WATU 23 WANADAIWA KUUAWA NA WAASI WA UGANDA HUKO DRC

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda.
Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC.

Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku.

Waasi wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanyana mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni.
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu
.
ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na ndo, panga na visu.



Chanzo: BBC

MVUA ZINAZOENDELEA DAR ES SALAAM KUPUNGUA MAKALI JUMAMOSI HII

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zitaendelea kunyesha na kwamba zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii.

Taarifa hiyo inaweza kuwa habari njema kwa wakazi wa Dar es Salaam na miji mingine iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na mvua hizo zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu, huku hali ya usafiri, upatikanaji wa bidhaa hasa za vyakula ikiwa ngumu katika maeneo mengi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa  Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii wa TAM, Hellen Msemo alisema mvua hizi zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii; lakini sio kuisha kabisa na kwamba kwa sasa wananchi waendelee kufuatilia taarifa zinazotolewa.

“Mvua hizi zitaendelea kunyesha mpaka Ijumaa ya wiki hii na tunaweza kuona jua kidogo Jumamosi lakini sio mvua za kukatika kabisa zitaendelea kunyesha kidogo kidogo,” alisema Msemo.

Shule zajaa maji

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msasani ‘B’, Jane Reuben alisema mvua zinazoendelea kunyesha zimeathiri kwa kiasi kikubwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni hapo huku wengine wakichelewa kufika darasani.

Gazeti hili lilishuhudia hali tete katika shule ya Msingi Msasani ‘A’ ambapo baadhi ya madarasa yamejaa maji na kushindwa kutumika na kuwalazimu wanafunzi kuchangia vyumba vya madarasa.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wengi wanaosoma katikati ya jiji wameshindwa kufika shuleni kwa kuhofia usumbufu wa usafiri kutokana na mvua ambayo imekuwa ikiendelea kunyesha.

Baadhi ya shule katika Kata ya Goba zimefungwa kwa muda kutokana na athari za mvua hizo. Foleni zawa kero Mvua hizo pia zimeendelea kuleta usumbufu mkubwa katika barabara nyingi za Dar es Salaam kutokana na kuharibika na kusababisha msongamano unaowafanya wakazi wa jiji hilo kupata wakati mgumu wa kuyafikia maeneo mbalimbali ama kikazi au shughuli binafsi.

HabariLeo ilishuhudia maeneo ya Posta Mpya katika barabara za Samora Avenue, Mkwepu, Ocean Road, Uhuru na zile zinazoelekea Magomeni na Mwenge zikiwa na msongamano wa magari.

Bidhaa bei juu Kwa upande wa bidhaa katika masoko, bei zimepaa na kusababisha kuongezeka kwa ukali wa maisha miongoni mwa wakazi wa Dar es Salaam.

Katika soko la Kariakoo, mfanyabiashara Baraka Lisulile anayeuza karoti alisema kabla ya mvua kilo moja ilikuwa inauzwa kwa Sh 2,000 lakini sasa imefikia Sh 3,000.

“Vile vile kabla ya mvua hizi kunyesha tenga la nyanya lilikuwa ni kati ya Sh 20,000 hadi Sh 35,000 lakini hivi sasa ni kuanzia Sh 48,000 hadi Sh 50,000,” alisema mfanyabiashara huyo.

Bidhaa za unga, mchele, maharage na aina nyingine za vyakula, nazo ziko juu. Nyumba zabomoka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Musa Natty alisema mvua hizo zimefanya wananchi kukumbwa na uharibifu mkubwa ambao ni nyumba kufurika maji, kubomoka na barabara na madaraja kukatika.

Alisema katika manispaa hiyo maiti nne za wanaume na mwanamke moja zimepatikana na zimeripotiwa kata za Wazo Kunduchi na Mbezi beach.

Katika manispaa hiyo pia eneo la Africana nyumba zimejaa maji huku maeneo ya Nyaishozi kaya 151 zinahitaji msaada wa haraka ikiwemo mahema na chakula.

Alisema kata ya Tandale maeneo ya bondeni maji yameingia katika mitaa ya Pakacha, kwa Tumbo, Mahalitani, Sokoni, Mtogole na kwa Mkunduge.

Nyumba 14 ndizo zilizoathirika kwa kubomoka ambapo wakazi wake wamehifadhiwa na majirani.

Kata ya Kwembe watu 23 wamepata majeraha baada ya nyumba kuezuliwa paa, Shule ya Msingi King’azi ambayo inamilikiwa na Manispaa nayo imepata maafa ya kutitia na kutoa ufa kati ya lenta na paa.

Kata ya Mbweni familia 128 zimeathirika kwa kuzungukwa na maji na kukosa makazi na kuhifadhiwa na majirani na kata ya Magomeni mwili wa mtu mmoja umeopolewa akiwa amekufa, katika mtaa wa Suna watu 450 wamekosa makazi na mtaa wa Makuti A watu 250 hawana makazi na wanahifadhiwa na majirani.

Mtaa wa Idrisa watu 180 hawana makazi na nyumba nyingine 450 kuzingirwa na maji Kata ya Mabwepande daraja la mto Nyakasangwa mtaa wa Mbopo limekatika na kutitia hakuna mawasiliano kati ya pande mbili na barabara ya kwenda Mabwepande imekatika karibu na njia panda iendayo kwa waathirika wa Mji Mpya na nyumba 20 zimezingirwa na maji.

Kata ya Hananasif nyumba 400 ambazo ziko mabondeni zimezungukwa na maji na wakazi wa nyumba hizo wamehama makazi yao. Nyumba hizo ni zile zilizopo bondeni ambazo zilizobaki baada ya kubomolewa na wamiliki kupelekwa Mabwepande.

Kata ya Mabibo daraja la Tasaf linalounganisha Kata ya Mabibo na Makuburi limekatika kwa sababu ya wingi wa maji pamoja na nyumba tisa na vyoo.

Kata ya Manzese kumeripotiwa kifo cha mtu mmoja na kubomoka kwa nyumba moja. Daraja la linalounganisha kata ya Mbezi juu kwa Londa na Makongo kukatika.

Kata ya Wazo mtaa wa Mivumoni nyumba 13 zimeezuliwa na upepo mkali na Kata ya Kawe Mtaa wa Mzimuni nyumba 64 zimebomoka na nyingine kuzunguka na maji.

Kata ya Makumbusho mwili wa mtu mzima miaka 45 umeokotwa na waathirika 109 waliobomokewa na nyumba na zingine kujaa maji wamehifadhiwa shule ya msingi Kisiwani ambao wanahitaji msaada.

Kata ya Msasani Shule ya msingi msasani A imejaa maji katika madarasa 7 na nyumba za walimu na shule imefungwa kwa muda, Kata ya Sinza maji yamejaa yanaelekea katika makazi ya watu huku mtaa wa Barafu nyumba 3 zimebomoka na watu kukosa makazi huku nyumba 275 zimezungukwa na maji na kuhatarisha makazi.

Kata ya Mwananyamala katika mitaa ya Msisiri A na Msisiri B, Bwawani na mtaa wa Mwinyijuma jumla ya nyumba 150 zimezingirwa na maji na kuleta taabu kwa wakazi wake.

Kata ya Makuburi nyumba mbili zimebomoka na daraja la waenda kwa miguu linalounganisha Kata za Makuburi na Kimara kusombwa.

Kata ya Kimara familia saba zimehamia katika Kituo cha Polisi cha Kilungule A baada ya nyumba yao kujaa maji na kukatika, Kata ya Mizimuni nyumba tano zimevunjika kuta na kaya 15 zimehamia kwa majirani huku kaya 30 nyumba zake zimezingirwa na maji.

Kufuatia maafa hayo, Halmashauri imechukua jitihada mbalimbali ili kuokoa maisha ya watu na kuwawezesha kurudi katika makazi yao. Jitihada hizo ni pamoja ni kununua pampu za kunyonya maji ambayo yamezunguka makazi ya watu.Kazi hiyo ya kunyonya maji imeanza pamoja na kuzibua mitaro.




Chanzo: Habari Leo

IN THE NEXT - A POEM BY VENANCE GILBERT


Poem: IN THE NEXT 
Composition: December 19, 2014 
First published on the blog: December 29, 2014


The system has turned to uplift us,
From nothing to something mammoth,
Look at them brother, look them twice more,
They have our consent in authority,
Having our consent to share our sufferings,
For self into their bellies,
Look brother, feel pitty for ourselves,
The cultural similarity is credited,
Now brother tell them involved,
Go into details to them,
In the next to put their money where their mouth are,
Let them experience a miss in the next,
To re-drink the milk of human kindness.



All rights reserved.
Venance Gilbert © 2014.



IF YOU HAVE ANYTHING TO COMMENT DON'T HESITATE TO CONTACT ME THROUGH:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert
Mobile: 0753400208
Email: venancegilbert@gmail.com.



VENANCE BLOG WISHES YOU A HAPPY NEW YEAR 2015!!

KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA


Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.

Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.

Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.


KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 TANGU JANGA LA TSUNAMI MWAKA 2004


Mataifa yaliyoathirika na janga la Tsunami yameandaa ibada za kuwakumbuka watu 220,000 waliouawa wakati mawimbi makali yalipoyapiga maeneo ya pwani ya Bahari Hindi mwongo mmoja uliopita.

Mnamo Desemba 26 mwaka wa 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.3 katika upande wa magharibi wa Indonesia lilianzisha msururu wa mawimbi makali ambayo yaliupiga mwambao wa mataifa 14 ikiwa ni pamoja na Indonesia, Thailand, Sri Lanka na Somalia.

Miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha yao ni maelfu ya watalii waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Krismasi katika eneo hilo, na kulipeleka janga la maafa ya asilia ambayo hayakuwa yametarajiwa hadi majumbani kote ulimwenguni.

Maelfu ya watu wameimba wimbo wa taifa wa Indonesia kama mwanzo wa kumbukumbu ya janga hilo, kwenye ibada iliyoandaliwa Banda Aceh - mji mkuu wa mkoa ulio karibu na kitovu cha tetemeko la arshi ambalo lilisababisha mawimbi hayo makali.

Mapema leo misikiti pia iliandaa maombi kite katika mkoa huo, wakati watu wakiyatembelea makaburi ya pamoja – ya karibu Waindonesia 170,000 waliopoteza maisha yao.

Kusini mwa Thailand, ambako nusu ya watu 5,300 waliokufa walikuwa watalii wa kigeni, umati wa wageni walio likizoni walikusanyika katika uwanja wa makumbusho katika kijiji kidogo cha wavuvi cha Ban Nam Khem, katika kumbukumbu ya janga hilo kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni.

Mataifa yaliyoathirika na maafa hayo yalikabiliwa na juhudi za kutafuta msaada, wakati miili ya watu ikiendelea kutapakaa kila mahali au kujazana kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti.
Ulimwengu ulimwaga fedha nyingi na watalaamu wa huduma za misaada na ujenzi, huku zaidi ya kiasi cha dola bilioni 13.5 zikikusanywa katika miezi iliyofuata baada ya janga hilo.

Karibu msaada wa kiasi cha dola bilioni 7 ulitumika katika ujenzi mpya wa zaidi ya nyumba 140,000 kote Aceh, barabara za umbali wa maelfu ya kilomita, na shule mpya pamoja na hospitali. Maelfu ya watoto pia ni miongoni mwa waliouawa.
Lakini janga hilo pia lilimaliza mgogoro uliodumu miongo mingi wa kutaka kujitenga eneo la Aceh, huku mkataba wa amani baina ya waasi na serikali ya Jakarta ukisainiwa chini ya mwaka mmoja baadaye.

Nchini Sri Lanka, ambako watu 31,000 waliuawa, maandalizi yanafanyika ili kuandaa kumbukumbu katika eneo la barabara ya reli ambako mawimbi yalilipiga treni ya abiria, na kuwauwan watu 1,500.

Mnamo mwaka wa 2011, mfumo wa kuonya kuhusu janga la Tsunami uliundwa, wakati nchi mbalimbali za eneo hilo zikiwezeka kiasi kikubwa cha fedha katika mifumo ya kujikinga na majanga.


Chanzo: DW 


BOTI YAZAMA NA WATU 36 JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO



Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36.
Maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika.


Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye mji wa Isangi ambapo mashua hiyo ilikuwa ikielekea nyumba kadha za serikali zinaripotiwa kuchomwa.



Chanzo: BBC Swahili







WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert
Simu: +255712586027/753400208 
Email: venancegilbert@gmail.com

VENANCE BLOG INAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS 2014

VENANCE BLOG inapenda kuwatakia heri ya Christmas kwa mwaka huu 2014 tusherekee kwa amani na upendo huku tukimtanguliza Mungu katika kila jambo kwani yeye ndo muweza wa yote. Heri ya Krismas na pia Heri ya Mwaka mpya 2015!!







WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert
Simu: +255712586027/+255753400208 
Email: venancegilbert@gmail.com

VIDEO MPYA: BRACKETS-ALIVE FT DIAMOND & TIWA ICHEKI HAPA NA KUDOWNLOAD


Alive -“Hii ni hadithi ya kweli ya Vast Bracket, safari yake hadi alivyopona kansa mwaka 2013. Huu ni wimbo wa shukrani kwa kumfanya mshindi aliyeishinda kansa.”



Hayo ni maneno yanayoonekana mwanzoni mwa video ya wimbo mpya ya kundi la Bracket kutoka Nigeria iliyotoka wiki hii, ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz na Tiwa Savage.


Kipindi Vast anaumwa kansa

Memba wa kundi hilo aitwaye Vast, mwaka 2013 alikuwa akipigania uhai wake baada ya kuugua kansa ya damu ambayo baadae alifanikiwa kupona, ndio sababu ya kundi hilo kuamua kurekodi wimbo huu ‘Alive’ kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kumuwezesha msanii huyo kupona.


Vast ni yule ambaye anaimba vesre ya kwanza na kwenye video anaonekana yupo hospitali.


Video hii hapa


Vast aliwahi kuelezea jinsi alivyougua hadi kupona katika mahojiano mbalimbali aliyofanyiwa 2013:

“It all started when we went on an American tour and I started feeling feverish. I found myself taking my bath with hot water even on a very hot day. That was when I started noticing something was wrong. I noticed that whenever I drank alcohol, the fever would come in an aggressive way. I eventually went to a hospital in London. The doctor told me not to worry that everything would be fine. He said to start the treatment, they would have to do something that would allow them take something from my spine. It was a very painful procedure.”

“There was a time that I felt I would die. My only fear was that I was not close to God. I was afraid that if I died, I would not make it to heaven. We musicians have a particular lifestyle. You may plan to be upright, but when you go into entertainment business, it would change you. I was regretting that I was not close to God. I did not want to go to hell. I felt so happy that I survived,”.

“After the treatment, I did two other tests and the doctors confirmed that I was okay. After three months, I am meant to go for a PET scan. I could remember that before the treatment, we had a meeting and agreed that we had to bring £50,000. After the seventh chemotherapy session, the whole money finished. They had to send more £8,000 into the account I was using. The last time I went to withdraw money, what was left there was £120. So I used about £58,000,”

What kind of cancer did you have?

“I had Lymphoma. It is a blood cancer. When I asked the doctor what could the cancer of the blood, he said, nobody knows the cause for now. According to him, it’s like a situation where a dark complexion couple making a baby and the baby turns out to be an albino and if you are asked to explain why, you cannot tell.

I must say that when I was hospitalised, my partner was doing a good job. He would call the producer and they would make a beat and send it to me. He even made the chorus. I picked one of the songs when I came back and hit the studio. We did one of the tracks, it was fantastic. We did another song and it was good as well, all within two days.”

