KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 TANGU JANGA LA TSUNAMI MWAKA 2004


Mataifa yaliyoathirika na janga la Tsunami yameandaa ibada za kuwakumbuka watu 220,000 waliouawa wakati mawimbi makali yalipoyapiga maeneo ya pwani ya Bahari Hindi mwongo mmoja uliopita.

Mnamo Desemba 26 mwaka wa 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.3 katika upande wa magharibi wa Indonesia lilianzisha msururu wa mawimbi makali ambayo yaliupiga mwambao wa mataifa 14 ikiwa ni pamoja na Indonesia, Thailand, Sri Lanka na Somalia.

Miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha yao ni maelfu ya watalii waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Krismasi katika eneo hilo, na kulipeleka janga la maafa ya asilia ambayo hayakuwa yametarajiwa hadi majumbani kote ulimwenguni.

Maelfu ya watu wameimba wimbo wa taifa wa Indonesia kama mwanzo wa kumbukumbu ya janga hilo, kwenye ibada iliyoandaliwa Banda Aceh - mji mkuu wa mkoa ulio karibu na kitovu cha tetemeko la arshi ambalo lilisababisha mawimbi hayo makali.

Mapema leo misikiti pia iliandaa maombi kite katika mkoa huo, wakati watu wakiyatembelea makaburi ya pamoja – ya karibu Waindonesia 170,000 waliopoteza maisha yao.

Kusini mwa Thailand, ambako nusu ya watu 5,300 waliokufa walikuwa watalii wa kigeni, umati wa wageni walio likizoni walikusanyika katika uwanja wa makumbusho katika kijiji kidogo cha wavuvi cha Ban Nam Khem, katika kumbukumbu ya janga hilo kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni.

Mataifa yaliyoathirika na maafa hayo yalikabiliwa na juhudi za kutafuta msaada, wakati miili ya watu ikiendelea kutapakaa kila mahali au kujazana kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti.
Ulimwengu ulimwaga fedha nyingi na watalaamu wa huduma za misaada na ujenzi, huku zaidi ya kiasi cha dola bilioni 13.5 zikikusanywa katika miezi iliyofuata baada ya janga hilo.

Karibu msaada wa kiasi cha dola bilioni 7 ulitumika katika ujenzi mpya wa zaidi ya nyumba 140,000 kote Aceh, barabara za umbali wa maelfu ya kilomita, na shule mpya pamoja na hospitali. Maelfu ya watoto pia ni miongoni mwa waliouawa.
Lakini janga hilo pia lilimaliza mgogoro uliodumu miongo mingi wa kutaka kujitenga eneo la Aceh, huku mkataba wa amani baina ya waasi na serikali ya Jakarta ukisainiwa chini ya mwaka mmoja baadaye.

Nchini Sri Lanka, ambako watu 31,000 waliuawa, maandalizi yanafanyika ili kuandaa kumbukumbu katika eneo la barabara ya reli ambako mawimbi yalilipiga treni ya abiria, na kuwauwan watu 1,500.

Mnamo mwaka wa 2011, mfumo wa kuonya kuhusu janga la Tsunami uliundwa, wakati nchi mbalimbali za eneo hilo zikiwezeka kiasi kikubwa cha fedha katika mifumo ya kujikinga na majanga.


Chanzo: DW 


Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU