MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA
Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya
ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi
uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo.
Katika
maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo
wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini
maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya
kwanza ya masalio hayo.Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment