, P Funk Majani na wengineo huku Platnumz akifanya vizuri zaidi. Video hii hapa:


VIDEO: KANYE WEST NA HEADLINE YA KUTAKA WALIOHUDHURIA SHOW YAKE WASIMAME (HADI WALEMAVU) KIM KADARSHIAN AMTETEA







Rapper Kanye West ametawala vichwa vingi vya habari weekend iliyopita baada ya tukio alilolifanya kwenye moja ya show za tour yake ya Australia. Katika show hiyo Kanye alisimamisha show na kuwataka watu wote wasimame ndio aendelee na show.


“I can’t do this song, I can’t do the rest of the show until everybody stands up, Unless you got a handicap pass and you get special parking,” Kanye alisikika akiwaambia mashabiki waliofurika kwenye uwanja wa Qantas Credit Union huko Sydney.

Baada ya mashabiki wengine kusimama kama walivyoombwa na Kanye, watu wawili waliendelea kukaa na ndipo Kanye alipowaona na kuendelea kuwamtaka nao wasimame, mpaka alipokuja kugundua kuwa ni walemavu ndipo akasema ‘”If he’s in a wheelchair, then it’s fine,” na kisha kuendelea kutumbuiza wimbo mwingine.

Kim Kardashian West ameibuka na kumtetea mume wake kwa kuvilaumu vyombo vya habari kuwa vimedanganya. Kim ameongeza kuwa Kanye hakumwambia mtu yeyote aliye kwenye ‘wheel chair’ asimame bali alichokisema Kanye ni kila mtu asimame na kucheza isipokuwa wale walioko kwneye ‘wheel chair”.

Kupitia Instagram Kim K ameandika:



“What an amazing Australian tour! Its frustrating that something so awesome could be clouded by lies in the media. Kanye never asked anyone in a wheel chair to stand up & the audience videos show that. He asked for everyone to stand up & dance UNLESS they were in a wheel chair. #JustWantedEveryoneToHaveAFunNight #TheMediaTwistsThings”



BONYEZA/CLICK HAPA KUANGALIA VIDEO YA SHOW HIYO

QUOTES OF THE DAY SEPTEMBER 15, 2014

1. By failing to prepare, you are preparing to fail. ~Benjamin Franklin

2. Optimism is the faith that leads to achievement. Nothing can be done without hope and confidence. ~Helen Keller

3. I don't believe you have to be better than everybody else. I believe you have to be better than you ever thought you could be. ~Ken Venturi

⁴. A creative man is motivated by the desire to achieve, not by the desire to beat others.

5. The will to win, the desire to succeed, the urge to reach your full potential... these are the keys that will unlock the door to personal excellence. ~Confucius

6. One of the most beautiful qualities of true friendship is to understand and to be understood. ~Lucius Annaeus Seneca

7. Problems are not stop signs, they are guidelines. ~Robert H. Schuller

8. In order to succeed, we must first believe that we can. ~Nikos Kazantzakis

9. You have to learn the rules of the game. And then you have to play better than anyone else. ~Albert Einstein

10. If you can dream it, you can do it. ~Walt Disney



Source: Brainy Quotes

3 IN ONE: PROFESA JAY KUZINDUA VIDEO MBILI NA WEBSITE YAKE KWA SIKU MOJA

Msanii Profesa Jay hapo kesho anataraji kuachia video za nyimbo zake mbili KIPI SIJASIKIA na TATU CHAFU pamoja na uzinduzi wa tovuti yake ambayo kiungo chake ni www.profesajay.com. Ni katika ukumbi wa TEN LOUNGE zamani LETASI LOUNGE BUSINESS PARK VICTORIA jijini DSM ni kw kiingilio cha Tsh. 10,000/= kuanzia saa mbili usiku hapo kesho Jumamosi...



Vyanzo: facebook, instagram na twitter accounts za Professor Jay



VENANCE BLOG © September 2014

YANGA KUMKOSA COUTINHO KATIKA MCHEZO WA NGAO YA HISANI


Coutinho aliumia katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Polisi Dar es Salaam mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Loyola, unaotumiwa na Yanga kwa mazoezi



TIMU ya Yanga huenda ikakosa huduma ya kiungo wake mshambuliaji wa kimataifa kutoka Brazili Andrew Coutinho,katika mchezo wa Ngao ya Jamii Jumapili wakati timu hiyo itakapokuwa inapambana na Azam FC,kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Goal inafahamu.

Coutinho ameumia kifundo cha mguu na taarifa za madaktari wa Yanga zinasema huenda Mbrazili huyo aliyejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili huenda akakaa nje kwa wiki mbili hadi tatu.

Daktari wa Yanga Juma Sufiani,ameiambia Goal,bado wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumtibu mchezaji huyo ili aweze kuichezea timu yake kwenye mchezo wa Jumapili kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi chao.

Kuelekea mchezo huo Azam tayari wametangaza nahodha wake John Bocco,kutocheza mechi hiyo ya Jumapili kutokana na kuumia misuli kwenye mchezo wa robo fainali ya michuno ya Kombe la Kagame iliyomalizika mwezi uliopita Kigali Rwanda.

Coutinho aliumia katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Polisi Dar es Salaam mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Loyola, unaotumiwa na Yanga kwa mazoezi.



Chanzo: Goal.com

BOB JUNIOR AZUNGUMZIA COLLABO ZAKE NA BEN POL NA CHAMELEONE


Bob Junior azungumzia collabo zake na Ben Pol na Jose ChameleoneBy Bongo5 Editor on September 12, 2014 (1 min ago)

Rais wa Masharobaro nchini, Bob Junior amefanya collabo mbili tofauti na Ben Pol pamoja na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.



Akiongea na Bongo5, Bob Junior ambaye hivi karibuni aliachia kazi yake mpya iitwayo Bolingo, alidai kuwa lengo la kushirikisha wasanii hao ni kuja na muziki mpya ambao watu hawajazoea kutoka kwake.

“Kuna project ya mimi na Chameleone ambayo inayoka mwezi wa 10 so bado sijajua kama itatangulia ya Ben Pol na mimi au ntatoa ngoma yangu mimi peke yangu au ya mimi na Chameleone,” alisema.

Hivi karibuni muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki alisema kuwa amebadilisha jina la studio yake kutoka Sharobaro Records na kuwa Sharobaro Music na kwamba muziki atakaokuwa anatayarisha utakuwa na ladha tofauti.

VIFAA VYA KUWATAMBUA WENYE UGONJWA WA EBOLA VYAINGIZWA NCHINI

Serikali imeanza kuingiza nchini vifaa vya kuwabaini watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa kali ya ebola ambavyo vitawekwa kwenye viwanja vya ndege pamoja na baadhi ya maeneo ya mipakani. Jana Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe alikabidhi mashine nne za kuwapima abiria wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege bila kuwagusa. Vifaa hivyo vinabaini mtu kuwa na dalili za ebola kutokana na joto lake na abiria wanapimwa kwa kumulikwa machoni na kwenye masikio. Kwa kuanzia mashine hizo ambazo ni mfano wa kamera zitapelekwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam. Maeneo hayo kwa mujibu wa naibu waziri huyo ndiyo yanapokea wagonjwa wengi kutoka nje ya nchi. Dk Kebwe pia aliagiza shehena ya mashine zingine zitakazoingizwa nchini kuanzia leo zipelekwe kwenye viwanja vingine vya Mtwara, Kigoma na maeneo ya mipakani kuhakikisha kuwa kila abiria anayetoka nje ya nchi anapimwa dalili za ugonjwa huo hatari. Pia aliagiza wanadiplomasia na viongozi wa kitaifa wanaotoka nje ya nchi ambako wanakwenda kuhudhuria mikutano mbalimbali pia wapimwe kwani ugonjwa hauchagui cheo wala fedha na hadhi aliyo nayo mtu. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alisema jana kuwa wamenunua mashine hizo nne kutoka Afrika Kusini, lakini zimetengenezwa nchini Marekani kwa kiasi cha Sh milioni 16. Alisema katika kipindi hiki ambacho kuna mlipuko wa ugonjwa wa ebola huko Afrika Magharibi, upatikanaji wa vifaa hivyo ni adimu na haiwezekani kupata mashine zote kwa msambazaji mmoja, hivyo akasema leo ziwawasili mashine nyingine mbili kutoka Ubelgiji. Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga alisema mashine hizo kitaalamu zinajulikana kama thermo scanners ni mashine za mkononi na kila abiria atakayeshuka uwanja wa ndege atapimwa kwenye macho au masikio bila kugusana.