MAREKANI NA URUSI ZAKUBALIANA KUSITISHA MAPIGANO SYRIA
Marekani na Urusi zimefikia makubalinao kuhusu mchakato wa kupatikana amani nchini Syria ikiwemo kusitishwa kwa mapigano kote nchini Syria kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa mapema Jumamosi (10.09.2016) kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yanafuatia mazungumzo ya kina yaliyokuwa yakifanyika mjini Geneva, Uswisi.
Lavrov amesema licha ya kuendelea kutoaminiana kati ya pande hizo mbili, wamefanikiwa kuafikiana kuhusu jinsi ya kushirikiana kupambana dhidi ya ugaidi na kuyafufua mazungumzo ya kisiasa ya kupatikana amani nchini Syria kwa njia bora zaidi.
Je mzozo wa Syria utakoma sasa?
Kerry ambaye alichelewesha kwa siku moja safari yake kutoka Geneva na kurejea Marekani ili kuhakikisha wamefikia makubaliano na mwenzake wa Urusi amesema utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama unajituma zaidi katika kuutatua mzozo wa Syria kwasababu wanaamini Urusi ina uwezo wa kuushinikiza utawala wa Rais wa Syria Bashar al Assad kusitisha vita na kuja katika meza ya mazungumzo ili kupatikane amani nchini humo.
![]() |
Kerry na Lavrov walikutana na maafisa wengine Geneva kuhusu Syria |
Kerry ameongeza kusema kuwa msingi wa mazungumzo hayo ya Geneva ilikuwa ni makubaliano kuwa serikali ya Syria haitafanya mashambulizi ya angani kwa kisingizio cha kuwasaka wapiganaji wa kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa al Nusra Front, linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amesema kusitishwa huko kwa mashambulizi ya angani katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi kutafikisha kikomo matumizi ya mabomu ya mapipa na mashambulizi ya kiholela na ina uwezo wa kubadili mkondo wa mzozo wa Syria.
Marekani na Urusi zimekubaliana iwapo mapigano yatapungua, nchi hizo mbili zitashirikiana kufanya operesheni za kijeshi kwa pamoja dhidi ya Al Nusra na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS.
Chini ya makubaliano hayo pande zote zinazohusika zinapaswa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kote nchini Syria, kusitisha mashambulizi yote yakiwemo ya angani, kutojaribu kuyadhibiti maeneo mapya wakati wa kusitishwa kwa mapigano, kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kufika katika maeneo yaliyozingirwa ikiwemo katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Aleppo.
Umoja wa Mataifa siku ya Ijumma ulisema serikali ya Syria imezuia misafara ya magari ya kutoa misaada ya kibiandamu mwezi huu kuingia katika mji wa Aleppo na mji huo unakumbwa na hatari ya kuishiwa mafuta katika kipindi cha wiki moja ijayo na hivyo kuyafanya mazungumzo kuhusu Syria kushughulikiwa kwa dharura zaidi.
Marekani na Urusi kushirikiana kijeshi
Iwapo hayo yatazingatiwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo, Urusi na Marekani zitaanza siku saba za kazi za maandalizi ya kuunda kituo cha pamoja cha kuteleza shughuli zao za kijeshi Syria ikiwemo kubadilishana taarifa kuhusu maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo na kuhusu makundi ya upinzani.
![]() |
Mwanamke akitathmini uharibifu mjini Aleppo
|
Marekani na Urusi zimekuwa kila moja ikiunga mkono upande tofauti katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria ambavyo havionyeshi dalili ya kukoma hivi karibuni hata baada ya miaka mitano ya mzozo ambao umesababisha nusu ya idadi ya Wasyria kuyahama makaazi yao, maelfu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.
Katika mzozo huo, Urusi inamuunga mkono Rais Bashar al Assad huku Marekani ikiunga mkono upinzani unaotaka kumng'oa madarakani Rais Assad. Pendekezo la Kerry la ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi yake na Urusi limekumbwa na upinzani kutoka kwa maafisa wa Marekani wa ulinzi na wa kijasusi wanaodai Urusi haiwezi kuaminiwa.
Chanzo: DW
LEO SEPTEMBA 10 KATIKA HISTORIA
![]() |
George Washington, Rais wa Kwanza wa Marekani |
TUANGALIE MATUKIO MUHIMU YALIYOTOKEA TAREHE KAMA YA LEO
210 K.K - Mtawala wa kwanza wa Dola ya Qin (Qin Dynasty) ya nchini China alifariki.
1776 - George Washington aliomba mpelelezi wa siri wa kujitolea, Nathan Hale akajitolea.
1993 - Israel ilisaini mkataba wa utambuzi na PLO.
1919 - Jiji la New York lilimkaribisha nyumbani Jenerali John J. Peshing na wanajeshi wengine 25,000 waliolitumikia jeshi la Marekanj katika vita ya kwanza ya Dunia katika divisheni ya kwanza.
1939 - Canada ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani.
1945 - Vidkun Quisling alihukumiwa kifo kwa kushirikiana na jeshi la Ujerumani Nazi nchini Norway. Aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 1945.
1963 - Wanafunzi weusi 20 (negro) waliruhusiwa kusoma katika shule za serikali za Alabama kufuatia makubaliano kati ya Serikali kuu na Gavana George C. Wallace.
1974 - Guinea-Bissau ilipata uhuru wake kamili kutoka kwa Ureno.
1979 - Wanaharakati wanne wa Puerto Rico walihukumiwa kwenda jela kwa kosa la kufanya shambulizi katika Bunge la Wawakilishi nchini Marekani mwaka 1953 na jaribio la kutaka kumuua Rais wa Marekani, Harry S. Truman mwaka 1950. Waliachiwa baadae kwa msaha kutoka kwa Rais Jimmy Carter.
2008 - Jaribio lililoitwa Hadron Collider ambalo ni jaribio kunwa kiwahi kufanyika katika historia ya binadamu lilifanywa huko Geneva, Uswisi.
KUZALIWA
1638 - Malikia Maria Theresa akiwa mke wa Mfalme Lous XIV wa Hispania maarufu kama "Maria Theresa wa Hispania" alizaliwa huko El Escorial nchini Hispania.
1928 - Mwanafalsafa wa Canada, Jean Vanier alizaliwa.
1931 - Muigizaji wa Matekani Philip Baker Hall alizaliwa.
1940 - Mwanamuziki wa Marekani Roy Ayers alizaliwa.
1953 - Muigizaji wa kike wa Marekani Amy Irving alizaliwa.
1957 - Mwanamuziki wa Uingereza Siobhan Fahey alizaliwa.
1958 - First lady wa Canada Margaret Trudeau alizaliwa.
1960 - Muigizaji wa Uingereza Colin Firth alizaliwa.
1968 - Muongozajj wa filamu wa Uingereza Guy Ritchie alizaliwa.
1974 - Muigizaji wa Marekani Ryan Phillippe alizaliwa.
1979 - Muigizaji wa Marekani Jacob Young alizaliwa.
1928 - Mwanafalsafa wa Canada, Jean Vanier alizaliwa.
1931 - Muigizaji wa Matekani Philip Baker Hall alizaliwa.
1940 - Mwanamuziki wa Marekani Roy Ayers alizaliwa.
1953 - Muigizaji wa kike wa Marekani Amy Irving alizaliwa.
1957 - Mwanamuziki wa Uingereza Siobhan Fahey alizaliwa.
1958 - First lady wa Canada Margaret Trudeau alizaliwa.
1960 - Muigizaji wa Uingereza Colin Firth alizaliwa.
1968 - Muongozajj wa filamu wa Uingereza Guy Ritchie alizaliwa.
1974 - Muigizaji wa Marekani Ryan Phillippe alizaliwa.
1979 - Muigizaji wa Marekani Jacob Young alizaliwa.
KWA MSAADA WA MTANDAO
WATU 10 WAMEKUFA KATIKA AJALI YA MOTO KIWANDANI HUKO BANGLADESH
Takribani watu 10 wamekufa katika mlipuko mkubwa wa moto huko Bangladesh kufuatia kulipuka kwa kontena la kuchemshia maji ya moto.
Polisi wamesema kuwa takribani watu 100 walikuwa ndani ya kiwanda hicho chenye jengo la ghorofa 4 ambapo mlipuko ulisikika katika mji wa Tongi.
Takribani watu 30 wamejeruhiwa kutokana na moto huo kusambaa kwa haraka katika jengo hilo.
Huduma za dharura zinadai kuwa moto bado unaendelea kuwaka na inasemekana idadi ya watu kufariki katika ajali hiyo inaweza kuongezeka.
"Mpaka sasa tumepata uhakika wa watu 10 kufariki. Lakini bado idadi inaweza kuongezeka kwa sababu moto bado ni mkali kushindwa kuzimwa." Inspekta wa Polisi Sirajul Islam aliiambia AFP.
Kumekuwa na majanga mengi ya moto viwandani nchini Bangladesh kufuatia kutokuwa na usalama wa kuzuia majanga hayo katika nchi hiyo.
Canzo: BBC
Polisi wamesema kuwa takribani watu 100 walikuwa ndani ya kiwanda hicho chenye jengo la ghorofa 4 ambapo mlipuko ulisikika katika mji wa Tongi.
Takribani watu 30 wamejeruhiwa kutokana na moto huo kusambaa kwa haraka katika jengo hilo.
Huduma za dharura zinadai kuwa moto bado unaendelea kuwaka na inasemekana idadi ya watu kufariki katika ajali hiyo inaweza kuongezeka.
"Mpaka sasa tumepata uhakika wa watu 10 kufariki. Lakini bado idadi inaweza kuongezeka kwa sababu moto bado ni mkali kushindwa kuzimwa." Inspekta wa Polisi Sirajul Islam aliiambia AFP.
Kumekuwa na majanga mengi ya moto viwandani nchini Bangladesh kufuatia kutokuwa na usalama wa kuzuia majanga hayo katika nchi hiyo.
Canzo: BBC
KANSELA ANGELA MERKEL ASEMA UJERUMANI YA SASA NI BORA ZAIDI
![]() |
Kansela Angela Merkel akihutubia bungeni siku ya Jumatano (7 Septemba 2016). |
Vichwa vya habari katika magazeti na ripoti za televisheni na redio mara tu baada ya CDU kushindwa uchaguzi huo wa Jumapili, zilitazamiwa kumrejesha Kansela Merkel nyuma, na hotuba ya leo ilidhaniwa kuwa ingekuwa nyepesi na laini. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa, kwani kwenye hotuba ya bungeni ya leo Jumatano (7 Septemba 2016), ambapo alionekana kusimama imara.
"Hali yetu leo ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita kwetu sote. Hapana shaka, bado kuna mambo ya kufanywa. Changamoto kubwa ikiwa kuwarejesha nyumbani wahamiaji ambao hawawezi kubakia hapa na sisi. Na kwa uadilifu kuwahudumia raia wetu, huku tukiwafahamisha kuwa tunapaswa kuwasiaidia wale wenye haki ya kusaidiwa," aliwaambia wabunge.
Katika hotuba hii, ambayo tayari imeshaonesha kuzua mjadala mkali, Kansela Merkel amesema si kweli kuwa mmiminiko wa mamia kwa maelfu ya wakimbizi nchini Ujerumani utapunguza mafao wanayopata raia wazawa wa Ujerumani, hoja ambayo imekuwa ikitumiwa na wapinzani wake wa kisiasa.
Chama chake, CDU, kiliangushwa kwenye uchaguzi wa mwishoni mwa wiki na chama kinachopinga wahamiaji nchini Ujerumani, AfD, katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern, kwa hoja hiyo hiyo dhidi ya wakimbizi.
Wapigakura kwenye jimbo hilo walitumia nafasi hiyo kumuonesha kutokubaliana na sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi na wahamiaji kutoka mataifa yenye Waislamu wengi, hasa baada ya matukio kadhaa ya mashambulizi kwenye miji ya kusini mwa Ujerumani, lakini kwenye hotuba yake ya leo bungeni, Kansela Merkel amesema ugaidi si jambo linalohusiana moja kwa moja na wakimbizi.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki wakiwa kwenye mkutano wa kilele wa mataifa ya G20, mjini Hangzhou, China.
![]() |
Makubaliano na Uturuki ni sahihi
Sambamba na hilo, alitetea pia namna anavyoliendea suala la mahusiano kati ya nchi yake na Uturuki, akiwakosoa wale wanaomwambia ameshinda kulaani hatua kali za ukandamizaji zinazochukuliwa na utawala wa Rais Tayyip Erdogan baada ya jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa mwezi Julai.
Merkel amesema makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Uturuki yaliyolenga kuzuia mmimiko wa wahamiaji yalikuwa hatua muhimu na inayoweza baadaye kuigizwa kama msingi wa makubaliano na mataifa mengine.
Mdahalo wa jioni ya leo kuhusiana na hotuba hii iliyoshadidia msimamo na muelekeo wa Kansela Merkel kwa masuala ya wakimbizi, usalama, na sera yake ya nje unatazamiwa kuwa mkali sana.
Tayari msuguano ndani ya serikali yake ya muungano umeshadhihirika, huku mshirika wake mkuu, chama cha SPD kikionekana kujipanga kumpiku.
Upinzani mkali pia umo ndani ya chake mwenyewe cha CDU, huku chama ndugu cha CSU kikiwa tangu mwanzoni mbali sana na sera ya wakimbizi ya Kansela Merkel.
Chanzo: DW
TCU IMEFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA AWAMU YA PILI
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imefungua tena dirisha la udahiri kwa Wanafunzi wanaoomba kuchaguliwa katika kozi mbalimbali za Shahada ya Kwanza mwaka huu wa masomo 2016/2017. Linasomeka hivi:
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe
31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba
udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali
mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe
12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
• Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
• Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
• Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana
na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
• Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na
matokeo yao yameshatoka,
• Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
• Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo
vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za
kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016.
Unaweza kusoma zaidi kwa KUBOFYA HAPA
RAIS WA UZBEKISTAN AZIKWA KWA HESHIMA YA DINI YA KIISLAMU
Karimov, mwenye umri wa miaka 78 na ambaye ameiongoza Uzbekistan kwa muda mrefu, alifariki dunia jana Ijumaa baada ya kuugua kiharusi mwishoni mwa wiki iliyopita. Waziri Mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev anatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayofanyika kwa heshima ya dini ya Kiislamu.
Mazishi hayo pia yatahudhuriwa na viongozi wengine wa mataifa ya iliyokuwa Umoja wa Kisovieti, akiwemo Rais wa Tajikistan, Emmomali Rakhmon, Rais wa Turkmenistan, Gurbanguly Berdymukhamedov na Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan, Belarus na Kazakhstan. Rais wa Marekani, Barack Obama ameelezea kusikitishwa na kifo hicho na amethibitisha kwamba nchi yake iko tayari kuwasaidia wananchi wa Uzbekistan katika kipindi hiki.
Waombolezaji wajipanga barabarani
Uvumi ulianza kuzagaa siku chache zilizopita kuwa kiongozi huyo amefariki dunia, lakini kifo chake kilithibitishwa rasmi hapo jana. Maelfu ya wananchi wa Uzbekistan wameanza kujipanga tangu mapema asubuhi ya leo, huku waombolezaji wengi wakiwa wamebeba maua waridi, ambayo wamekuwa wakiyaweka kwenye barabara. Waziri Mkuu wa Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev, ameteuliwa kuwa kiongozi wa kusimamia mazishi ya Karimov, hatua inayoonyesha kuwa huenda akawa rais ajaye wa nchi hiyo.
Mapema jana, serikali ya Uturuki ilitoa salamu za rambirambi kutokana na msiba huo. Akizungumza katika mkutano na baraza la mawaziri, Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim amesema wanaungana na watu wa Uzbekistan katika kipindi hiki cha majonzi. Aidha, katika taarifa yake aliyoitoa jana Rais wa Urusi, Vladmir Putin amekielezea kifo cha Karimov kama pigo kubwa kwa watu wa Uzbekistan.
Karimov ameitawala nchi hiyo ya Asia ya Kati tangu mwaka 1989 akiwa kama mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti na mwaka 1991 alikuwa rais wa Uzbekistan wakati nchi hiyo ilipokuwa huru kutokana na kuvunjika kwa uliokuwa Umoja wa Kisovieti. Karibu ya nusu ya raia milioni 32 wa Uzbekistan, walizaliwa wakati wa utawala wake.
Wengi wanamchukulia Karimov kama kiongozi dikteta kutokana na maamuzi ya kikatili aliyoyafanya wakati wa utawala wake na serikali yake imekuwa ikishutumiwa kwa kukiuka haki za binaadamu. Steve Swerdlow mtaalamu kutoka Shirika la kimataifa la haki za binaadamu, Human Rights Watch Asia ya Kati, anasema kuwa Karimov alikuwa na utawala wa kimabavu, kwani aliwafunga gerezani na kuwatesa wapinzani na mahasimu wake kisiasa. Kwa mujibu wa Swerdlow, kiongozi huyo aliamuru jeshi kuwapiga risasi waandamanaji katika mji wa mashariki wa Andijan mnamo mwaka 2005, mauaji mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
Hadi sasa kiongozi huyo wa kimabavu hana mrithi kamili, hali inayozusha wasiwasi kwamba kifo chake kinaweza kusababisha kukosekana kwa hali ya utulivu. Mtoto mkubwa wa kike wa Karimov, ambaye alionekana kama anaandaliwa kuchukua nafasi ya baba yake, hajaonekana hadharani tangu mwaka 2014, huku kukiwa na uvumi kwamba yuko katika kizuizi cha nyumbani. Amekuwa akishutumiwa na waendesha mashtaka wa nchini Marekani na Ulaya, kwa kuhusika na rushwa.
Mtoto wa pili wa kike wa Karimov, Lola Karimov-Tillyaeva, ni balozi wa Uzbekistan katika shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO. Nchi ya Uzbekistan ina utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, gesi asilia na pia ni msafirishaji mkubwa wa pamba.
Chanzo: Deutsche Welle (DW)
NEW VIDEO: ANGALIA VIDEO YA RAYMOND-NATAFUTA KIKI HAPA
Hatimaye Raymond a.k.a. RayVanny wa WCB Wasafi Classic ameachia video ya wimbo wake Natafuta kiki. Production ya video imefanyika Kwetu studios ya hapa hapa Tz. Pata nafasi ya kuangalia video hiyo hapa.
ACTION MUVI MPYA INATOKA AGUST 2, SNIPER: GHOST SHOOTER
Muvi inaitwa Sniper: Ghost Shooter inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 2 Agost mwaka huu (siku chache kutoka leo kama siku 5 mbele).
Imechezwa na Chad Michael Collins, Billy Zane, Dennis Haysbert na wengine wengi.
STORI KWA UFUPI
Masnaipa wenye akili Chad Collins (katika muvi hii ameigiza kama Brandon Beckett) na Billy Zane (katika muvi hii anaitwa Richard Miller) wanapewa jukumu la kulinda bomba la gesi ili lisiharibiwe na magaidi. Wanapokuwa katika mambano na maadui inapelekea masnaipa wenzao wengine kuuawa na adui asiyefahamika alipo lakini yeye akiwa anafahamu wao (Richard na Brandon) walipojificha. Hofu inazidi kutanda hadi kufikia safu ya ulinzi kushutumiwa kushirikiana na maadui. Kuna mmoja kati yao anashirikiana na upande wa maadui? Je, mpango ni mwanzo wa mpango mwingine kumjua msaliti? Je, Kanali atatumia muda mwingi kuamua nini kifanyike? Haya yote utayapata katika muvi hii Sniper: Ghost Shooter kuanzia Agost 2, mwaka huu katika tovuti na application za kupakua muvi mpya.Wasiliana nami.
LIKE VENANCE BLOG ON FACEBOOK
NIFOLO KWENYE TWITTER
NIFOLO INSTAGRAM
CHADEMA 'YAIBIPU' POLISI
Ni wazi sasa kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kujipima nguvu na Jeshi la Polisi baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu.
Kamati Kuu hiyo katika maazimio yake yaliyosomwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ilisisitiza kuwa azma yake hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kupinga agizo la jeshi hilo la kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Sababu nyingine zilizoisukuma Kamati Kuu kufikia azma hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ni pamoja na kupinga zuio la urushwaji wa moja kwa moja wa mijadala ya Bunge, kupinga wabunge wa upinzani kudhibitiwa bungeni, kuingiliwa kwa mhimili wa mahakama, upuuzwaji wa utawala wa sheria na haki ya kupata habari.
Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya Chadema imezindua operesheni Ukuta yenye lengo la kupambana na kile ilichokiita kuwa ni udikteta nchini, huku ikitangaza kushirikiana na wale tu watakaoona umuhimu wa kuwepo kwa haki na demokrasia nchini.
Mbowe aliyeambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, aliagiza maagizo hayo kupewa umuhimu na ngazi zote za chama hicho kuanzia vijiji, kata, majimbo, wilaya, mikoa, kanda, mabaraza hadi taifa.
Alisema Jeshi la Polisi nchini limeamua kuvidhibiti vyama vya siasa ili visiweze kufanya mikutano ya kisiasa, wakati serikali inaongozwa na viongozi ambao ni wanasiasa na ambao wamekuwa wakifanya kazi zao za kisiasa kupitia nafasi zao za kiserikali.
Mwenyekiti huyo wa Chadema Taifa alisema katika maandalizi ya mikutano hiyo, chama hicho kitafuata taratibu, kanuni na sheria zinazostahili ili waweze kupata ruhusa huku akisisitiza kwamba si nia ya chama hicho kuanzisha vurugu, bali kutumia haki ya msingi ya kukosoa akisema ndiyo njia sahihi ya kufuatwa katika ukuzaji wa haki na demokrasia nchini.
Alisema Kamati Kuu imeagiza ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi, kata, majimbo, wilaya, mikoa, kanda, mabaraza na Taifa kukaa vikao vyake vya kikatiba haraka na ajenda za vikao hivyo iwe ni kujadili maandalizi ya mikutano hiyo ya hadhara, kujadili hali ya siasa na pia hali ya uchumi nchini.
Alisema Kamati Kuu imewataka wanasheria wa chama hicho wakiongozwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kukaa na kuyatazama mambo yote ambayo yametokea na kuchukua hatua za kisheria kwa lengo la kuyatafutia suluhisho la kisheria.
“Inaonekana kwamba wao ndio wana haki lakini sio sisi. Viongozi wetu wakubali kukosolewa na waamini kuwa taifa ni letu sote, hali ya sasa imesababisha Taifa kuwa lenye uoga wa kupindukia,” alisema na kuongeza kuwa Septemba mosi ni siku ya kukata misingi ya uonevu wa demokrasia.
Kuhusu ni nini kitazungumzwa na viongozi wa chama hicho katika mikutano hiyo ya hadhara Mbowe alisema kwa kifupi; “Lazima tufanye mikutano ya hadhara. Tutaelezana namna ya kukatiza mto pindi tutakapoufikia.
” Kuhusu operesheni Ukuta, Mbowe alisema jana ni siku ya kwanza ya utekelezaji wa operesheni hiyo yenye maana ya ‘Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania’ huku akisisitiza kuwa inatokana na chama hicho kutokuwa tayari kuruhusu nchi kuongozwa nje ya misingi ya demokrasia.
Alisema kupitia operesheni hiyo chama hicho kitashirikiana na wale wote ambao wanaona umuhimu wa kuzingatiwa kwa misingi ya haki na demokrasia, na kuongeza kuwa hiyo haina maana kwamba chama hicho hakiungi mkono hatua za serikali katika kupambana na matendo maovu nchini.
Kauli yapingana na agizo la Polisi
Msimamo huo wa Chadema ni wazi kwamba sasa utakifanya chama hicho kukabiliana na Jeshi la Polisi ambalo limezuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya kisiasa nchini.
Agizo hilo la Jeshi la Polisi lilitolewa na Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo, Nsato Mssanzya. “Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
“Aidha vyama vingine vya siasa vimeonesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao. Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.
“Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Juni 7, mwaka huu hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa. Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. “Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii,” alisema Kamishna Mssanzya katika agizo hilo la Jeshi la Polisi.
Katika tukio jingine, Mwandishi Wetu John Mhala kutoka Arusha anaripoti kwamba wabunge wawili na wenyeviti wawili wa Chadema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Karatu bila ya kibali.
Waliokamatwa na polisi ni pamoja na Mbunge wa Karatu, Willey Kaboroo (58) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha kupitia chama hicho, Cecilia Pareso (35).
Wengine waliokamatwa na kuhojiwa na polisi Arusha kwa zaidi ya saa tatu ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Jubilet Mnyenye (55) na Makamu wake Lazoro Kajuta ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ganako.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema kuwa viongozi hao walifanya mkutano wa hadhara Julai 23, mwaka huu, bila kufuata tararibu kama inavyotakiwa.
Kamanda Ilembo alisema wabunge hao na wenyeviti hao wa halmashauri waliamua kukiuka taratibu za kufanya mkutano wa hadhara hivyo polisi iliamua kuwaita na kuwahoji sababu za kushindwa kufuata tararibu.
Alisema wamefunguliwa jalada la uchunguzi na wote wamehojiwa na kuachiwa kwa dhamana yao wenyewe na upelelezi wa shauri hilo unaendelea.
Hata hivyo, wabunge hao na wenyeviti baada ya kuhojiwa walisema kuwa wamesikitishwa na hatua ya kuitwa polisi na kuhojiwa kwa kufanya mikutano ya hadhara wakati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu alikuwa anajua kila kitu.
Chanzo: Habari Leo
WAZIRI MKUU WA NEPAL KHADGA PRASAD OLI AMEJIUZURU
Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli amejiuziru wadhifa wake ikiwa ni muda mchache kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la nchi hiyo. Inadaiwa katika kura hiyo Oli angeshindwa.
Oli mwenye umri wa miaka 64 alishinikizwa kujiuzuru na wapinzani wa chama chake kufuatia kutoheshimu mgawanyo wa madaraka ambao ndiyo uliompa Uwaziri mkuu miezi 9 iliyopita.
"Nimekwisha wasilisha barua yangu ya kujiuzuru kwa Rais nilipokutana naye kabla hata ya Bunge" amesikika akisema Oli aliponukuliwa na The Reuters katika Bunge la Nepal.
Oli aliyezaliwa kaskazini mwa Nepal Fenruari 22 mwaka 1952 alikuwa mwanachawa wa Nepal Communist Party mwaka 1970 baada ya kuvutiwa na viongozi wa kikomunisti alipokuwa kijana.
Amewahi kutumikia kifungo cha miaka 14 jela.
Oli aliingia madarakani Oktoba mwaka jana huku akikosolewa sana na kuwepo kwa maandamano kufuatia kushindwa kuchukua hatua katika tetemeko lililowaacha wananchi katika umaskini mkubwa.
Zaidi ya watu 50 waliuawa katika mvutano kati ya polisi na waandamanaji waliopinga katiba ambayo ilikuwa inawakandamiza kisiasa mwezi Desemba mwaka jana.
Katiba mpya ilitakiwa kudumisha amani na kuchochea mabadiliko nchini Nepal kwenda katika utwala wa kidemokrasia baada ya kupitia katika hali ya hatari kwa miongo kadhaa, serikali ilishindwa kuafikiana na waandamanaji licha ya kuwepo mijadala mbalimbali kusuluhisha mgogoro huo.
Mabadiliko serikalini Nepal sio kitu kigeni kukiwa na Oli waziri mkuu wa 8 katika miaka 10 iliyopita.
Rejendra Daahl mshauri wa zamani wa Rais Ram Baran Yadav amesema kuwa uamuzi wa Oli kujiuzulu ulikuwa usisubiriwa sana Nepal.
"Katika miaka 25 iliyopita hii ilikiwa ni serikali ya 22 ya Nepal na bado tunatarajia serikali nyingine mbili katika kipindi cha Bunge hili kwa hivyo hii ni hali ya sintofahamu ya kisiasa".
"Itachukia majuma kadhaa na labda miezi kadhaa kuunda serikali mpya". Daahl aliiambia Al Jazeera.
Rais Bidhya Devi Bhandari anatarajiwa kupiga hatua nyingine ambapo inamaana kwba anaweza kuiomba serikali ya Oli kuendelea kubaki madarakani mpaka pale serikali mpya itakapopatikana au ataita vyama kuunda serikali kwa makubaliano.
Chanzo: Al Jazeera
SATELITE YA JUNO YAFIKA KATIKA SAYARI YA JUPITA
![]() |
Satelite ya Juno ikiwa imewasili katika sayari ya Jupita. |
Satelite ya Juno inayokuwa inayoongozwa taasisi ya Utafiti wa Anga NASA iliyoko nchini Marekani imefanikiwa kufika katika sayari ya Jupita ambayo ni sayari ya tano katika mfumo wa jua kutoka kwenye jua.
Satelite hiyo ya Juno iliondoka duniani miaka mitano iliyopita ambayo ilikuwa na rocket engine kuiongoza satelite hiyo mpaka kuifika satelite hiyo..
Wattafiti wanapanga kuitumia satelite hiyo kuichunguza sayari hiyo kwa jina. Wanadai kuwa muonekano wa sayari hiyo na kemia yake unaweza kuichunguza zaidi sayari hii ambayo ni kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua toka ilipotengenezwa zaidi ys miaka bilioni 4 na nusu iliyopita.
Hakuna chombo kilichofanikiwa kupita au kuisogelea sayari hiyo ya Jupita kutokana na mionzi iliyopo katika sayari hii kama chombo hicho hakijalindwa na vifaa maalumu vya kieletroniki ambavyo vinazuia mionzi hiyo kupenya.
Mahesabu ya haraka yanaonesha kuwa satelite hiyo imeundwa kwa miyonzi zenye X Ray zinazokadiriwa kuwa zaidi ya milioni. Kabla chombo hicho hakijafikia mwisho wa electron za kujilinda, chombo hiyo inatakwa ianze kuichunguza sayari hiyo mapema baada ya kuwasili katika sayar hyo.
Satelite ya Juno kama inavyoonekana angani. |
Rocket ya pili ambayo inatarajiwa kuanza kuungua katikati ya mwezi wa kumi mwaka huu itaungua hasa kwa muda wa siku 14 na ndipo hapo sasa utafiti utanza rasmi.
Juno iitataumia vifaa vyake 8 vya kuhisi pamoja na kamera kuelekea katika ukanda wa gesi chini ya sayari hiyo ili kupima vlivyounda sayari hiyo, joto na mambo mengne. Utafiti huo utsisitizwa zaidi katika ugunduzi wa uwepo wa hewa ya Oksijeni pamoja na maji.
"Ni kwa kiasi gani sayari hii itakuwa na maji kitatuekeza ni lini sayari hii iliundwa katka mfumo wa jua" alieleza Candy Hansen mmoja wa timu ya Juno.
MAMBO 8 UNAYOTAKIWA KUYAFAHAMU
- Sayari hii ina ukubwa mara 11 ya ukubwa wa Dunia yetu tunayoishi.
- Inaichukua dunia mara 12 kulizunguka jua katika mhimili wake; siku inakuwa na masaa 10.
- Katika kuundwa kwake inafanana na nyota; imeundwa sana kwa gesi ya Oksijeni na Haidrojeni.
- Katika mgandamizo wa hewa wa kawaida Haidrojeni inakadiriwa kuwa gesi ya ambayo inaconduct umeme.
- Hii metallic haidrojeni ni chanzo kikuu cha utepe wa kimagnetic.
- Mawingu mengi yanaonekana kuwa yameundwa na gesi ya Amonia na Haidrojeni Salfaidi.
- Sayari ya Jupita ina upepo mkali unaotoka mashariki kwenda magharibi.
- The Great Red Spot is a giant storm vortex twice as wide as Earth.
NASA wamepanga kukiongoza chombo hicho hadi mwezi wa pili mwaka 2018 (Februari) ambapo bado mionzi hiyo itakuwa haijakiharibu chombo hicho. Kamera yake inakadiriwa kupungua uwezo miezi michache ijayo.
Kama ilivyo katika tafiti kwenye sayari zilizopita, utafiti katika sayari hii utaishia katika kuchunguza tabaka la hewa lilipo katika sayari hiyo.
Chanzo: BBC
MAN WATER AELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA WAKONGWE KWENYE MUZIKI
Producer Man Water wa combinataion sound, ameelezea sababu ya kupenda kuwarudisha wasanii wa kitambo kwenye game, ambao tayari walishapotea kimuziki.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Water amesema hupenda kufanya hivyo kwani ana imani wasanii hao bado wana uwezo mkubwa, na kwa kuwa alitoka nao mbali kikazi.
“Kurudisha wasanii waliopotea mimi na kuwa nao karibu kwa sababu ni watu wangu ambao nimetoka nao mbali, najua hustle zao tulipita wote, na kwa sababu mi mwenzao bado nimebaki kwenye game, sasa nikiwaita wale nawaambia jinsi gani game ya sasa ilivyo na wabadilike vipi ili waweze kurudi”, alisema Man Water.
Man Water alishawahi kumrudisha kwenye game msanii 20% , Alikiba, Lady Jaydee na wengine, huku bado akiwa na mpango wa kuendelea kuwarudisha wasanii wengine kama Mr. Nice.
Chanzo: EATV
MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA
Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya
ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi
uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo.
Katika
maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo
wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini
maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya
kwanza ya masalio hayo.Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo.
Chanzo: BBC