Skip to main content

KUREJESHWA KWA ADHABU YA KIFO AFGHANSTAN KWAWAPA WASIWASI AMNESTY

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametangaza kurejeshwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, kwa watakaokutwa na hatia ya ugaidi ingawa Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linapinga sheria hiyo.

Pakistan imetoa uamuzi wa kurejesha sheria ya kunyonga watakaokutwa na hatia ya ugaidi. Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif, siku moja baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Taliban na kusababisha vifo vya watu 150, wakiwemo wanafunzi 135. Mashambulizi hayo yalitokea tarehe (16.12.2014), katika shule inayomilikiwa na jeshi ilioko mjini Peshawar.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kurejeshwa kwa adhabu ya kifo, hakutaisaidia Pakistan kupambana na Ugaidi.

Azimio hilo lilipitishwa bila ya pingamizi tarehe (17.12.2014), katika mkutano uliojumuisha vyama vyote vya siasa vya nchi hiyo. Pakistan imesema kuwa kurejesha kwa sheria ya kunyonga walio na hatia ya ugaidi ni hatua muhimu, kwani katu haiwezi kuonyesha huruma yoyote kwa wale wanaohusika na matendo ya ugaidi na kuua watu wasio na hatia.

“Nimetangaza kurejeshwa kwa sheria ya adhabu ya kifo leo, na taifa zima liko pamoja na sisi,” alisema Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif.

Tangu tangazo hilo kutolewa na serikali ya Pakistan, watu wanne tayari wameshanyongwa katika jimbo la Punjab. Watu hao walikutwa na hatia za kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Rais wa zamani Jenerali Pervez Musharraf, mwaka 2003 na Jenerali wa Makao Makuu ya Jeshi la Pakistan mwaka 2009.

Hata hivyo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuanza tena kunyonga watu baada ya sheria hiyo kusimamishwa mwaka 2008 sio suluhisho ya kuzuia matatizo ya ugaidi.

“Hii ni hatua ya kijinga. Serikali inataka kuficha kushindwa kukabiliana na suala la msingi lililooneshwa na mashambulizi ya Peshawar, yaani ukosefu wa ulinzi madhubuti kwa raia wa maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Pakistan," alisema Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International wa Asia-Pacific David Griffiths katika taarifa yake.
Aliongeza kwa kusema, adhabu ya kifo inakiuka haki za kibinaadamu. Hali hii inatupa wasiwasi mkubwa , kwani itasababisha ukiukwaji wa sheria mbalimbali za kimataifa wakiendelea kutekeleza mpango wao.

Lakini serikali kwa upande wake imejitetea kwa kusema kuwa nchi hio ipo katika wakati mgumu wa kupambana na ugaidi, hivyo hakuna njia nyengine bali kurejesha sheria ya kunyonga, huku makundi ya kidini pamoja na ya kisiasa yakikubaliana na uwamuzi huwo wa serikali.

"kunyongwa kwa magaidi wawili tarehe 19 Disemba ilikuwa ni ushindi kwa sheria ya nchi," Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf aliliambia shirika la habari la IPS, na kuongeza " Hatimaye serikali imewatendea haki magaidi."

Pakistan ina wafungwa 8000 ambao wamekuwa wakisubiri adhabu ya kifo tangu mwaka 2008. 17 kati yao walifungwa kwa mashtaka ya ugaidi, na adhabu yao ya kifo kwa kunyongwa itatekelezwa katika siku saba zijazo.

"Kutokana na hali ilivyo nchini humo, maisha ya watu wengi yapo hatarini. Serikali ya Pakistan inalazimika kufuta tena sheria ya adhabu ya kifo," alionya Griffiths wa shirika la Amnesty International.


Comments

Popular posts from this blog

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika. Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo: 1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia. 2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti. 3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takriba...

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi. Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!! Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj.  WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert  Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

Chuo cha Mipango ama Institute of Rural Development Planning kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za shahada (Bachelor Degree) chuoni hapo mwa mwaka wa masomo 2016/207. BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO IMPORTANT NOTICES TO SELECTED STUDENTS The selected candidates must report at the Institute’s main campus Miyuji area on Monday 17 th October, 2016 ready for orientation program. Joining instructions can be downloaded from the website www.irdp.ac.tz and can also be collected from the main campus admission office. Tuition fees for Bachelor Degree courses 850,000/= Registration fee is 50,000/=, Students organization fee 20,000/= sports and games is 10,000/= and NACTE Quality Assurance Fee 20,000/=. Students are required to pay atleast half of the tuition fee and 100,000/= for registration, students organization, sports and games and NACTE Quality Assurance Fee. The payment should be made through CRDB Bank account no. 01J1082678600 before 1...

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

Jana nilikuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea Kusini, leo tuangalie upande wa pili kwa akina dada ambao ni warembo zaidi. #10. Han Ye Seul   Han Ye Seul alizaliwa chini Marekani japokuwa ana asili ya Korea. Anaigiza series na filamu za kawaida. Alionekana katika Nonstop 4 na pia ameigiza katika muvi kama vile Couple or Truble, Birth of a Beauty, Miss Gold Digger na Penny Pincher. Baada ya kupata umaarufu nchini Korea aliamua kufuta uraia wake wa Marekani na kuamua kuwa raia wa Korea Kusini. #9. Song Hye Kyo Song Hye Kyo alipata umaarufu katika tasnia ya muvi nchini Korea katika muvi kama vile Autumn in My Heart, All In, Full House, The World They Live In na nyinginezo. Ni mwenye furaha na amekuwa akiigiza muvi zake vizuri sana. #8. Lee Da Hae Lee Da Hae ni muigizaji maarufu nchini Korea Kusini. Ameigiza katika My Girl, Green Rose, The Slave Hunter, Miss Ripley na Hotel King. Ameigiza pia katika muvi za Kichina kama vile Actually Lob...

UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU GOOGLE BARD

Nembo (logo) ya Google Bard Kufuatia mafanikio ya robotisogozi ya OpenAI ambayo ni ChatGPT, Google ilitoa robotisogozi yake ya akili bandia, Bard. Kwa vile inapatikana sehemu kubwa haya ndiyo unayohitaji kufahamu kuihusu Bard lakini kabla sijaendelea nikufahamishe vifupisho vya maneno yatayotumika katika makala hii: AI - Artificial Intelligence ambayo ni Akili Bandia. LaMDA - Language Model for Dialogue Applications ambao ni Mfumo wa Lugha kwa Mazungumzo na Matumizi. LLM - Large Language Model ambao ni Mfumo Mkubwa wa Lugha. PALM (PaLM) - Pathways Language Model ambavyo ni vigezo bilioni 540 va kigezo cha lugha kubwa modeli iliyotengenezwa na Google AI Bard ni huduma ya Google ya majaribio ya mazungumzo ya akili bandia. Inakusudiwa kufanya kazi sawa na ChatGPT huku tofauti kubwa ni kwamba huduma ya Google itatoa habari zake kutoka katika wavuti. Picha ya skrini: Venance Gilbert  Kama vile gumzo nyingi za akili bandia, Bard anaweza kuandika msimbo (code), kuj...

LIST OF UNDERGRADUATES SELECTED TO JOIN TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

The following applicants have been selected to join various programmes offered by Tanzania Institute of Accountancy for the Academic year 2018/2019. Selected candidates should report to their respective campuses on 29 th  OCTOBER 2018. Joining instructions and admission letters can be downloaded through our website www.tia.ac.tz The Institute has limited accommodation facilities for students. Those who wish to stay at the Institute’s Hostels should apply in advance to their respective campuses before commencement of an academic year. Applicants with status  “PENDING FOR SELECTION’’  are advised to communicate with the institute through mobile numbers  062577774 OR O677777746 OR 0764777746.  Applicants with  ‘‘Prior admission status’’  in their accounts are advised to clear their prior admission status through filling TCU prior admission clearance form .  Unsuccessful applicants for the second round are advised to re-apply for third ro...

LEO SEPTEMBA 10 KATIKA HISTORIA

George Washington, Rais wa Kwanza wa Marekani Leo ni tarehe 10 Septemba siku ya 254 katika mwaka 2016, zimesalia siku 112 kuumaliza mwaka huu 2016. TUANGALIE MATUKIO MUHIMU YALIYOTOKEA TAREHE KAMA YA LEO 210 K.K - Mtawala wa kwanza wa Dola ya Qin (Qin Dynasty) ya nchini China alifariki. 1776 - George Washington aliomba mpelelezi wa siri wa kujitolea, Nathan Hale akajitolea. 1993 - Israel ilisaini mkataba wa utambuzi na PLO. 1919 - Jiji la New York lilimkaribisha nyumbani Jenerali John J. Peshing na wanajeshi wengine 25,000 waliolitumikia jeshi la Marekanj katika vita ya kwanza ya Dunia katika divisheni ya kwanza. 1939 - Canada ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani. 1945 - Vidkun Quisling alihukumiwa kifo kwa kushirikiana na jeshi la Ujerumani Nazi nchini Norway. Aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 1945. 1963 - Wanafunzi weusi 20 (negro) waliruhusiwa kusoma katika shule za serikali za Alabama kufuatia makubaliano kati ya Serikali kuu na Gavana George C. W...

MAREKANI NA URUSI ZAKUBALIANA KUSITISHA MAPIGANO SYRIA

Marekani na Urusi zimefikia makubalinao kuhusu mchakato wa kupatikana amani nchini Syria ikiwemo kusitishwa kwa mapigano kote nchini Syria kuanzia Jumatatu wiki ijayo. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuimarisha shughuli za kutolewa kwa misaada na opereshenzi za pamoja za kijeshi kupambana dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali. Makubaliano hayo yaliyofikiwa mapema Jumamosi (10.09.2016) kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yanafuatia mazungumzo ya kina yaliyokuwa yakifanyika mjini Geneva, Uswisi. Lavrov amesema licha ya kuendelea kutoaminiana kati ya pande hizo mbili, wamefanikiwa kuafikiana kuhusu jinsi ya kushirikiana kupambana dhidi ya ugaidi na kuyafufua mazungumzo ya kisiasa ya kupatikana amani nchini Syria kwa njia bora zaidi. Je mzozo wa Syria utakoma sasa? Kerry ambaye alichelewesha kwa siku moja safari yake kutoka Geneva na kurejea Marekani ili kuhakikisha wamefikia makubaliano na mwenzake wa Urusi a...

LEO AGOSTI 6 KATIKA HISTORIA

Leo ni Agosti 6, 2018 ikiwa ni siku ya 218 katika mwaka 2018. Zimesalia siku 147 katika mwaka huu. Nakukaribisha tena katika muendelezo ya Leo Katika Historia. Kwa leo nimekuletea matukio kadhaa yaliyopata kutokea katika historia ya dunia, na tuanze kuyahesabu matukio hayo: MATUKIO 1787 - Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ilianza kujadiliwa huko Philadelphia. 1890 - Hukumu ya kuuawa kwa kiti cha umeme ilianza kutekelezwa katika gereza la Auburn huko New York, Marekani ambapo William Kemmier alihukumiwa kifo katika kiti cha umeme kwa kumuua mpenzi wake Matilda Ziegler kwa shoka. Adhabu hii ya kifo ilipendekezwa mwaka 1881 na Dk. Albert Southwick baada kushuhudia mlevi akiuawa kwa shoti ya umeme. Katika kutekeleza adhabu hii zilitumika volti 700 za umeme na katika sekunde 17 umeme ulifeli kabla Kemmier hajafariki na baadaye waliongeza umeme hadi volti 1,030 ndani ya dakika 2 na ndipo Kemmier alifariki. Kiti cha Umeme kilichotumika kutekeleza adhabu ya kifo kwa Kemmier. ...

SHAIRI: HEKO LIBERIA

Picha kwa hisani ya Freepik Shairi hili linakuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka huu nchini Liberia. Katika hali isiyo ya kawaida George Weah aliyekuwa akitetea nafasi yake ali kubali kusindwa na mpinzani wake Joseph Boakai katika Uchaguzi huo pasipo mvutano na migogoro kama ilivyozoeleka katika mataifa mengi ya bara hili . Kama mshairi niliwiwa kuandika ili kupongeza kitendo hiki cha uungwana kukubali kukabidhi madaraka pasipo mvutano ambao mara nyingi hupelekea umwagaji damu. Karibu katika shairi letu kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Shairi: Heko Liberia Mtunzi: Venance Gilbert Mpate Mwaka: 19 Novemba 2023 HEKO LIBERIA Heko Liberia naisifu yenu demokrasia, Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia, Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia, Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia, Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia, Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia, Mpinzani akashika dola imani ikaendelea, Heko Liberia naisifu yenu demokrasia. Mtawala aku...