What have you learnt from your experience?

“I learnt that life is very precious. No matter what you do and wherever you are, don’t look down on anybody because you don’t know who will help you tomorrow. Another thing is that you don’t have to be scared of death. You have to face the challenge. Live a normal life. If you are scared of death, you will die. At a point, when I got very scared, the sickness came in full force, but when I started picking courage, it subsided and I recovered.”


KUREJESHWA KWA ADHABU YA KIFO AFGHANSTAN KWAWAPA WASIWASI AMNESTY

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametangaza kurejeshwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, kwa watakaokutwa na hatia ya ugaidi ingawa Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linapinga sheria hiyo.

Pakistan imetoa uamuzi wa kurejesha sheria ya kunyonga watakaokutwa na hatia ya ugaidi. Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif, siku moja baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Taliban na kusababisha vifo vya watu 150, wakiwemo wanafunzi 135. Mashambulizi hayo yalitokea tarehe (16.12.2014), katika shule inayomilikiwa na jeshi ilioko mjini Peshawar.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kurejeshwa kwa adhabu ya kifo, hakutaisaidia Pakistan kupambana na Ugaidi.

Azimio hilo lilipitishwa bila ya pingamizi tarehe (17.12.2014), katika mkutano uliojumuisha vyama vyote vya siasa vya nchi hiyo. Pakistan imesema kuwa kurejesha kwa sheria ya kunyonga walio na hatia ya ugaidi ni hatua muhimu, kwani katu haiwezi kuonyesha huruma yoyote kwa wale wanaohusika na matendo ya ugaidi na kuua watu wasio na hatia.

“Nimetangaza kurejeshwa kwa sheria ya adhabu ya kifo leo, na taifa zima liko pamoja na sisi,” alisema Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif.

Tangu tangazo hilo kutolewa na serikali ya Pakistan, watu wanne tayari wameshanyongwa katika jimbo la Punjab. Watu hao walikutwa na hatia za kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Rais wa zamani Jenerali Pervez Musharraf, mwaka 2003 na Jenerali wa Makao Makuu ya Jeshi la Pakistan mwaka 2009.

Hata hivyo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuanza tena kunyonga watu baada ya sheria hiyo kusimamishwa mwaka 2008 sio suluhisho ya kuzuia matatizo ya ugaidi.

“Hii ni hatua ya kijinga. Serikali inataka kuficha kushindwa kukabiliana na suala la msingi lililooneshwa na mashambulizi ya Peshawar, yaani ukosefu wa ulinzi madhubuti kwa raia wa maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Pakistan," alisema Naibu Mkurugenzi wa Amnesty International wa Asia-Pacific David Griffiths katika taarifa yake.
Aliongeza kwa kusema, adhabu ya kifo inakiuka haki za kibinaadamu. Hali hii inatupa wasiwasi mkubwa , kwani itasababisha ukiukwaji wa sheria mbalimbali za kimataifa wakiendelea kutekeleza mpango wao.

Lakini serikali kwa upande wake imejitetea kwa kusema kuwa nchi hio ipo katika wakati mgumu wa kupambana na ugaidi, hivyo hakuna njia nyengine bali kurejesha sheria ya kunyonga, huku makundi ya kidini pamoja na ya kisiasa yakikubaliana na uwamuzi huwo wa serikali.

"kunyongwa kwa magaidi wawili tarehe 19 Disemba ilikuwa ni ushindi kwa sheria ya nchi," Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf aliliambia shirika la habari la IPS, na kuongeza " Hatimaye serikali imewatendea haki magaidi."

Pakistan ina wafungwa 8000 ambao wamekuwa wakisubiri adhabu ya kifo tangu mwaka 2008. 17 kati yao walifungwa kwa mashtaka ya ugaidi, na adhabu yao ya kifo kwa kunyongwa itatekelezwa katika siku saba zijazo.

"Kutokana na hali ilivyo nchini humo, maisha ya watu wengi yapo hatarini. Serikali ya Pakistan inalazimika kufuta tena sheria ya adhabu ya kifo," alionya Griffiths wa shirika la Amnesty International.


MMAREKANI MWEUSI AWAUA ASKARI WAWILI WA MAREKANI NA BASTOLA NA KISHA KUJIUA MWENYEWE

Mtu mmoja nchini Marekani amewaua askari wawili waliokuwa kaka patrol wakiwa wamevalia nguo za kazi. Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwalenda askari hao na kuwafatulia risasi na baadae kujiua mwenyewe. 

Hii ni bastola iliyokutwa eneo la tukio.


Inasemekana kuwa mwanaume huyo aliwahi kumjeruhi mpenzi wake wa zamani kwa kumfyatulia risasi iliyomsababishia majeraha.


Áidha inasemekana pia kuwa kabla hajatenda tukio hilo aliandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe ambao si mzuri kwa polisi. Pia aliweka picha ya bastola hyo katika akaunti yake ya Instagram na kuañdika kuwa hiyo ndio itakuwa post yake ya mwisho.

Aidha mtu huyo ambaye ni Mmarekani mweusi ametajwa kwa jina la Ismaail Brinsley miaka 28 na maofisa hao kuwa ni Liu Wenjin na Raphael Ramos.

Mauàji hayo yametokea kufuatia kuwepo na mauaji ya watu weusi Marekani wanaouawa na maaskari weupe wa Marekani na kutochukuliwa hatua zozote na nchi hiyo..

Rais Obama wa Marekàni aliye katika jimbo la Hawaii kwa mapumziko ya sikukuu amelaani tukio hilo.



ChanzO: BBC NEWS




WASILIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert
Simu: 0712586027/0743400208
Email: venancegilbert@gmail.com




ICHEKI KWA MARA YA KWANZA VIDEO YA ALI KIBA - "MWANA"


Alikiba - Mwana (Official Music Video)
Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’ imeachiwa leo hii Ijumaa ya 19 Decemba 2014. 
Ali Kiba Alithibitisha kuwa video imekamilika na kusema Video imetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town.

Vituo vitakavyo rusha hii video 
Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks.

Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv.

Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTVUganda.

Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto.

Tanzania itachezwa kwenye kituo cha CloudsTV.

Hii ndio Video Halisi ya Mwana itazame.

DOWNLOAD WIMBO MPYA WA BRACKETS FT DIAMOND PLATNUMZ NA TIWA SEVAGE HAPA

Wakati Davido wa Nigeria akimponda sana Diamond Platnumz, kuwa hana fadhila, wasanii kutoka Nigeria Brackets wamakuja na ujio mpya wa Wimbo wao uitwao Alive ukiwa kama gospel fulani, wakiwa wanamshukuru Mwenyezi Mungu. Mwanadada Tiwa Savage pia amehusika humu ndani. Diamond a.k.a. Chibu Dangote kama kawaida kawakilisha kwa lugha yetu ya KISWAHILI.

