BAISKELI YA DHAHABU YATENGENEZWA BEI YAKE INASHINDA FERARI


Kampuni ya Goldgenie iliyopo nchini Uingereza inayojihusisha na kutengezeza vitu vya kifahari, imezindua baiskeli yake mpya ya dhahabu yenye thamani ya dola 390,000 ambayo ni bei ghali hata kuliko gari jipya la Ferrari.



Gia za baikeli hiyo zimetengezwa kwa dhahabu pamoja na mikono na vyuma vyake vyote ambapo kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.



Mkurugenzi wakampuni iliyotengeza baiskeli hiyo anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo. Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkurugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.



“Baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.” Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,” aliongeza kusema mkurugenzi huyo.



Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.













WASLIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG
Source: Bongo5 via BBC

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

EMINEM FT RIHANNA-THE MONSTER SONG LYRICS

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017