MORSI ACHELEWA KUWASILI MAHAKAMANI

Inasemekana kuwa hali mbaya ya anga imeizuia helikopta iliyotarajiwa kumsafirisha hadi katika mji mkuu huo anakokabiliwa pamoja na maafisa wengine wa utawala wake na tuhuma za kuchochea mauaji ya waandamanji mnamo mwaka 2012 alipokuwa madarakani.
Awali vikosi vya usalama viliimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo ,Morsi akitarajiwa kuwasili mahakamani.
Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake wanashutumiwa kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo wa kigeni kuvunja gereza.
Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa . Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni Rais na alifungwa kinyume na matakwa yake.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

BEYONCÉ FT JAY Z-DRUNK IN LOVE SONG LYRICS

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI (AWAMU YA PILI)

ABIRIA 52 WALIOKWAMA KATIKA MELI HUKO ANTAKTIKA WAOKOLEWA

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA