Posts
(NEW VIDEO) SNURA - NIMEVURUGWA
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
August 2013 ndio Snura aliishusha single yake ya ‘nimevurugwa’ kwenye radio za bongo ikiwa ni miongoni mwa single zinazopata airtime bila kuwa na video lakini leo November 22 2013 kaishusha video on AyoTV… itazame hapa chini na uache maoni yako mtu wangu, atapita hapa baada ya saa 6. Snura alisema kwenye video ya ‘majanga’ hakuweza kucheza kama inavyotakiwa lakini huku kwenye ‘nimevurugwa’ ndio kajiachia
BONY M-MARYS BORN CHILD SONG LYRICS
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Mary's boy child, Jesus Christ, was born on Christmas Day And man will live forevermore because of Christmas Day Long time ago in Bethlehem, so the Holy Bible said Mary's boy child, Jesus Christ, was born on Christmas Day Hark, now hear the angels sing, a king was born today And man will live forevermore because of Christmas Day Mary's boy child, Jesus Christ, was born on Christmas Day While shepherds watch their flocks by night They see a bright new shining star They hear a choir sing a song, the music seemed to come from afar Hark, now hear the angels sing, a king was born today And man will live forevermore because of Christmas Day Mmh-mmh Mmh-hmm Mmh-mmh Mmh-mmh-hmm Mmh-mmh-mmh-hmm Mmh-hmm-mmh-mmh For a moment the world was aglow, all the bells rang out There were tears of joy and laughter, people shouted "Let everyone know, there is hope for all to find peace" Oh my Lord You sent Your son to save us Oh my Lord Your very self You gave us Oh my Lord That sin m...
KNOW ABOUT BIG RESULTS NOW ON EDUCATION IN TANZANIA
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Improving education is of high importance to Tanzania – it is a strategic agent for development for the country. With this perspective, significant efforts have been made to increase access for all, resulting in a huge enrollment expansion over the last ~10 years. Over the same period of time quality of education dropped significantly. To address this challenge and reverse the trend, the education lab has focused on finding ways to raise the quality of basic education, and has set a very ambitious target to improve pass rates1 in primary and secondary schools to 60% in 2013, 70% in 2014 and 80% in 2015 Among several drivers of quality, the lab team has analyzed the most important challenges, and gone through an extensive prioritization effort to determine the focus areas that will give Big Results Now. Among the top issues we have addressed are lack of accountability, availability of teaching and learning materials, low support for struggling students and poor school ...
QUOTES BY BRUCE LEE
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
1. Love is like a friendship caught on fire. In the beginning a flame, very pretty, often hot and fierce, but still only light and flickering. As love grows older, our hearts mature and our love becomes as coals, deep-burning and unquenchable. 2. Always be yourself, express yourself, have faith in yourself, do not go out and look for a successful personality and duplicate it. 3. Mistakes are always forgivable, if one has the courage to admit them. 4. I fear not the man who has practiced 10,000 kicks once, but I fear the man who has practiced one kick 10,000 times. 5. If you love life, don't waste time, for time is what life is made up of. 6. A wise man can learn more from a foolish question than a fool can learn from a wise answer. 7. If you always put limit on everything you do, physical or anything else. It will spread into your work and into your life. There are no limits. There are only plateaus, and you must not stay there, you must go beyond them. ...
QUOTES BY BOB MARLEY
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
1. My music fights against the system that teaches to live and die. 2. Get up, stand up, Stand up for your rights. Get up, stand up, Don't give up the fight. 3. Me only have one ambition, you know. I only have one thing I really like to see happen. I like to see mankind live together - black, white, Chinese, everyone - that's all. 4. The good times of today, are the sad thoughts of tomorrow. 5. I don't stand for the black man's side, I don' t stand for the white man's side. I stand for God's side. 6. If you're white and you're wrong, then you're wrong; if you're black and you're wrong, you're wrong. People are people. Black, blue, pink, green - God make no rules about color; only society make rules where my people suffer, and that why we must have redemption and redemption now. 7. The greatness of a man is not in how much wealth he acquires, but in his integrity and his ability to affect those around him pos...
MWILI WA NELSON MANDELA KUZIKWA LEO KIJIJINI KWAKE QUNU
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
NDEGE ya kijeshi aina ya C-130 Hercules iliyobeba mwili wa Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini, ilitua Uwanja wa Ndege wa Mthatha jana majira ya saa 6.37.Ikisindikizwa na ndege nyingine mbili za kijeshi, iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Waterkloof, Pretoria saa 4:58, tayari kwa safari ya mwisho ya kuuhifadhi mwili wa Mandela kwa maziko kijijini kwake Qunu katika Jimbo la Eastern Cape.Mwili wa mwanamapinduzi huyo kipenzi cha dunia, unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya familia ya Mandela, shughuli inayotarajiwa kuanza saa 3 asubuhi.Shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, alifariki dunia Alhamisi ya Desemba 5, 2013 saa 2:50 usiku nyumbani kwake, Mtaa wa Laa Namba 12, Houghton jijini Johannesburg akiwa amezungukwa na wanafamilia wote, wakiwemo mkewe Graca Machel na mtalaka wake, Winnie Medikizela –Mandela na mtoto wake mkubwa, Makaziwe Mandela.Tayari Serikali imetangaza leo kuwa siku ya mapumziko, ili kuwawezesha wananchi kufuatilia maziko ya kiongozi h...
BBC YALAUMIWA KUVUNJA VIPINDI KWA AJILI YA MSIBA WA MANDELA
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Wakati Dunia ikifuatilia kwa karibu safari ya mwisho ya Mandela hapa duniani, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripotiwa kuingia lawamani kutokana na uamuzi wake wa kupangua vipindi vingi na kuweka matangazo ya moja kwa moja ya mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ambaye kabla ya kuingia Ikulu, alisota gerezani kwa miaka 27 kutokana na harakati zake zilizowakera makaburu. Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti kuwa, watazamaji na wasikilizaji 1,834 wa redio na televisheni za BBC, wamelalamikia matangazo mfululizo ya mazishi ya Mandela. Mmoja wa wabunge wa chama cha Conservative, Conor Burns amekaririwa akisema hakukuwa na ulazima wa BBC kutumia muda mwingi na pia kupoteza fedha za walipa kodi kutuma wanahabari wanane kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya vipindi vya mahojiano katika shughuli ya kumuaga Mzee Mandela.“Tunafahamu heshima ya Mzee Mandela, alikuwa mmoja wa viongozi wa kipekee katika karne ya 20 na 21. Ametufundisha mengine ju...
ZITTO AKERWA KUITWA MUONGO BUNGENI
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, amesema anatarajia kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu, kauli ya Mwanasheria Mkuu aliyoitoa juzi bungeni dhidi yake na kumuita muongo kuhusu suala la kuwa na orodha ya watu wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi.Zitto, aliyasema hayo bungeni juzi, ikiwa ni siku moja tu baada ya Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, kudai mbele ya Bunge kuwa Serikali inashughulikia kisheria suala la Zitto kudanganya Bunge na Kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi.Akizungumza na HabariLeo Jumapili, Zitto alisema kwa sasa hataki kuzungumzia suala hilo, ila ukweli wote ataubainisha kwenye maelezo yake binafsi ambayo atayawasilisha wiki ijayo kwenye mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea.“Nimeamua hili suala nilizungumzie ndani ya Bunge, kwa hiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye Ofisi ya Bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitakibainisha siku hiyo, sina zaidi,” alisisitiza Zitto....
POLISI WAKAMATA BASTOLA NYUMBA YA KULALA WAGENI
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
JESHI la Polisi wilayani Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kukamata bastola katika nyumba ya kulala wageni ambayo inadhaniwa imesahaulika na majambazi.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Tabora, Peter Ouma alisema silaha hiyo imekamatwa juzi katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Sophia Lodge iliyopo mtaa wa Bank, Igunga mjini.Alisema kuwa bastola hiyo yenye namba za usajili 224335 aina ya Browing Court ilidakwa na risasi 38 pamoja na magazini 4.
KENYA YASHEREHEKIA MIAKA 50 YA UHURU
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Kenya jana ilisherehekea miaka 50 ya uhuru walioupata chini ya utawala wa Uingereza.Mamia ya raia na wageni mbali mbali wamehudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika katika mji mkuu wa Nairobi.Wageni mbali mbali pamoja marais wa mataifa mbali mbali wamehudhuria sherehe hizo akiwemo Rais Godluck Jonathan wa Nigeria, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Joseph Kabila wa DRC, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Ali Bongo wa Gabon, Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka.Usiku wa kuamkia Alhamis bendera ya Kenya ilipandishwa katika eneo hilo hilo siku bendera ya uhuru ilipopandishwa wakati nchi hiyo inapata uhuru katika bustani ya Uhuru Desemba 12, 1963.Siku hiyo ya uhuru Rais Jomo Kenyatta, baba yake rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitawazwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.
KINGEREZA CHAMCHANGANYA MKALIMANI AFRIKA KUSINI
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbukumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa ikidanganya kwa miaka mingi na imekuwa ikitoa watafsiri wenye kiwango cha chini. Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne. Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali. Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa. Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo imetupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu. Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyanty kutoka kampuni ya SA Interpreters."Mtafsiri huyo anazungumza lug...
AJALI: BASI LAUA WATU 12 PAPO HAPO
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
Watu 12 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Korogwe, Tanga kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea jana saa 1.30 asubuhi kwenye barabara kuu ya Segera-Chalinze katika kijiji cha Kwalaguru kata ya Kwedizinga wilayani hapa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo ya basi la Burudani namba T 610 ATR aina ya Nissan. Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga, kwa matibabu ya awali na miili ya marehemu, akiwamo dereva wa gari hilo, Luta Mpenda (35) imehifadhiwa hospitalini hapo. “Tukiwa tunakaribia kwenye kona ile, tulipishana na lori hilo likiwa kasi upande wetu, dereva wetu akajitahidi kulikwepa lakini kutokana na ile kona kuwa kali, gari lilimshinda na kupinduka,” alisema Bendera. Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema walisikia kishindo kutoka eneo hilo wakaenda na kukuta gari limepinduka na baadh...
PINDA: NITAFURAHI NIKIONDOLEWA
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda uwaziri mkuu ni mzigo anaobeba kama Msalaba na ikiwa ataondolewa, atafurahi kwa kuwa atapumzika. Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kassim Mohamed (CUF), katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo.“Rais akiniambia nimeshindwa majukumu nitaondoka, huku nikiwa na kicheko, hata ninyi wabunge mna nafasi ya kuniondoa, mnaweza kufanya hivyo mkiona inafaa kwani nitafurahi na kupumzika,” alisema.Rukia katika swali lake, alimtaka Pinda kutoa ufafanuzi kuhusu kauli za wabunge wa CCM kuwa yeye ndiye mzigo. Alisema licha ya jitihada anazofanya kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia wizara 20, anashangaa kuhukumiwa kwa upungufu unaotokea katika wizara moja au mbili.Alifafanua, kuwa anasimamia wizara kama 20 na zote zinafanya kazi vizuri, lakini kama kuna wizara moja au mbili hazijafanya vizuri sana, hiyo haitoshi kudai atimuliwe kazi.Alisema uzuri wa nafasi ya uwaziri mkuu, mtu haombi, bali anateuliwa na Rais kwa majaaliw...
UGANDA YAANZA KUILIPA TANZANIA FIDIA
- Get link
- X
- Other Apps
Written by
Venance Gilbert
-
SERIKALI ya Uganda tayari imeshaanza kulipa deni lake kwa Tanzania la dola za Marekani milioni 9.6 kati ya dola za Marekani milioni 18.4 ikiwa ni fidia kwa Tanzania kwa mchango wake katika kumuondoa Idd Amin Dada Uganda mwaka 1978.Hayo yalibainishwa bungeni jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Shamsi Vuai Nahodha, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mbinga, John Komba (CCM).Katika swali lake Komba alitaka kujua kama Tanzania ilishaanza kudai fidia kwa Serikali ya Uganda kutokana na mchango wake wa kuisaidia nchi hiyo kumuondoa Idd Amin na kumfanya Rais wa sasa Yoweri Museveni kutawala kwa amani nchini humo.Akijibu swali hilo, Nahodha alikiri kuwa Tanzania ilipigana vita na Uganda kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 1979 kutokana na uvamizi uliofanywa na Uganda chini ya utawala wa Idd Amin aliyevamia na kukalia sehemu ya ardhi ya Tanzania mkoani Kagera.“Kwa kuwa vita hivyo vilitokana na uvamizi wa Idd Amin, baada ya vita kumalizika Serikali ya Tanzania iliitaka Uga...