WAFUNGAJI BORA NA WALIOCHEZA MECHI NYINGI KATIKA KOMBE LA DUNIA 1930-2014

WAFUNGAJI 5 WA MUDA WOTE

1. Miroslav Klose - Ujerumani

Klose wakati wa droo ya kombe la dunia mwaka jana 2017.
Amezaliwa Juni 9, 1978. Ana jumla ya magoli 16 katika michuano ya kombe la dunia na magoli 23 katika mechi za kufuzu, hii inafanya jumla ya magoli kuwa 29.  Aling'aa katika mechi ya awali kufuzu michuano hii ambapo Ujerumani iliichapa Abania 2-1 mwaka 2002. Amecheza mechi 43; 24 zikiwa za kombe la dunia na 19 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza na timu yake wameshinda mechi 30 wamesuluhu mechi 8 na kupoteza mechi 5. Ana kadi 1 ya njano katika michuano ya FIFA na kadi 2 za njano katika hatua ya makundi kufuzu kucheza kombe la dunia. Mwaka 2006 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas na mwaka 2014 alikuwepo katika kikosi cha Ujerumani walipotwaa kombe la dunia katika fainali dhidi ya Ajentina nchina Brazil.
Klose wakati wa mechi ya robo fainali kati ya Ujerumani na Ufaransa katika dimba la Marakana Rio de Jeneiro Julai 4, 2014.


2. Ronaldo de Lima - Brazil

Ronaldo de Lima alipokabidhiwa tuzo ya Hall of Fame nchini Italia mwaka 2016
Amezaliwa Septemba 22, 1976. Amecheza mechi 45; 19 za kombe la dunia, 15 za kufuzu kombe la dunia, 5 za kombe la mabara na 6 za Olimpiki. Katika mechi hizi alifunga jumla ya magoli 34; 15 ya kombe la dunia, 10 ya kufuzu michuano hii, 4 ya kombe la mabara na 5 ya Olimpiki. Akiwa katika timu ya Brazil walishinda mechi 31, suluhu 8 na kufungwa mechi 6. Umaarufu wake ulianza kuonekana katika michuano ya Olympic mwaka 1996 iliyofanyika Atlanta dhidi ya Japan. Brazil iliifunga Japan 1-0. Amewahi kupewa kadi za njano mara 4 tu katika michuano yote. Alipokuwa Brazil walitwaa kombe la dunia mwaka 1994 na 2002. Mwaka 2002 ndiye aliyekua mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia FIFA. Mwaka 1997 akiwa na timu yake walishinda kombe la dunia la mabara. Ronaldo amewahi kushinda tuzo ya mpira wa dhahabu ya Adidas kama mchezaji bora. Mwaka 2002 pia alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas. Amewahi kushinda tuzo ya Balloon d'Or ya Ufransa mwaka 1997 na 2002.
Ronaldo enzi za Brazil.


    3. Gerd Mueller - Ujerumani

    Mueller alipokua kocha wa Bayern Munich  II
    Alizaliwa Novemba 3, 1945. Amecheza mechi 19 na timu yake ya Ujerumani; 13 zikiwa za kombe la dunia na 6 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi hizo alizokuwepo walishinda mechi 16, suluhu 1 na kufungwa 2. Ana magoli 23; 14 yakiwa ya kombe la dunia la 9 yakiwa ya kufuzu michuano hiyo. Amewahi kupewa kadi za njano 2 tu katika michuano ya kombe la dunia. Mwaka 1970 alishinda tuzo mbili; kiatu cha dhahabu cha Adidas pamoja tuzo ya Ballon d'Or. Pia ni miongoni mwa waliokuwepo katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia mwaka 1974.
    Gerd Mueller mwaka 1974 waliposhinda fainali ya kombe la dunia.

    4. Just Fontaine - Ufaransa

    Fountaine mwaka 2017
    Alizaliwa Agosti 18, 1933. Yeye alicheza 8 tu 6 zikiwa zakombe la dunia na 2 zikiwa za kufuzu michuano hiyo, katika mechi hizi alifunga magoli 16; katika hayo 13 yalikua ya kombe la dunia na 3 yalikuwa ya mechi za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza 6 walishinda na hawakusuluhu ila walipoteza nchi 2 tu. Alionekana katika kombe la dunia kwenye mechi ya kati ya Ufaransa na Luxembourg ambapo waliifunga nchi hiyo 8-0 na hapo nyota yake iling'aa. Hakuwahi kupewa kadi katika mechi zote alizocheza. Mwaka 1958 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas. Katika kipindi chote alichocheza hawakuwahi kushinda ubingwa. Ufaransa illitwaa ubingwa baadaye mwaka 1998. Fontaine aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Morocco ambapo aliiongoza timu hiyo katika kufuzu kucheza kombe la dunia. Kama kocha timu yake ya Morocco ilicheza mechi 4. Mwaka 1982 Morocco ilicheza na Zambia na waliifunga 2-0.
    Fontaine mwaka 1958

    5. Pele (Edson Arantes do Nascimento) - Brazil

    Pele mwaka 2017
    Alizaliwa Oktoba 23, 1940. Alicheza mechi 20 ambapo 14 zilikuwa za kombe la dunia na 6 zikiwa za kufuzu kucheza kombe la dunia. Alifunga magoli 18 katika michuano hiyo 12 yakiwa ya kombe la dunia na 6 yakiwa katika hatua za kufuzu. Pele anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee duniani aliyeshuhudia timu yake ya Brazil ikishinda kombe la dunia mara 3 (1958, 1962, 1970) akiwepo katika kikosi cha timu hiyo mara 3 zote. Mwaka 1958 alishinda tuzo ya Hyundai ya mchezaji mdogo wakati ule akiwa na miaka 18 tu. Mwaka 2007 Pele alishinda tuzo ya heshima ya Rais wa FIFA. Katika mechi hizo 20 alizocheza, 18 walishinda, 1 walisuluhu na 1 walifungwa.
    Pele katika enzi zake kwenye soka.


    WACHEZAJI 5 WALIOCHEZA MECHI NYINGI

    1. Luthar Matthaus - Ujerumani

    Matthaus kwa sasa yupo Sky Sport.
    Amezaliwa Machi 21, 1961. Amecheza mechi 36; 25 zikiwa za kombe la dunia, 8 zikiwa za kufuzu michuano hiyo na 3 zikiwa za kombe la mabara. Umaarufu wake ulitokana na mechi ya kombe la dunia 1982 na Chile ambapo waliichapa timu hiyo 4-1. Katika mechi zote 36 alishinda 22, alisuluhu 8 na kufungwa 6. Mwaka 1990 alishinda Ballon d'Or pamoja na kuchukua ubingwa wa dunia na timu yake ya Ujerumani. Mwaka 1991 alikuwa mchezaji bora wa mwaka. Alifunga magoli 10; 6 yakiwa ya kombe la dunia, 3 yakufuzu michuano hiyo na 1 ikiwa kombe la mabara. Amewahi kupewa kadi za njano mara 9. Pia amewahi kua kocha wa timu ya Croatia, kama kocha aliifunga Hungaria magoli 3-0.
    Lothar akibusu kombe la dunia waliposhinda mwaka 1990.

    2. Miroslav Klose - Ujerumani

    Klose akiwa na wanaye baada ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Ajentina.
    Amezaliwa Juni 9, 1978. Ana jumla ya magoli 16 katika michuano ya kombe la dunia na magoli 23 katika mechi za kufuzu, hii inafanya jumla ya magoli kuwa 29. Aling'aa katika mechi ya awali kufuzu michuano hii ambapo Ujerumani iliichapa Abania 2-1 mwaka 2002. Amecheza mechi 43; 24 zikiwa za kombe la dunia na 19 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza na timu yake wameshinda mechi 30 wamesuluhu mechi 8 na kupoteza mechi 5. Ana kadi 1 ya njano katika michuano ya FIFA na kadi 2 za njano katika hatua ya makundi kufuzu kucheza kombe la dunia. Mwaka 2006 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas na mwaka 2014 alikuwepo katika kikosi cha Ujerumani walipotwaa kombe la dunia katika fainali dhidi ya Ajentina nchina Brazil.
    Klose katika kombe la dunia mwaka 2006.

    3. Paulo Maldini - Italia

    Maldin mwaka 2013.
    Alizaliwa Juni 26, 1968. Amecheza mechi 48; 23 zikiwa za kombe la dunia, 23 za kufuzu na 2 zikiwa za kombe la mabara. Alifunga magoli 3 tu katika mechi za kufuzu. Amewahi kupewa kadi za njano mara 3 tu. Katika mechi zote alizocheza 31 walishinda, 13 wakisuluhu na kupoteza 4. Mechi ya kombe la dunia mwaka 1990 wakati Italia ilipoifunga Austria 1-0 ilipelekea nyota yake kung'aa.
    Maldin mwaka 1998 katika robo fainalai ya kombe la dunia.

    4. Uwe Seeler - Ujerumani

    Seeler mwaka 2016
    Alizaliwa Novemba 5, 1936. Amecheza mechi 28; 21 zikiwa za kombe la dunia wakati 7 zikiwa za kufuzu. Amefunga magoli 23; 9 yakiwa ya kombe la dunia na 3 yakiwa ya kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza 19 walishinda, 5 walisuluhu na 4 walifungwa. Nyota ilianza kung'aa katika kombe la dunia 1958 wakati Ujerumani ilipoifunga 3- 1 Ajentina. Hakuwahi kupewa kadi.

    5. Diego Maradona - Ajentina

    Maradona.
    Alizaliwa Oktoba 30, 1960. Alicheza mechi 35; 21 zikiwa za kombe la dunia, 8 zikiwa za kufuzu kombe la dunia na 6 zikiwa za kombe la dunia chini ya miaka 20 (U-20). Maradona alifunga magoli 17; 8 yakiwa ya kombe la dunia, 3 ya kufuzu na 6 kombe la dunia U-20. Katika mechi alizocheza 23 walishinda, 6 walisuluhu na 6 walifungwa. Nyota ya Maradona iling'aa wakati wa michuano ya vijana nchini Japan mwaka 1979 wakati Ajentina ilipoifunga 5-0 Indonesia. Mwaka 1979 alishinda mpira wa dhahabu wa Adidas, FIFA U-20 pamoja na kombe hilo mwaka huo huo. Mwaka 1986 alishinda kiatu cha dhahabu pamoja na kushinda kombe la dunia. Maradona amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa lake ambapo mechi 13 zilichelezwa akiwa kocha. Alishinda mechi 8 na kufungwa 5. Umaarufu wake kama kocha ulitokana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuela mwaka 2010 ambapo waliichapa timu hiyo 4-0.
    Maradona akinyanyua kombe la dunia mwaka 1986 dhidi ya Ujerumani.


    MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA MTANDAO WA FIFA.

    Comments

    Popular Posts

    CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

    MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

    ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

    WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

    WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

    HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

    WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

    BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

    BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA