Fikiria ulikuwa unafanya kazi katika taasisi ya maendeleo na kupunguza umasikini mwanzoni mwa miaka ya 1990. Mwandishi wa makala hii, Abhas Jha anasema yeye aliwahi kufanya kazi zama hizi. Anasema kipindi hicho kulikuwa na tovuti moja tu iliyokuwepo duniani mpaka kufikia Agosti mwaka 1991 (leo kuna zaidi ya tovuti bilioni 1.5 duniani kote). Anasema kipindi hicho simu za mkononi zilikuwa ghali sana, chache na zilikuwa nzito na za kishamba sana ukilinganisha na hizi za sasa. Ni watu wachache wangetazamia kuhusu hali iliyopo nchini India kwa sasa kwamba kungekua na idadi kubwa ya simu za mkononi kuilko idadi ya vyoo.
Bill Gates aliwahi kusema "tunayapa uzito sana mabadiliko ambayo yatatokea ndani ya kipindi cha muda mfupi sana na kuyapuuza yale yaliyotokea kwa muda mrefu sana". Teknolojia inakua kwa kasi sana na kufanya na mabadiliko makubwa sana kwenye majiji ili kufikisha huduma kwa jamii. Teknolojia inafanya hivi ili sio tu kufikisha huduma haraka kwa wateja bali pia kukuza uchumi na kuimarisha namna ya kufanya mikakati ya kuboresha njia za kuongeza ufanisi wa kifedha.
Hizi hapa ni teknolojia 7 zilizofanya na zitakazokuja kufanya mabadiliko makubwa sana katika majiji duniani na kufanya mabadiliko ya ufikishaji wa huduma kwa wateja:
1. TEKNOLOJIA YA MTANDAO (INTERNET) YA 5G
5G inasimama kwa kumaanisha "kizazi cha tano". Hii ni teknolojia ambayo itatumika kwa simu za mikononi na kompyuta kurahisisha uharaka wa mtanadao, inategemewa kuanza kutumika rasmi kuanzaia mwaka 2020 kwa sasa bado iko katika majaribio. Itakuwa na uwezo mara 40-60 ya uwezo wa teknojia ya sasa ya mtandao wa simu za mkononi. Benki ya Dunia inasema kwamba "kwa ongezeko la 10% la kasi ya mtandao, uchumi utaongezeka kwa 1.3% na kupelekea kile kinachoitwa kitaalamu uhuru wa ugunduzi. Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Benki ya Dunia wanasema kwamba "kama 40% tu ya watu wote wangetumia mtandao duniani, tungeweza kuongeza pato la dunia kwa kiasi cha dola za Marekani $1 trilioni kwa kuunganisha watu wengine milioni 327". Mtandao wa 5G utasaidia matumizi madogo, matumizi madogo ya vifaa vya kuhisi (sensor) ambavyo vitawekwa kwenye majengo, magari, vifaa vingine n.k. Kiufupi utakuwa ni "mtandao wa muunganiko wa vitu" yaani Internet of Things (ToT)
Benki Kuu ya Dunia inakubaliana na miradi mikubwa ambayo ufikishwaji wake unategemea mtandao kwa mfano mradi mkubwa unaojulikana kama BridgeIT nchini Tanzania unaofanya urahisishaji wa kuangalia video za kidijitali madarasani wakati wa kufundisha na kujifunza kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi. Mtandao wa 5G utarahisisha sana matumizi ya mambo haya na mengineyo.
2. TEKNOJIA YA MALIPO YA KIFEDHA "BLOCKCHAIN"
Hii ni teknolojia ya malipo ambayo inafanywa na bitcoin. Teknolojia hii itaweza kurahisisha malipo kama jinsi mtandao unavyofanya kufikisha taarifa kwa haraka zaidi. Lengo la teknolojia hii ni kusambaza mifumo ambayo itasaidia kufanya malipo kwa njia ya mtandao kwa haraka ziadi hata ya mifumo mingine kama Western Union, PayPal, MasterCard na VISA. Hii itasaidia miamala ya kifedha kufanyika bila kuwepo na upatanishi kwa mfano kupitia soko la hisa ambayo kwa sasa inafanya kazi kama mpatanishi wa miamala.
Teknolojia hii inatumiaka kwa matumizi mbalimbali kama vile kurahisisha usajili wa maeneo na kurahisisha usalama wa chakula nchini China. Benki ya Dunia inasema imechapisha makala ambayo inaitambua teknolojia hii kama kichocheo cha maendeleo ya kimataifa. Pia teknolojia hii imesaidia kuwalipa mamilioni ya watu wanaofanya michezo ya upatu mtandaoni na hata wale wanaofanya baadhi ya kazi za bitcoin.
3. TEKNOLOJIA YA AKILI BANDIA "ARTIFICIAL INTELLIGENCE" INAYOHUSISHA KUJIFUNZA KWA VIFAA "MACHINE LEARNING" NA DATA KUBWA "BIG DATA"
Kuna baadhi ya wataalamu kama Stephen Hawking (mtaalamu wa Fizikia aliyefariki Machi 14 mwaka huu) na Elon Musk waliowahi kuonya dhidi ya matumizi ya teknolojia hii ambayo ina madhara makubwa baadaye. Wengine kama vile Fei-Fei Li, ambaye ni profesa wa Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu Stanford anasema kwamba "tunakaribia kwenye mashine ya kufua kuliko kuharibu mambo" akiwa na maana kwamba tunaelekea kwenye urahisi zaidi wa mambo kuliko hatari ambazo watu wanafikiria kuhusu teknolojia hii.
Aliongezea kwamba teknolojia hii ya akili bandia "Artificial Intelligence" na data kubwa, ni teknolojia ambazo zinarahisisha urahisi wa mambo hasa katika majiji ambayo yanahitaji matumizi makubwa ya data kama vile Shanghai, Hong Kong, Sydney na New York hususani katika maeneo ambayo yanafanya maegesho ya magari kwa teknolojia hii, kusimamia ubora wa hewa na kuongeza matumizi ya nishati katika majengo makubwa na marefu.
Kwanza, tufahamu Artificial Intelligence na Machine Learning ni nini? Artificial Intelligence ama kwa ufupi AI kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni Akili Bandia, inaitwa hivi kwa vile Akili Asilia anayo mwanadamu tu. AI ni matokeo ya Akili Asilia. Pia, Machine Learning (ML) ama kwa tafsiri yangu nyepesi Ujifunzaji wa Vifaa kwa Kujazwa Taarifa ni tokeo la AI. Kwa hivyo AI na ML ni dhana mbili zinazokwenda sambamba, dhana hizi zinahusika na utengenezaji wa kanuni ambazo zinaruhusu Kompyuta kufanya kazi ambazo zinahitaji akili ya mwanadamu. AI ni uwanda mpana wa Sayansi ya Kompyuta ambao unalenga kutengeneza mifumo inayoweza kufanya kazi ambazo zikifanywa na mwanadamu huhitaji akili. Mambo hayo ni utatuzi wa changamoto, ufahamu na utambuzi wa lugha, kutambua kanuni na mifumo ya asili na kufanya maamuzi. AI ipo katika aina mbili: Akili Bandia Nyembamba (Narrow AI) ambayo imetengenezwa na kufunzwa kwa kazi mahsusi na Akili Bandia ya Jumla (General AI) ambayo iko na utambuzi na sifa zote za akili ya mwanadamu.
ML ni kipengele cha AI ambacho kinahusika na utengenezaji wa kanuni (algorithms) ambazo zinaruhusu Kompyuta kujifunza na kufanya maamuzi kutokana na taarifa zinawekwa katika kifaa husika. Badala ya kujazwa taarifa za kufanya kazi mahsusi, kanuni za ML zinatumia njia za kitakwimu kujifunza mambo mbalimbali kutokana na taarifa zinazowekwa katika kifaa husika. Kuna aina kadhaa za ML ambazo nitazitaja tu kwa lugha ya kigeni:
(i) Supervised Learning
(ii) Unsupervised Learning
(iii) Reinforcement Learning
AI na ML zinatumika katika uwanda mpana wa mambo mengi mathalani:
• Utambuzi wa Sauti na Uzungumzaji (Voice and speech recognition) kwa mfano katika huduma kama Siri au Google Assistant.
• Utambuzi wa Picha (Image recognition)
• Vipimo vya Kitabibu (Medical diagnosis)
• Utabiri wa masuala ya fedha (Financial forecasting)
• Njia tofauti za masoko (Personalized marketing)
• Gari zinazojiendesha (Self-driving cars) na mengine mengi.
Na pili, tuangalie Big Data ama kwa tafsiri yangu nyepesi nimeamuia kuita Data Kubwa. Kwa maana nyepesi kabisa data kubwa ni taarifa ambazo ni kubwa (kama jina lenyewe) na hivyo huwa ni changamoto kuzipangilia, kuzichakata na kuzichanganua kwa kutumia njia za kawaida/asili za uchanganuzi wa taarifa. Big data inasifika kwa kuhusu mambo matatu ambayo ni ukubwa (volume), kasi (volume) na namna nyingi (variety). Matumizi ya data kubwa yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi, kuchochea umaizi (insights) na maendeleo. Big data inasaidia katika nyanja zifuatazo:
(i) Afya, hapa teknolojia hii inasaidia kutabiri mlipuko wa magonjwa (disease outbreak prediction), namna ya kuboresha huduma ya afya kwa wagonjwa (optimized patient care), ugunduzi wa dawa (drug discovery) na mengine mengi.
(ii) Fedha, benki na taasisi nyingine za kifedha zinatumia teknolojia hii kugundua udanganyifu (fraud detection), kupima madhara (risk assessment), upangiliaji wa taarifa za kibiashara kutokana na mapendeleo ya mtu (algorithmic trading) na mgawanyo wa mateja (customer segmentation)
(iii) Elimu, taasisi na majukwaa ya kielimu yanatumia biga data kufahamu maendeleo ya wanafunzi katika masomo (student performance), kuboresha njia za ujifunzaji (personalized learning paths) na kutabiri kiwango cha idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kuendelea na masomo (dropout rates).
(iv) Kilimo, wakulima wanatumia teknolojia hii kufanya kilimo kuwa cha kisasa (precision agriculture) ambacho kinatumia taarifa za kiteknolojia ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza hasara zitokanazo na shughuli za kilimo. Teknolojia hii inawasaidia wakulima kupitia picha za satelaiti kuhusu upatikanaji au ukosefu wa mvua na majanga ya asili, vifaa vinavyohisi (sensor) katika kilimo, matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) katika kilimo hasa upuliziaji wa madawa ili kuboresha uzalishaji na matumizi ya raslimali.
(v) Mauzo, big data inasaidia watoa huduma za mauzo kufahamu vitu wapendavyo wateja (customer preference), kuboresha mikakati ya mauzo (optimize pricing strategies), kusaidia ugunduzi (managing inventory) na ufikishaji wa huduma za masoko kwa wateja wa aina tofauti kwa njia mbalimbali (tailor marketing campaigns)
(vi) Burudani, big data inatumika kupendekeza mambo ya kutazama/kusikiliza kwa watazamaji wa huduma za mtandaoni (streaming) kulingana upendeleo wa mtazamaji na historia ya mambo aliyotazama katika kwa mfano watumiaji wa YouTube, Netflix, Hulu, Amazon Prime Video, Max, Disney+, Apple TV+, Spotify, Tidal, Apple Music, Paramount+ n.k. Hapa teknolojia hii inapendekeza nyimbo na picha mjongeo (video) pamoja na filamu ama michezo ya kuigiza (drama series)
(vii) Nishati, kampuni zinatumia big data kufahamu vifaa ambavyo vimeshindwa kufanya kazi (equipment failure), kuboresha namna ya usambazaji wa nishati (optimize energy distribution) na matumizi ya njia za nishati zisizo na madhara katika mazingira na zinazoweza kutumika kwa ufanisi (integrate renewable sources efficiently)
(viii) Uboreshaji wa miji na majiji, teknolojia hii inasaidia mipango miji (urban planning), upatikanaji wa hewa safi (monitoring air quality), uboreshaji wa huduma za usafiri wa umma (optimize public transport) na usafi wa miji (waste management).
(ix) Viwanda, big data inasaidia viwandani kufahamu vifaa vinavyohitaji matengenezo (predict maintenance), kuhakikisha ubora ya bidhaa inayozalishwa kiwandani (product quality assurance) na uboreshaji wa mnyororo wa thamani (supply chain optimization).
(x) Mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram n.k. hutumia teknolojia hii kupendekeza maudhui anayoweza kuyapenda mtumiaji wa mtandao (tailor content suggestion), kufahamu maudhui yanayotazamwa au kufuatiliwa sana (detecting trending topics) na kupendekeza matangazo kulingana na tabia za mtumiaji wa mtandao (target advertisments)
(xi) Usafirishaji, teknolojia hii inasaidia kuboresha safari (route optimization), kupendekeza matengenezo ya vyombo vya usafirishaji (predictive maintenance of vehicles) na uchanganuzi wa taarifa za barabarani ili kupunguza msongamano barabarani na ucheleweshwaji wa huduma (analyzing traffic patterns to reduce congestion)
(xii) Michezo, walimu wa mpira wa miguu (coaches) na timu zao wanatumia big data kufahamu ufanisi wa wachezaji (evaluate player performance), kuboresha mikakati ya mchezo (strategize game plans), na kufatilia maendeleo na hatua za kumnunua na kumuajiri mchezaji katika timu (scouting and player recruitment)
(xiii) Biashara mtandao (E-commerce), watoa huduma za mauzo mtandaoni huchanganua taarifa za watumiaji (analyze customer behavior), kuboresha matokeo ya utafutaji wa bidhaa au huduma (optimize search results) na ufikishaji wa huduma za masoko kwa wateja wa aina tofauti kwa njia mbalimbali (tailor marketing campaigns)
Hayo ni machache katika mengi ambayo teknolojia hii imesaidia utendaji kazi wa mambo kadha wa kadha.
4. TEKNOLOJIA YA MAGARI YANAYOJIENDESHA "AUTONOMOUS VEHICLES (AV)"
Licha ya kuwepo taarifa ya hivi karibuni kuhusu kifo cha mtembea kwa miguu kugongwa na gari linalojiendesha, teknolojia hii bado itakuwa ni ya kushangaza na bora zaidi na itakuwa na matokeo mazuri sana katika majiji makubwa na kwingineko ulimwenguni.
Mwaka 2016 John Zimmer ambaye ni miongoni mwa waanzilishi na Rais wa kampuni ya Lyft ambayo inahusika na utengenezaji wa magari hayo alichapisha chapisho refu ambapo alidai kuwa teknolojia hii ya magari yanayojiendesha itachukua nafasi ya teksi ndani ya miaka 5 na mpaka kufikia mwaka 2025 umiliki binafsi wa gari nchi Marekani katika majiji makubwa utafikia kikomo kutokana na teknolojia hii ya magari kuanza kutumika katika majiji hayo. Nimeamua kuiita teknolojia hii kama teknolojia ya magari huru kutokana na kutoendeshwa na mtu; ni magari yanayojiongoza yenyewe.
5. TEKNOLOJIA YA BEI RAHISI YA UTAFITI WA ANGA "LOW-COST SPACE EXPLORATION"
Kampuni ya Elon Musk, Heavy Reusable Rocket inao uwezo wa kutengeneza roketi kwa gharama za dola za Marekni 1000. Hii ni teknolojia ambayo itakuwa ni ya kushangaza na kurahisisha sana utafiti wa anga kwa maisha ya mwanadamu. Musk ana wazo la kufanya utafiti wa usafiri wa anga kutoka jiji moja hadi jingine kwa kutumia roketi ambayo kwa mawazo yake ni kwamba ingerahisisha kwenda mahala popote duniani ndani ya saa moja tu kwa kutumia teknolojia hii.
Kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya tafiti ya Gartner, zaidi ya vitu bilioni 20 vitakuwa vimeunganishwa dunia nzima mpka kufikia mwaka 2020. Wanadai kuwa teknolojia hii itashirikiana na ile ya OneWeb ili kusambaza satelaiti ndogo ili kuunda mkusanyiko ambao utafanikisha kutataua changamoto kubwa ya kutoa urahisi wa kuunganisha watu zaidi ya bilioni 4 duniani kote kuwa na urahisi wa kupata huduma ya mtandao kwa wale ambao wasingefikiwa na huduma hii kutokana na kuwa katika maeneo ambayo mtandao ungekuwa kitendawili kwao. Huduma hii pia itaunganisha mambo bilioni 20 ambao yataletwa na teknolojia ya Mtandao wa Muunganiko wa Vitu "Internrt of Things (IoT)"
6. TEKNOLOJIA YA UTAMBUZI YA KIELEKTRONIKI-BAIOMETRIKI (BIOMETRIC) INAYOHUSISHA VITAMBULISHO VYA KISASA (DIGITAL ID) NA MALIPO YA KISASA (DIGITAL PAYMENTS)
Idara ya Utambuzi kwa Mandeleo ya Benki ya Dunia (ID4D) imekediria kwamba takribani watu bilioni 1.1 hawana uwezo wa kuhakiki vitambulisho vyao (hii ni sawa na mtu 1 katika kila mkusanyiko wa watu 7) Haya ni mabadiliko ya haraka sana. Idara ya Aadhar nchini India imesajili takribani watu bilioni 1.1. Kwa kuruhusu Aadhar kama mfumo rasmi wa vitambulisho, kulingana na utafiti mmoja, kiwango cha ushirikishwaji wa kifedha nchini India umeongezeka kwa 24% miongoni mwa wanawake kati ya mwaka 2014 na 2015. Kwa pamoja, makadirio yanaonesha kuwa akaunti takribani milioni 22o zilifunguliwa kufiki April 2016.
Kuunganisha malipo kwa mfumo huu kumesidia kufanya malipo ya ruzuku na pesa na mabo mengine kwa kutumia vitambylisho vya baiometriki kumepunguza udanganyifu, ujanja ujanja na rushwa kwa mfano kutambua watumishi hwa nchini Nigeria.
Mfumo wa Vitambulisho vya kisasa unaohusisha na progamu za simu za mkononi pia ulianzishwa nchini Algeria, Cameroon, Jordan, Italia, Senegal na Thailand ukienda sambamba na tangazo la kuwepo kwa matumizi ya mpango huu nchini Uholanzi, Bulgaria, Norway, Liberia, Poland, Jamaica na Sri Lanka pamoja na kujaribiwa jijini Mynmar nchini Burma. Teknolojia hii kwa sasa inahusisha mfumo ya kibaiometriki kwa mfumo wa alama za vidole (fingerprint).
7. TEKNOLOJIA YA VIFAA VYA ANGA VISIVYO NA WAONGOZAJI NDANI YAKE "UNMANNED AERIAL VEHICLES (UAVs) mathalani Drones
UAVs ni vifaa ambavyo vinajiongoza bila kuendeshwa na rubani ndani yake aidha kwa kuongozwa na mtu aliyeko chini au katika kifaa kingine ama kuongozwa na Kompyuta iliyoko ndani ya kifaa husika. Hii ni teknolojia ambayo kwa sasa imesaidia sana upatikanaji wa taarifa ndani ya muda mfupi sana hasa hasa kwa kamera ambazo huongozwa kwa kutumia rimoti. Mawasiliano yanakuwepo baina ya kamera hii na muongozaji ambaye anakua ardhini kuiongoza kamera hiyo. Wakati mwingine kamera hii inaweza kujiongoza yanyewe kwa kutumia kompuya inayokuwa ndani ya kamera hiyo. Teknolojia hii ilisaidia kupata taarifa kuhusu mafuriko yaliyosumbua jiji la Dar es Salaam mwezi April mwaka 2018.
Changamoto ya teknolojia hii ni nguzo za umeme, miti mirefu na upepo mkali ambavyo ni vikwazo vinavyozuia kamera hizi kwenda umbali mrefu sana. Kama kunakuwa hakuna vikwazo hivi, kamera hizi zinauwezo wa kusafiri kulingana jinsi kilivvyowekewa umbali husika.
Ndege zisizo na rubani (Drones) zimesaidia katika mambo mengi kwa sasa mathalani upuliziaji wa dawa na uangalizi wa afya ya mazao mashambani, ulinzi na usalama, upigaji picha za matukio mbalimbali, ukaguzi wa madaraja, nguzo za umeme, ufikishaji wa huduma kwa wateja na uangalizi wa mazingira hasa misitu, mbuga na kufatilia mabadiliko ya kimazingira.
Benki ya Dunia ina uwezo wa kufanya jambo la msingi katika teknolojia hizi ili kuhakikisha kuwa zinatumiaka kote duniani na kuzingatia kuwa hata masikini hawaachwi mbali sana na teknolojia hii. Kwa kuhitimisha ni kwamba Ripoti ya Mendeleo Duniani ya mwaka 2016 kuhusu mgawanyo wa teknolojia ya kisasa unatoe masomo matatu:
1. Kutumia data ili kulenga maeneo ambayo yako mbali sana na upatikanaji wa mtandao kama jinsi Sao Paulo walifanya kuwa na taarifa za kijografia kufanya kipaumbele kuhusu makazi.
2. Kufungua data ili kurahisisha uwazi hii ikijumuisha kuwa na ramani za vitu, uchafuzi na mahitaji ya jamii huko Kiberia, eneo ambalo halina makazi yaliyipangiliwa jijini Nairobi; na
3. Kuwepo na teknolojia ya kuunganisha simu za mkononi ili kurahisisha ushiriki wa wanchi kama jinsi majiji ya nchini Ufilipino kwa kushirikisha wananchi wake katika bajeti za majiji hayo.
MAKALA HII IMENDALIWA NA BENKI YA DUNIA NA KUTAFSIRIWA NA KUONGEZWA MANENO MENGINE NA VENANCE BLOG.
MAWASILIANO
barua pepe: venancegilbert@gmail.com
simu: 0753400208
0 comments:
Post a Comment