UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU TEKNOLOJIA YA 5G
Logo rasmi ya teknolojia ya mtandao wa 5G. |
Kwa teknolojia ya mtandao huu wa simu za mkononi kasi ya mtandao inatarajiwa kuwa mara 8 ya hii ya sasa mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2023 huku kukiwa na uhitaji wa teknolojia imara, viwango vikubwa vya data na wigo mpana wa matumizi ya mtandao huu tofauti na hii iliyopo sasa (4G). Vitumizi vipya kama vile 4K/8K vya kutazamia video mtandaoni moja kwa moja, uwezo wa mtandao ambao umeongezwa karibia na uhalisia pamoja matumizi ya data ambao kwa sasa yanachipukia kwa kasi, yote haya yatahitaji vipimo vikubwa vya data, uwezo wa hali ya juu, ulinzi pamoja na utulivu wa kusafirisha data katika mtandao. Haya yote ni miongoni mwa yatakayokuwa katika mtandao wa 5G. Mtandao huu utaleta fursa mpya kwa watu, jamii na biashara.
Ericsson pamoja na washirika wake wamekuwa wakifanya kazi katika teknolojia ya mtandao wa 5G kwa miaka mingi sasa katika maabara za mtandao na katika miaka 2 iliyopita waliamua kuijaribu teknolojia hii kuiweka katika matumizi. Pia, tayari wameshaingia ubia wa kusaini mikataba ya mtandao huu wa 5G kwa awamu ya kwanza ambapo mpaka kufikia sasa kampuni 39 tu duniani zimesaini mkataba wa matumizi ya teknolojia hii.
Kiwango cha teknolojia hii ya mtandao kimepelekea uwepo wa redio mpya ya mtandao wa 5G "5G New Radio" ambayo tayari imekamilika tangu Desemba mwaka jana 2017 na inatarajiwa kuanza kupatikana katikati mwa mwaka huu 2018. Mitandao ya kwanza ya kibiashara pamoja na vifaa vyenye teknolojia hii (simu, kompyuta, iPad, tablets n.k.) vya teknolojia hii vitakamilika mwakani 2019 kwa mujibu wa Mpango wa Ushirikiano wa Mtandao wa Kizazi cha tatu "3GPP" lakini yote haya yataanza kutumika kuanzia 2020. Ericsson imekadiria idadi ya watumiaji wa teknolojia hii kwamba watafika bilioni 1 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2023.
UFAHAMU NA TAARIFA KUHUSU TEKNOLOJIA HII
Mtandao huu utafanya mambo mengi sana na ndiyo sababu ukaitwa Mtandao wa Muunganiko wa Vitu (Internet of Things) utakuwa na mengi sana ya kufanya kupitia teknolojia hii. Haya ni baadhi ya mambo ambayo Ericsson inayataja kuwepo katika teknolojia hii:
ULINZI
Vifaa vilivyounganishwa pamoja na vitumizi vitahitaji kuunganishwa katika mtandao ambao ni stahimilivu, wenye ulinzi na wenye uwezo wa kulinda siri na faragha za mtumiaji. Teknolojia hii imetengenezwa kwa kuyafanikisha haya.
BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO ULIOIMARISHWA
Modem za mtandao chini ya teknolojia hii zitakuwa na nguvu zaidi ili kuimarisha biashara za wateja. Tafiti zilizofanywa na Ericsson zinaonesha kwamba mabadiliko kuelekea 5G yanaweza kupunguza karibia mara 10 ya gharama ya mtandao kwa kila gigabaiti moja tofauti na ilivyo kwa mtandao wa sasa wa 4G.
UFIKISHWAJI WA TEKNOLOJIA HII KWA NJIA YA MODEM KWANZA
Ericsson wanadai kwamba jambo la kwanza litakuwa ni kuboresha modem za sasa ili ziendane na kasi ya 5G.
MTANDAO HUU UTATEKA SOKO LA BIASHARA
Ericsson wanadai kwamba mtandao huu utakuwa wa matumizi ya vitu kwa mfano vifaa vya kujiendesha venyewe kama vile magari. Wametaja fursa, changamoto pamoja mifano ya baadhi ya mambo yanayotokea katika usasa wa viwanda.
VIWANDA VINAISUBIRIA TEKNOLOJIA HII
Je ni kwa namna gani kampuni kubwa zitaitumia teknolojia hii katika biashara zao? Ericsson imewauliza wafanya maamuzi 900 katika viwanda 10 na ripoti hiyo ipo nitaizungumzia siku nyingine.
5G KWA VIWANDA
Teknolojia hii itawawezesha wamiliki wa kampuni za simu za mikononi fursa ya kuwasaidia wamiliki wa viwanda kuwa viwanda vya kisasa na kuangalia faida za teknolojia hii kama vile utumiaji wa mitambo inayojiendesha (automation), akili bandia (artificial intelligence), ukweli thabiti (augmented reality) pamoja na mtandao wa muunganiko wa vitu (Internet of Things "IoT")
FURSA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA
Teknolojia hii itawasaidia watoa huduma za afya kwa urahisi zaidi kwa wateja wao. Hii itawezesha njia za mtandao kuwa kasi zaidi hivyo itawezesha hata kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya video bila mushkeri ya mtandao. Hii pia itawafanya watoa huduma kupanua huduma zao zaidi kuliko kusubiriana ofsini tu.
MUHTASARI KUHUSU UTAYARI WA TEKNOLOJIA HII
Ericsson wanadai kwamba utafiti mfupi uliofanywa mwaka jana 2017 unaonesha kwamba mtandao huu utakuwa na watumiaji bilioni 1 mpaka kufikia mwisho mwa mwaka 2023 kama nilivyosema hapo juu.
KUONGEZA IDADI YA WATAZAMAJI WA MPIRA
MAJARIBIO YA TEKNOLOJIA YA MTANDAO WA 5G
KOREA KUSINI
Mwezi Februari mwaka huu 2018, Ericsson, Shirika la mawasiliano la Korea Kusini na Intel walifanya majaribio ya mtandao huu katikati ya jiji la Seoul ambapo kuna idadi ya watu milioni 25. Teknolojia ya 4K video ilijaribiwa ili kutoa picha kwa watumiaji kuona uwezo wake. Matumizi ya data yalifikia 900Mbps kwa upande wa kupakua (downloading) huku yale ya kupakia (uploding) yakifikia 600Mbps. Kwa kutumia bendi 28Ghz uunganishwaji wa mtandao ulikua imara kabisa licha ya kuwepo changamoto ya uenezi wa mtandao.
ESTONIA
Telia, Ericsson na Intel walifanya majaribio ya mtandao katika kampuni ya usafirishaji ya Tallink ambayo husafirisha watu na mizigo. Kila meli hubeba hadi kufikia watu 2,000. Mafanikio bado yalionekana kwa mtandao huu. Abiria waliweza kutumia mtandao huu safarini bila kuwepo na mushkeri ya aina yoyote ile.
KASI MPYA YA 5G
KAMPUNI ZILIZOINGIA UBIA NA ERICSSON
Mpaka kufikia mwezi April mwaka huu 2018 ni kampuni 39 tu duniani ambazo zimeingia mkataba wa matumizi ya mtandao huu wa 5G kama jinsi inavyoonekana. Kwa bara la Afrika ni kampuni 2 tu za mawasiliano ambazo tayari zimesaini mkataba wa ubia na Ericsson. Kampuni hizo ni MTN ya Afrika Kusini na Etisalat ya nchini Misri. Unaweza kuziangalia nchi hizo kama jinsi kampuni zinavyoonekana kwenye ramani ya dunia akatika picha hii:
MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA MTANDAO WA ERICSSON.
Comments
Post a Comment