CHINA YATOA DOLA BILIONI 85 KUPAMBANA NA EBOLA KATIKA NCHI TATU ZA AFRIKA




SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imetangaza kuwa, kwa mara ya nne katika kipindi kifupi inapeleka msaada wa dawa, vifaa na mahitaji mengine ya tiba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 85 kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa nchi tatu za Afrika Magharibi, ambazo zinapambana na ugonjwa huo, ambao mpaka sasa umeua zaidi ya watu 4,000.

Aidha, China imetangaza kuwa itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba katika nchi ya Liberia, kama sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo. Msaada huo mwingine wa China umetangazwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, XI Jinping katika mazungumzo yake rasmi na Rais Jakaya Kikwete.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye The Great Hall of the People mjini Beijing, ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya Rais Kikwete, Rais Jinping alisema: “Hali katika Afrika sasa ni ya utulivu lakini yapo matishio ya mara kwa mara mengine ya ndani ya Afrika na mengine ya nje na mojawapo ya matishio hayo ni ugonjwa wa ebola.”

Aliongeza Rais Jinping: “Mpaka sasa, China imetuma misaada ya dawa na rasilimali nyingine mara tatu kwa nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zinakabiliana na ugonjwa wa ebola. Napenda kutangaza China, imeamua kupeleka msaada mwingine wenye thamani ya RMB 500 ikiwa ni fedha taslim, wataalamu wa afya, wataalamu wengine na rasilimali nyingine.”

Alisema “China pia itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba ili kiweze kusaidia nchi zote tatu ambazo zinakumbwa na ugonjwa huo wa ebola Liberia, Guinea na Sierra Leone. Tunaungana na wananchi wa nchi hizo tatu katika kukubaliana na tishio hili kubwa ambalo kwa hakika linahitaji ushirikiano wa dunia nzima.”




Chanzo: Habari Leo

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU