VIDEO: KANYE WEST NA HEADLINE YA KUTAKA WALIOHUDHURIA SHOW YAKE WASIMAME (HADI WALEMAVU) KIM KADARSHIAN AMTETEA







Rapper Kanye West ametawala vichwa vingi vya habari weekend iliyopita baada ya tukio alilolifanya kwenye moja ya show za tour yake ya Australia. Katika show hiyo Kanye alisimamisha show na kuwataka watu wote wasimame ndio aendelee na show.


“I can’t do this song, I can’t do the rest of the show until everybody stands up, Unless you got a handicap pass and you get special parking,” Kanye alisikika akiwaambia mashabiki waliofurika kwenye uwanja wa Qantas Credit Union huko Sydney.

Baada ya mashabiki wengine kusimama kama walivyoombwa na Kanye, watu wawili waliendelea kukaa na ndipo Kanye alipowaona na kuendelea kuwamtaka nao wasimame, mpaka alipokuja kugundua kuwa ni walemavu ndipo akasema ‘”If he’s in a wheelchair, then it’s fine,” na kisha kuendelea kutumbuiza wimbo mwingine.

Kim Kardashian West ameibuka na kumtetea mume wake kwa kuvilaumu vyombo vya habari kuwa vimedanganya. Kim ameongeza kuwa Kanye hakumwambia mtu yeyote aliye kwenye ‘wheel chair’ asimame bali alichokisema Kanye ni kila mtu asimame na kucheza isipokuwa wale walioko kwneye ‘wheel chair”.

Kupitia Instagram Kim K ameandika:



“What an amazing Australian tour! Its frustrating that something so awesome could be clouded by lies in the media. Kanye never asked anyone in a wheel chair to stand up & the audience videos show that. He asked for everyone to stand up & dance UNLESS they were in a wheel chair. #JustWantedEveryoneToHaveAFunNight #TheMediaTwistsThings”



BONYEZA/CLICK HAPA KUANGALIA VIDEO YA SHOW HIYO

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017