Posts

MOVIE MPYA KATI YA SEPTEMBA 15 HADI 19

Image
Hii ni orodha ya muvi mpya zitakazooneshwa kwenye Cinema kuanzia Septemba 15 hadi Septemba 19 na baadae kuanza kuuzwa na kusambazwa kwingineko duniani. Nimekusogezea movie mpya 9 ambazo kama wewe ni mfuatiliajia, mpenzi na muangaliaji unaweza kununua pindi zitakapotoka. Hii inatwa BLAIR WITCH itaoneshwa kwenye Cinema Septemba 15 na baadae kusambazwa duniani. Ndani wapo James Allen McCune,  Callie Hernandez na Corbin Reid. Hiii inaitwa BRIDGET JONES' BABY. Hii itakuwa tayari kuoneshwa kwenye Cinema Septemba 16. Ndani wapo  Renèe Zellweger, Colin Firth na Patrick Dempsey. Hii inaitwa SNOWDEN. Itaoneshwa kwenye Cinema Septemba 16. Ndani yake kuna Joseph Gordon-Levitt, Shailene Woodley na Merissa Leo. Hii inaitwa MR. CHURCH. Itaoneshwa kwenye Cinema Septemba 16. Ndani wapo Edson Murphy, Britt Robertson na Madison Wolfe. Hii inaitwa THE GOOD NEIGHBOR. Itaoneshwa kwenye Cinema Septemba 16. Ndani wapo James Caan, Logan Miller na Keir Gilrchrist. Hii inaitwa T...

MAREKANI NA URUSI ZAKUBALIANA KUSITISHA MAPIGANO SYRIA

Image
Marekani na Urusi zimefikia makubalinao kuhusu mchakato wa kupatikana amani nchini Syria ikiwemo kusitishwa kwa mapigano kote nchini Syria kuanzia Jumatatu wiki ijayo. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuimarisha shughuli za kutolewa kwa misaada na opereshenzi za pamoja za kijeshi kupambana dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali. Makubaliano hayo yaliyofikiwa mapema Jumamosi (10.09.2016) kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yanafuatia mazungumzo ya kina yaliyokuwa yakifanyika mjini Geneva, Uswisi. Lavrov amesema licha ya kuendelea kutoaminiana kati ya pande hizo mbili, wamefanikiwa kuafikiana kuhusu jinsi ya kushirikiana kupambana dhidi ya ugaidi na kuyafufua mazungumzo ya kisiasa ya kupatikana amani nchini Syria kwa njia bora zaidi. Je mzozo wa Syria utakoma sasa? Kerry ambaye alichelewesha kwa siku moja safari yake kutoka Geneva na kurejea Marekani ili kuhakikisha wamefikia makubaliano na mwenzake wa Urusi a...

LEO SEPTEMBA 10 KATIKA HISTORIA

Image
George Washington, Rais wa Kwanza wa Marekani Leo ni tarehe 10 Septemba siku ya 254 katika mwaka 2016, zimesalia siku 112 kuumaliza mwaka huu 2016. TUANGALIE MATUKIO MUHIMU YALIYOTOKEA TAREHE KAMA YA LEO 210 K.K - Mtawala wa kwanza wa Dola ya Qin (Qin Dynasty) ya nchini China alifariki. 1776 - George Washington aliomba mpelelezi wa siri wa kujitolea, Nathan Hale akajitolea. 1993 - Israel ilisaini mkataba wa utambuzi na PLO. 1919 - Jiji la New York lilimkaribisha nyumbani Jenerali John J. Peshing na wanajeshi wengine 25,000 waliolitumikia jeshi la Marekanj katika vita ya kwanza ya Dunia katika divisheni ya kwanza. 1939 - Canada ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani. 1945 - Vidkun Quisling alihukumiwa kifo kwa kushirikiana na jeshi la Ujerumani Nazi nchini Norway. Aliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 1945. 1963 - Wanafunzi weusi 20 (negro) waliruhusiwa kusoma katika shule za serikali za Alabama kufuatia makubaliano kati ya Serikali kuu na Gavana George C. W...

WATU 10 WAMEKUFA KATIKA AJALI YA MOTO KIWANDANI HUKO BANGLADESH

Image
Takribani watu 10 wamekufa katika mlipuko mkubwa wa moto huko Bangladesh kufuatia kulipuka kwa kontena la kuchemshia maji ya moto.  Polisi wamesema kuwa takribani watu 100 walikuwa ndani ya kiwanda hicho chenye jengo la ghorofa 4 ambapo mlipuko ulisikika katika mji wa Tongi. Takribani watu 30 wamejeruhiwa  kutokana na moto huo kusambaa kwa haraka katika jengo hilo. Huduma za dharura zinadai kuwa moto bado unaendelea kuwaka na inasemekana idadi ya watu kufariki katika ajali hiyo inaweza kuongezeka. "Mpaka sasa tumepata uhakika wa watu 10 kufariki. Lakini bado idadi inaweza kuongezeka kwa sababu moto bado ni mkali kushindwa kuzimwa." Inspekta wa Polisi Sirajul Islam aliiambia AFP. Kumekuwa na majanga mengi ya moto viwandani nchini Bangladesh kufuatia kutokuwa na usalama wa kuzuia majanga hayo katika nchi hiyo. Canzo: BBC

