WAZIRI MKUU WA NEPAL KHADGA PRASAD OLI AMEJIUZURU


Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli amejiuziru wadhifa wake ikiwa ni muda mchache kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la nchi hiyo. Inadaiwa katika kura hiyo Oli angeshindwa.

Oli mwenye umri wa miaka 64 alishinikizwa kujiuzuru na wapinzani wa chama chake kufuatia kutoheshimu mgawanyo wa madaraka ambao ndiyo uliompa Uwaziri mkuu miezi 9 iliyopita.

"Nimekwisha wasilisha barua yangu ya kujiuzuru kwa Rais nilipokutana naye kabla hata ya Bunge" amesikika akisema Oli aliponukuliwa na The Reuters katika Bunge la Nepal.

Oli aliyezaliwa kaskazini mwa Nepal Fenruari 22 mwaka 1952 alikuwa mwanachawa wa Nepal Communist Party mwaka 1970 baada ya kuvutiwa na viongozi wa kikomunisti alipokuwa kijana.

Amewahi kutumikia kifungo cha miaka 14 jela.

Oli aliingia madarakani Oktoba mwaka jana huku akikosolewa sana na kuwepo kwa maandamano kufuatia kushindwa kuchukua hatua katika tetemeko lililowaacha wananchi katika umaskini mkubwa.

Zaidi ya watu 50 waliuawa katika mvutano kati ya polisi na waandamanaji waliopinga katiba ambayo ilikuwa inawakandamiza kisiasa mwezi Desemba mwaka jana.

Katiba mpya ilitakiwa kudumisha amani na kuchochea mabadiliko nchini Nepal kwenda katika utwala wa kidemokrasia baada ya kupitia katika hali ya hatari kwa miongo kadhaa, serikali ilishindwa kuafikiana na waandamanaji licha ya kuwepo mijadala mbalimbali kusuluhisha mgogoro huo.

Mabadiliko serikalini Nepal sio kitu kigeni kukiwa na Oli waziri mkuu wa 8 katika miaka 10 iliyopita.

Rejendra Daahl mshauri wa zamani wa Rais Ram Baran Yadav amesema kuwa uamuzi wa Oli kujiuzulu ulikuwa usisubiriwa sana Nepal.

"Katika miaka 25 iliyopita hii ilikiwa ni serikali ya 22 ya Nepal na bado tunatarajia serikali nyingine mbili katika kipindi cha Bunge hili kwa hivyo hii ni hali ya sintofahamu ya kisiasa".

"Itachukia majuma kadhaa na labda miezi kadhaa kuunda serikali mpya". Daahl aliiambia Al Jazeera.

Rais Bidhya Devi Bhandari anatarajiwa kupiga hatua nyingine ambapo inamaana kwba anaweza kuiomba serikali ya Oli kuendelea kubaki madarakani mpaka pale serikali mpya itakapopatikana au ataita vyama kuunda serikali kwa makubaliano.



Chanzo: Al Jazeera

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017