SCOTLAND HAITAJITENGA NA UINGEREZA, KURA YA HAPANA YAAMUA
Scotland imefanya uamuzi wa mwisho kuwa itaendelea kubaki sehemu ya Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland kujitenga kuwa taifa huru.
Maeneo 31 kati ya 32 wamepiga kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura 1,914,187 dhidi ya kura 1,539,920.
Ushindi huo ni asilimia 55 dhidi ya asilimia 45 waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.
Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment