MIAKA 5 YA VENANCE BLOG NAWASHUKURU SANA KUWEPO HAPA TANGU KUANZISHWA KWAKE MEI 2013
VENANCE BLOG ilianzishwa Mei 2, 2013. |
Alhamis ya tarehe 2 Mei, 2013 nilitimiza kiu yangu ya kufungua Blog hii, lilikuwa ni wazo lililoishi toka mwaka 2012 nilipoanza kufahamu matumizi ya mtandao na tarehe hiyo lengo hili lilitimia. Huu ni mwaka wa 5 sasa nikiwa katika tasnia hii.
Kuna wakati majukumu ya kitaaluma shuleni yanakaba sana mpaka nashindwa kuwa active kutokana na kufanya kazi hii nikiwa bado masomoni toka mwaka 2013 mpaka sasa.
Kuwepo kwa Blog hii kumesaidia baadhi ya watu kupata taarifa na habari nyingine kwa mfano zile za kielimu hasa wakati wa selection za vyuo vikuu. VENANCE BLOG imekua msaada kwa baadhi ya watu, nimekua nikiwapa taarifa za habari hizi hasa wale walio katika mazingira ya kutokua na access ya mtandao.
Pamoja na mengine mengi kama haya nimekua nikiitumia Blog hii kama platform ya kuchapisha mashairi yangu ambayo nimekua nikiyaandika kwa nyakati tofauti tofauti. Nawashukuruni sana wasomaji wangu kwa kutembelea Blog hii na kuyasoma mashairi hayo na pia kutumia muda wenu kutoa maoni kadiri inavyowapendeza. Asanteni sana.
Aidha nimekua nikiandika habari za kitaifa, kimataifa, siasa, udaku, nyimbo mpya, video mpya, habari za masuala ya anga, Teknolojia, Michezo, nimekua nikiandika pia nukuu kutoka kwa wanafalsafa wakubwa dunia na watu wengineo kama vile wanasiasa, wanamuziki, wanaharakati wa masuala tofauti tofauti n.k. Aidha nimekua nikiandika habari za mitindo na mambo mengine kadha wa kadha.
Habari, Picha, Matukio na mambo mengine ninayoyachapisha hapa nimekua nikipitia kwa ukaribu katika vyanzo makini kama vile Habari Leo, Mwananchi, BBC, DW, VoA, Jarida la Mitindo la Vogue, Forbes, Kitabu cha kumbukumbu cha rekodi za dunia Guinness, Blogs za watu binafsi, taasisi na kadhalika.
Katika mwaka huu wa 5 naahidi kuendelea kufanya kazi hii kwa ukaribu kabisa na watu, moja ya mpango wa hivi karibuni ni kuanza kuandika habari za matangazo ya kazi pamoja na kuongeza zaidi taarifa za nafasi za masomo ya nje ya nchi (scholarship) ambayo hii tayari nimeanza kuifanyia kazi. Pia kuna mengine mengi yanakuja katika Blog hii. Endelea kufuatilia VENANCE BLOG na nakushukuru sana kuendelea kuwa msomaji wa Blog hii.
Kwa maoni na mengineyo, wasiliana nami kwa moja kati ya njia hizi:
barua pepe: venancegilbert@gmail.com
Simu ya mkononi: 0753400208.
Comments
Post a Comment