YANGA KUMKOSA COUTINHO KATIKA MCHEZO WA NGAO YA HISANI


Coutinho aliumia katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Polisi Dar es Salaam mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Loyola, unaotumiwa na Yanga kwa mazoezi



TIMU ya Yanga huenda ikakosa huduma ya kiungo wake mshambuliaji wa kimataifa kutoka Brazili Andrew Coutinho,katika mchezo wa Ngao ya Jamii Jumapili wakati timu hiyo itakapokuwa inapambana na Azam FC,kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Goal inafahamu.

Coutinho ameumia kifundo cha mguu na taarifa za madaktari wa Yanga zinasema huenda Mbrazili huyo aliyejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili huenda akakaa nje kwa wiki mbili hadi tatu.

Daktari wa Yanga Juma Sufiani,ameiambia Goal,bado wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumtibu mchezaji huyo ili aweze kuichezea timu yake kwenye mchezo wa Jumapili kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi chao.

Kuelekea mchezo huo Azam tayari wametangaza nahodha wake John Bocco,kutocheza mechi hiyo ya Jumapili kutokana na kuumia misuli kwenye mchezo wa robo fainali ya michuno ya Kombe la Kagame iliyomalizika mwezi uliopita Kigali Rwanda.

Coutinho aliumia katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Polisi Dar es Salaam mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Loyola, unaotumiwa na Yanga kwa mazoezi.



Chanzo: Goal.com

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017