KANSELA ANGELA MERKEL ASEMA UJERUMANI YA SASA NI BORA ZAIDI

Image
Kansela Angela Merkel akihutubia bungeni siku ya Jumatano (7 Septemba 2016). Licha ya chama cha CDU kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi la kwao la Mecklenburg-Vorpommern kutokana na sera yake ya wahamiaji, Kansela Angela Merkel anasema sera yake ni sahihi na kamwe hatarudi nyuma. Vichwa vya habari katika magazeti na ripoti za televisheni na redio mara tu baada ya CDU kushindwa uchaguzi huo wa Jumapili, zilitazamiwa kumrejesha Kansela Merkel nyuma, na hotuba ya leo ilidhaniwa kuwa ingekuwa nyepesi na laini. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa, kwani kwenye hotuba ya bungeni ya leo Jumatano (7 Septemba 2016), ambapo alionekana kusimama imara. "Hali yetu leo ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita kwetu sote. Hapana shaka, bado kuna mambo ya kufanywa. Changamoto kubwa ikiwa kuwarejesha nyumbani wahamiaji ambao hawawezi kubakia hapa na sisi. Na kwa uadilifu kuwahudumia raia wetu, huku tukiwafahamisha kuwa tunapaswa kuwasiaidia wale wenye haki ya kusaidiwa," aliwaambi...

TCU IMEFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA AWAMU YA PILI

Image
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imefungua tena dirisha la udahiri kwa Wanafunzi wanaoomba kuchaguliwa katika kozi mbalimbali za Shahada ya Kwanza mwaka huu wa masomo 2016/2017. Linasomeka hivi: TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU) TAARIFA KWA UMMA Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili. • Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza • Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza • Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati, • Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka...

RAIS WA UZBEKISTAN AZIKWA KWA HESHIMA YA DINI YA KIISLAMU

Image
Rais wa Uzbekistan, Islam Karimov amezikwa leo kwenye mji wa nyumbani kwake wa Samarkand, ulioko katikati ya nchi hiyo, wakati ambapo taifa hilo limeanza siku tatu za maombolezo ya nchi nzima. Karimov, mwenye umri wa miaka 78 na ambaye ameiongoza Uzbekistan kwa muda mrefu, alifariki dunia jana Ijumaa baada ya kuugua kiharusi mwishoni mwa wiki iliyopita. Waziri Mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev anatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayofanyika kwa heshima ya dini ya Kiislamu. Mazishi hayo pia yatahudhuriwa na viongozi wengine wa mataifa ya iliyokuwa Umoja wa Kisovieti, akiwemo Rais wa Tajikistan, Emmomali Rakhmon, Rais wa Turkmenistan, Gurbanguly Berdymukhamedov na Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan, Belarus na Kazakhstan. Rais wa Marekani, Barack Obama ameelezea kusikitishwa na kifo hicho na amethibitisha kwamba nchi yake iko tayari kuwasaidia wananchi wa Uzbekistan katika kipindi hiki. Waombolezaji wajipanga barabarani Uvumi ulianza kuzagaa siku chache zilizopita kuwa kiongozi h...

NEW VIDEO: ANGALIA VIDEO YA RAYMOND-NATAFUTA KIKI HAPA

Image
Hatimaye Raymond a.k.a. RayVanny wa WCB Wasafi Classic ameachia video ya wimbo wake Natafuta kiki. Production ya video imefanyika Kwetu studios ya hapa hapa Tz. Pata nafasi ya kuangalia video hiyo hapa.   

ACTION MUVI MPYA INATOKA AGUST 2, SNIPER: GHOST SHOOTER

Image
Muvi inaitwa Sniper: Ghost Shooter inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 2 Agost mwaka huu (siku chache kutoka leo kama siku 5 mbele). Imechezwa na Chad Michael Collins, Billy Zane, Dennis Haysbert na wengine wengi. STORI KWA UFUPI Masnaipa wenye akili Chad Collins (katika muvi hii ameigiza kama Brandon Beckett) na Billy Zane (katika muvi hii anaitwa Richard Miller) wanapewa jukumu la kulinda bomba la gesi ili lisiharibiwe na magaidi. Wanapokuwa katika mambano na maadui inapelekea masnaipa wenzao wengine kuuawa na adui asiyefahamika alipo lakini yeye akiwa anafahamu wao (Richard na Brandon) walipojificha. Hofu inazidi kutanda hadi kufikia safu ya ulinzi kushutumiwa kushirikiana na maadui. Kuna mmoja kati yao anashirikiana na upande wa maadui? Je, mpango ni mwanzo wa mpango mwingine kumjua msaliti? Je, Kanali atatumia muda mwingi kuamua nini kifanyike? Haya yote utayapata katika muvi hii Sniper: Ghost Shooter kuanzia Agost 2, mwaka huu katika tovuti na application za kupakua muvi...

CHADEMA 'YAIBIPU' POLISI

Image
Ni wazi sasa kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kujipima nguvu na Jeshi la Polisi baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu. Kamati Kuu hiyo katika maazimio yake yaliyosomwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ilisisitiza kuwa azma yake hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kupinga agizo la jeshi hilo la kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Sababu nyingine zilizoisukuma Kamati Kuu kufikia azma hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ni pamoja na kupinga zuio la urushwaji wa moja kwa moja wa mijadala ya Bunge, kupinga wabunge wa upinzani kudhibitiwa bungeni, kuingiliwa kwa mhimili wa mahakama, upuuzwaji wa utawala wa sheria na haki ya kupata habari. Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya Chadema imezindua operesheni Ukuta yenye lengo la kupambana na kile ilichokiita kuwa ni udikteta nchini, huku ikitangaza kus...

WAZIRI MKUU WA NEPAL KHADGA PRASAD OLI AMEJIUZURU

Image
Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli amejiuziru wadhifa wake ikiwa ni muda mchache kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la nchi hiyo. Inadaiwa katika kura hiyo Oli angeshindwa. Oli mwenye umri wa miaka 64 alishinikizwa kujiuzuru na wapinzani wa chama chake kufuatia kutoheshimu mgawanyo wa madaraka ambao ndiyo uliompa Uwaziri mkuu miezi 9 iliyopita. "Nimekwisha wasilisha barua yangu ya kujiuzuru kwa Rais nilipokutana naye kabla hata ya Bunge" amesikika akisema Oli aliponukuliwa na The Reuters katika Bunge la Nepal. Oli aliyezaliwa kaskazini mwa Nepal Fenruari 22 mwaka 1952 alikuwa mwanachawa wa Nepal Communist Party mwaka 1970 baada ya kuvutiwa na viongozi wa kikomunisti alipokuwa kijana. Amewahi kutumikia kifungo cha miaka 14 jela. Oli aliingia madarakani Oktoba mwaka jana huku akikosolewa sana na kuwepo kwa maandamano kufuatia kushindwa kuchukua hatua katika tetemeko lililowaacha wananchi katika umaskini mkubwa. Zaidi ya watu 50 wali...

BARAZA LA MITIHANI LIMETANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016

Image
Matokeo ya Kidato cha Sita 2016 yametoka, unaweza kuyaona kwa kubofya  HAPA

SATELITE YA JUNO YAFIKA KATIKA SAYARI YA JUPITA

Image
Satelite ya Juno ikiwa imewasili katika sayari ya Jupita. Satelite ya Juno inayokuwa inayoongozwa taasisi ya Utafiti wa Anga NASA iliyoko nchini Marekani imefanikiwa kufika katika sayari ya Jupita ambayo ni sayari ya tano katika mfumo wa jua kutoka kwenye jua. Satelite hiyo ya Juno iliondoka duniani miaka mitano iliyopita ambayo ilikuwa na rocket engine kuiongoza satelite hiyo mpaka kuifika satelite hiyo.. Wattafiti wanapanga kuitumia satelite hiyo kuichunguza sayari hiyo kwa jina. Wanadai kuwa muonekano wa sayari hiyo na kemia yake unaweza kuichunguza zaidi sayari hii ambayo ni kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua toka ilipotengenezwa zaidi ys miaka bilioni 4 na nusu iliyopita. Hakuna chombo kilichofanikiwa kupita au kuisogelea sayari hiyo ya Jupita kutokana na mionzi iliyopo katika sayari hii kama chombo hicho hakijalindwa na vifaa maalumu vya kieletroniki ambavyo vinazuia mionzi hiyo kupenya. Mahesabu ya haraka yanaonesha kuwa satelite hiyo imeundwa kwa miyonzi zenye...

MAN WATER AELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA WAKONGWE KWENYE MUZIKI

Image
Producer Man Water wa combinataion sound, ameelezea sababu ya kupenda kuwarudisha wasanii wa kitambo kwenye game, ambao tayari walishapotea kimuziki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Water amesema hupenda kufanya hivyo kwani ana imani wasanii hao bado wana uwezo mkubwa, na kwa kuwa alitoka nao mbali kikazi. “Kurudisha wasanii waliopotea mimi na kuwa nao karibu kwa sababu ni watu wangu ambao nimetoka nao mbali, najua hustle zao tulipita wote, na kwa sababu mi mwenzao bado nimebaki kwenye game, sasa nikiwaita wale nawaambia jinsi gani game ya sasa ilivyo na wabadilike vipi ili waweze kurudi”, alisema Man Water. Man Water alishawahi kumrudisha kwenye game msanii 20% , Alikiba, Lady Jaydee na wengine, huku bado akiwa na mpango wa kuendelea kuwarudisha wasanii wengine kama Mr. Nice. Chanzo: EATV

MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA

Image
Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo. Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo. Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo. Chanzo: BBC