 
ILI KUDOWNLOAD WIMBO HUU BONYEZA HAPA




WASILIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

UMOJA WA MATAIFA WAOMBA MSAADA KWA AJILI YA SYRIA

Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha Dola bilioni 8.4 kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura wa kibinaadamu kwa takribani watu milioni 18 wa Syria na kuzunguka ukanda huo unaokumbwa na mzozo.
Ombi hilo limetolewa jana na maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Berlin, Ujerumani kwenye mkutano wa wafadhili na wamesema msaada huo unahitajika haraka nchini Syria, na katika nchi na jamii zinazopambana kuwahifadhi wakimbizi wa Syria.
Kwa mara ya kwanza ombi hilo la Umoja wa Mataifa, linahusisha msaada wa chakula cha kuwapa nguvu na kurudisha afya, malazi, msaada mwingine wa kibinaadamu pamoja na msaada wa maendeleo.
Maafisa wa umoja huo wamesema Dola bilioni 2.9 zinahitajika ili kuwasaidia watu milioni 12.2 walioko ndani ya Syria kwa mwaka 2015, na Dola bilioni 5.5 zinahitajika kwa ajili ya Wasyria walioomba hifadhi ya ukimbizi kwenye nchi jirani na zaidi ya watu milioni moja katika jamii zinazowahudumia.
Kiasi hicho cha fedha kilichoombwa mjini Berlin, ni kikubwa zaidi ya kile kilichoombwa mjini Geneva, mwanzoni mwa mwezi huu, msaada ambao haukujumuisha fedha kwa ajili ya nchi jirani. Hata hivyo, umoja huo umeshapata nusu tu ya kiwango kilichoombwa mwaka huu 2014.
Mahitaji ya kibinaadamu yanaongezeka
Kamishna Mkuu wa Shirika linalowahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR, Antonio Gutteres ameonya kuwa wakimbizi na watu wasio na makaazi ndani ya Syria hawana akiba na nchi zinazowahifadhi ziko katika wakati mgumu, hivyo utaratibu mpya wa misaada unahitajika.
''Mahitaji ya kibinaadamu duniani yanaongezeka, na yanaongezeka kwa kasi. Na ni wazi kwamba fedha zilizopo kwa ajili ya kutimiza mahitaji hayo, haziongezeki kulingana na kukua kwa kasi ya mahitaji,'' alisema Gutteres.
Naye Mkuu wa shughuli za kibinadamu na misaada ya dharura ya Umoja wa Mataifa, Valerie Amos amesema Syria imetoka katika taifa la watu wenye kipato cha kati na kutumbukia kwenye nchi inayopambana na umaskini mkubwa. Amesema watu walioathirika na mzozo wanahitaji chakula, malazi, maji, dawa na ulinzi, lakini pia wanahitaji msaada wa kujenga upya maisha yao, kupata elimu na huduma za afya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amesema mzozo wa kibinaadamu nchini Syria na kwenye nchi jirani unatoa kitisho kwa utulivu wa ukanda wote. Amesema huo ni mwito wa mshikamano kwa mataifa yote na nchi yake iko tayari kutoa sehemu yake.
Mwezi Oktoba, Ujerumani ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria, ambapo wajumbe waliahidi kuongeza msaada wa kifedha wa muda mrefu katika nchi kama vile Lebanon na Jordan, ambazo zinakabiliana na mamilioni ya wakimbizi wa Syria wanaoingia kwa kasi kwenye nchi hizo.
Kiasi watu 200,000 wamekufa na karibu nusu ya idadi ya wakaazi wa Syria hawana makaazi kutokana na mgogoro ulioanza kwa maandamano ya kuipinga serikali ya Rais Bashar al-Assad mwaka 2011 na kugeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.




Chanzo: Deustche Welle (DW)












WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

BAISKELI YA DHAHABU YATENGENEZWA BEI YAKE INASHINDA FERARI


Kampuni ya Goldgenie iliyopo nchini Uingereza inayojihusisha na kutengezeza vitu vya kifahari, imezindua baiskeli yake mpya ya dhahabu yenye thamani ya dola 390,000 ambayo ni bei ghali hata kuliko gari jipya la Ferrari.



Gia za baikeli hiyo zimetengezwa kwa dhahabu pamoja na mikono na vyuma vyake vyote ambapo kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.



Mkurugenzi wakampuni iliyotengeza baiskeli hiyo anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo. Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkurugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara.



“Baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.” Muundo wa baiskeli hii ni wa hali ya juu,” aliongeza kusema mkurugenzi huyo.



Kwa sasa haijulikani idadi ya baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unweza kupata moja kama hio. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo ambako umeiwacha.













WASLIANA NAMI:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: venancegilbert

Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG
Source: Bongo5 via BBC

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM


Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi.



Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!!




Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj. 






WASILIANA NAMI: 
Facebook: VENANCE BLOG 
Twitter: @Venancetz 
Instagram: venancegilbert 



Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014