RAIA NCHINI MISRI WAANDAMANA KUPINGA HUKUMU YA MUBARAK


Polisi nchini Misri wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi ya mauaji dhidi ya Rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.

Zaidi ya watu 2000 walikusanyika katika viunga vya Tahrir mahala ambapo ndipo zilipozaliwa harakati za mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 2011.

Awali Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo kwa sasa anatumikia pia kifungo cha miaka mitatu kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa sasa Hosni Mubarack anashikiliwa katika hospitali ya jeshi ambako pia anapatiwa matibabu.

Waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani Habib al-Adly na wenzake sita walihukumiwa kifungo cha maisha 2012, inakadiriwa takriban watu 800 waliuawa wakati wa harakati za kumuondoa kiongozi huyo Februari 11.2011.


Chanzo: BBC

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU