QUOTES OF THE DAY JUNE 5, 2014

1. Success is not final, failure is not fatal: it is the courage to continue that counts. - Winston Churchill 2. Coming together is a beginning; keeping together is progress; working together is success. - Henry Ford 3. Success consists of going from failure to failure without loss of enthusiasm. - Winston Churchill 4. In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. - Bill Cosby 5. The price of success is hard work, dedication to the job at hand, and the determination that whether we win or lose, we have applied the best of ourselves to the task at hand. - Vince Lombardi 6. Always be yourself, express yourself, have faith in yourself, do not go out and look for a successful personality and duplicate it. - Bruce Lee 7. Try not to become a man of success, but rather try to become a man of value. - Albert Einstein 8. Take up one idea. Make that one idea your life - think of it, dream of it, live on that idea. Let the brain, muscles, nerves, every part of your body, be full of that idea, and just leave every other idea alone. This is the way to success. - Swami Vivekananda 9. I've failed over and over and over again in my life and that is why I succeed. - Michael Jordan 10. I don't measure a man's success by how high he climbs but how high he bounces when he hits bottom. - George S. Patton.

MUME WA FROLA MBASHA ASEMA NI VIGUMU SANA NDOA YAO KUFIKIA MUAFAKA TENA

BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi. Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke. Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara. “Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo. TUJIUNGE NA MBASHA Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe. “Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi, Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa.” FLORA ATIMKA NYUMBANI Mbasha anaendelea: “Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo. “Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja,” alisema Emmanuel. Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa. “Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora. FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili. “Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa,” kilisema chanzo. GWAJIMA ACHOMOA Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata. “Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho,” alisema Gwajima. KWA NINI CHALI? Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu ‘Mike’ ambaye pia ni mwigizaji. Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana. “Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?” alihoji Mbasha. Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha. Canzo: GPL

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: ENGLAND YATOKA SARE NA ECUADOR 2-2

Katika mechi za kirafiki kwa maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, England ilitoka sare ya 2 - 2, dhidi ya Ecuador katika mechi iliyochezwa huko Miami.

Timu ya England iliongozwa na Frank Lampard. Raheem Sterling ambaye huchezea klabu ya Liverpool, alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United. Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki itakayofuata. 

Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda mapumziko. 

Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.

RAIS MTEULE WA MISRI KUAPISHWA JUMAPILI

Abdel Fatah al-Sisi ambaye amempinduwa kiongozi wa kwanza aliechaguliwa kwa njia ya demokrasia nchini Misri ataapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Jumapili baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais wiki iliopita. Tume ya uchaguzi hapo juzi imesema Sisi alishinda kwa asilimia 96.91 ya kura sawa na asilimia 47.5, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kumpinduwa Mohamed Mursi wa itikadi kali za Kiislamu. Ushindi wake huo mkubwa dhidi ya mpinzani pekee kiongozi wa sera za mrengo wa shoto Hamdeen Sabahi ulikuwa haukutiliwa mashaka kabisa kutokana na kupongezwa na watu wengi kwa jemedari huyo mkuu mstaafu kukomesha utawala wa mwaka mmoja wa Mursi uliowagawa wananchi miezi kumi na moja iliopita. Sisi ataapishwa saa moja na nusu asubuhi hapo Jumapili katika baraza kuu la Mahakama Kuu ya Kikatiba.Sherehe za kuapishwa kwake zitahudhuriwa na rais wa kipindi cha mpito Adly Mansour, Waziri Mkuu Ibrahim Mahlab na baraza lake la mawaziri,Imamu Mkuu Ahmed al- Tayeb wa Taasisi kuu ya Kiislamu nchini humo Al Azhar,Papa wa Kanisa la Koptik Tawadros wa Pili na viongozi wengine wa kisiasa na wa serikali. Sherehe hizo zitafuatiwa na tafrija itakayohudhuriwa na wafalme na wakuu wa nchi katika Kasri la Ittihadiya mjini Cairo. Wananchi watekeleze wajibu wao Rais wa mpito anayeondoka madarakani amesema wananchi lazima wasimame kutekeleza wajibu wao kutokana na changamoto kubwa zinazoikabili nchi hiyo ambayo imetibuliwa na ghasia za umwagaji damu, machafuko ya kisiasa na njama za kimataifa zenye kutishia utambulisho wake na heshima ya mamlaka ya dola. Katika hotuba yake ya kuaga aliyoitowa leo hii Adly Mansour mara nyengine akionekana karibu kutokwa na machozi,ameorodhesha matatizo yanayoikabili Misri wakati alipochukuwa madaraka karibu mwaka mmoja uliopita.Amesema hivi sasa nchi hiyo iko katika hali nzuri baada ya kupitishwa kwa katiba na sasa kufanyika kwa uchaguzi ambapo mkuu wa majeshi wa zamani al-Sisi ameshinda. Hotuba yake hiyo inalingana na ilani ya kampeni ya Sisi kwamba Wamisri lazima wakomeshe machafuko nchini humo na kuwezesha ujenzi mpya wa taifa hilo. Changamoto ni nzito Hapo jana Sisi alijaribu kupunguza wasi wasi ulioko nchini humo wakati aliporudia kauli mbiu ya uasi wa mwaka 2011 akiwataka wananchi wa Misri kufanya kazi kwa ajili ya kujipatia mkate,uhuru,utu wa binaadamu na haki ya kijamii. Mashrika ya haki za binaadamu ,viongozi wa kimataifa na wataalamu wameonya kwamba changamoto nzito zinamkabili Sisi wakati akiongoza nchi hiyo iliogawika vibaya. Marekani imesema inasubiri kwa hamu kushirikiana na Sisi lakini pia imeelezea wasi wasi wake juu ya mazingira ya kisiasa yenye vikwazo ambapo kwayo uchaguzi wa wiki uliopita ulifanyika. Uchaguzi huo wa Mei 26 hadi 28 ulisusiwa na kundi la Mursi la Udugu wa Kiislamu na makundi ya vijana ya vuguvugu la uasi wa umma wa mwaka 2011 kutokana na ukandamizaji wa sauti za upinzani unaoendelea nchini humo.

KESI YA UMILIKI WA NYIMBO ZA BOB MARLEY YAMALIZIKA

Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London. Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao. Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena. Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992. Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo. Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.

DICAPRIO' JACK WA TITANIC' NA PARIS HILTON WASUSIA KUONEKANA KATIKA KIPINDI CHA KIM KADARSHIAN

Muigizaji maarufu nchini Marekani, Leonard DiCaprio au maarufu kama 'Jack' aliyeigiza katika muvi ya Titanic, amekata kurekodiwa na kipindi cha Kim Kadarshian 'Keeping Up With the Kadarshians' walipokuwa katika pati ya majira ya joto Jumapil mchana. "Leo hakutaka kurekodiwa kwa ajili ya kipindi cha Kim na hakuwasili mpaka pale shughuli za kurekodi zilipokwisha" alisema mpasha habari mmoja. Pia, Paris Hilton ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Kim, naye hakupenda kuonekana katika kipindi hicho ambaye naye ameanzisha fani yake kama DJ.

KOCHA NOOIJ ASEMA HATOPANGUA KIKOSI CHA TAIFA STARS

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’, Mholanzi Mart Nooij amesema kamwe hatakifanyia marekebisho kikosi chake kilichotinga raundi ya pili ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa Afrika kwa kuifunga Zimbabwe jumla ya mabao 3-2. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salam, Stars ilipata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji wao Zimbabwe Jumapili iliyopita Jijini Harare na kukata tiketi ya kucheza raundi hiyo ya pili na sasa itakutana na Msumbiji Julai 18. Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Harare juzi usiku, kocha huyo alisema: “Mechi na Zimbabwe ilikuwa nzuri na ngumu kwetu, lakini nawapongeza vijana wangu walicheza kwa kujituma na kupata matokeo ambayo yametupeleka hatua nyingine, tuna muda mrefu kabla ya kucheza mechi inayofuata nitatumia muda huu kukirekebisha kikosi changu lakini siwezi kukibadilisha,” alisema Nooij. Akiuzungumzia mchezo wao unaofuata dhidi ya Msumbiji aliyowahi kuifundisha siku za nyuma, Nooij alisema ni timu ngumu yenye wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya na Afrika, lakini anayajua vyema mapungufu yao na atayatumia ili kuweza kuiondosha kwenye kinyang’anyiro hicho kama ilivyokuwa kwa Zimbabwe. “Hakuna asiyejua kama Msumbiji ni timu nzuri ina wachezaji wengi wenye uzoefu kutokana na kucheza soka Ulaya na wengine kwenye klabu kubwa Afrika, lakini hilo halinipi wasiwasi kwa sababu nawajua vyema wapinzani wetu na Watanzania watarajia kupata matokeo mazuri,” alisema Nooij. Nooij alisema kitu kikubwa ambacho angependa kulishauri Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ni kuiandaa timu mapema, ikiwa ni pamoja na kupata mechi za kirafiki za kimataifa ambazo zitawasaidia kujua mapungufu na uwezo waliokuwa nao kabla ya kuwavaa Msumbiji. “Itafurahisha kuanza maandalizi mapema kwa sababu tutapumzika muda mrefu na kwa vile hakuna ligi kwa sasa, lengo ni kutaka kujifunza zaidi uwanjani na kupata mechi za majaribio ambazo zitarudisha ari ya vijana wangu kabla ya kumenyana na Msumbiji,” alisema Nooij. Nooij, kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika, alianza kuifundisha Stars miezi mitatu iliyopita akichukua nafasi ya Kim Poulsen, siku za nyuma kuanzia mwaka 2007 hadi Septemba 2011 alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Msumbiji na kuiongoza kwenye michuano ya Mataifa Afrika yaliyofanyika Angola na timu hiyo kumaliza ya mwisho kwenye kundi lake baada ya kufungwa michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: BLATTER AWASILI BRAZIL NA KUKUTANA NA RAIS WA NCHI HIYO, DILMA ROUSSEFF

Rais wa FIFA, Joseph S. Blatter amekutana na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff huko Palacio do Planalto, Brasilia. Kwa msisimko wa kihistoria wa kombe hilo ambalo litatolewa kwa bibngwa wa dunia, kombe hilo limetolewa na Blatter na Cafu aliyekuwa nahodha wakati Brazil ilipotwaa kombe hilo mwaka 2002. 

"Nilishasema kabla ya kuja Brazil, kwa mara ya kwanza itakuwa ni kuonana na Rais wa nchi hii. Hii yote ni kwa heshima na taadhima" alisema Blatter kabla ya kuanza kwa sherehe ambapo Rais Rousseff aliinua juu kombe la dunia ambalo huguswa na Marais na mabingwa pekee.

"Ni matumaini yangu na Wabrazil wenzangu zaidi ya milion 200, wanategemea hapo tarehe 13 Julai zaidi ya watu 23 wataweza kuligusa kombe hili" alisema Rousseff.Siku 10 kabla ya michuano kuanza.

Rais Dilma alishaitisha mkutano huko Brazil na wakuu wa majimbo kujadili juu ya mechi ya maandalizi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia huko Palacio do Planato katika dimba la Arena de Sao Paulo. Baada ya sherehe za ufunguzi Blatter na Rais Dilma walihudhuria mkutano na waandishi wa habari ambapo pia alikuwepo Waziri wa Michezo wa Brazil, Aldo Rebelo. 

Mwishoni mwa mwezi Januari Rais Blatter aliwkaribisha wakuu wa majimbo ya Brazil makao makuu ya FIFA huko Zurich."Ni matumaini yangu kwa zadi ya mwezi mmoja macho yote yataelekezwa Brazil katika kombe la dunia" alisema Blatter

QUOTES OF THE DAY JUNE 1, 2014

Education is what survives when what has been learned has been forgotten. - B. F. Skinner Love Quote of the Day: I love you the more in that I believe you had liked me for my own sake and for nothing else. -John Keats Art Quote of the Day: Every child is an artist. The problem is how to remain an artist once we grow up. -Pablo Picasso Nature Quote of the Day: If the skies fall, one may hope to catch larks. -Francois Rabelais Funny Quote of the Day: Only two things are infinite, the universe and human stupidity, and I'm not sure about the former. -Albert Einstein

ASILILIA 25 YA WALIMU HUFUNDISHA MAMBO YASIYO YA MSINGI

Wakati Serikali ikiahidi kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha, imebainika kuwa asilimia 25 ya walimu huwafundisha wanafunzi mambo yasiyo ya msingi. Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), iliyozinduliwa Dar es Salaam hivi karibuni, imebainisha kuwa wakati wananchi wakilalamika kuwa elimu inayotolewa haimsaidii mwanafunzi kupata ajira nzuri, wanafunzi hawajifunzi mambo ya msingi yatakayowasaidia kupambana na changamoto za maisha. Akizindua ripoti hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa ripoti hiyo imeweka wazi ukubwa wa tatizo la ufundishaji, akieleza kwamba jumla ya watoto milioni 250, duniani wanakosa mafunzo ya msingi ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ingawa wanaingia darasani. “Tanzania kama sehemu ya dunia, haijakwepa tatizo hilo. Baadhi ya watoto wetu wamekuwa wakimaliza shule za misingi bila ya kuwa na ujuzi huo. Hii ni hali ya kushtua, inayohitaji nguvu za pamoja za wadau wote wa elimu duniani,” alisema Kawambwa. Alibainisha kwamba ripoti hiyo imependekeza mpango wa elimu mwaka 2015, uzingatie ubora utakaotokana na mipango sahihi inayotekelezeka akitaka tatizo la walimu lipatiwe ufumbuzi wa kudumu kwa lazima ili kuwanusuru wanafunzi. “Kama suala la walimu halitapatiwa ufumbuzi sasa, tofauti kwenye ufundishaji itakuwepo kwa vizazi vingi huku ikitoa tafsiri mbaya dhidi ya jitihada za kuondoa umaskini duniani na kufikiwa kwa maendeleo endelevu,” alisema Dk Kawambwa. Aliongeza kuwa kwa namna hali ilivyo sasa, Serikali inalazimika kuhakikisha inaajiri walimu wenye dhamira ya kweli ya kufundisha na kutoa elimu bora. Ripoti ya Unesco inaeleza kuwa licha ya kuwepo kwa mafanikio ya kuridhisha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, wananchi masikini ndiyo walioathirika zaidi na tatizo la utoaji elimu mbaya sababu ikiwa kutokuwepo kwa walimu wenye mafunzo ya kutosha. Unesco ilisema kuwa kutokana na matatizo ya walimu, wanafunzi 130 milioni wanaosoma shule za msingi duniani, hawana uwezo wa kusoma hata sentensi moja, jambo linalowafanya washindwe kujiunga na sekondari. “Matatizo ya elimu siyo tu yanaathiri malengo ya watoto ya baadaye, lakini pia uchumi wa Serikali hizo. Gharama ya watoto 250 milioni kutosoma elimu ya msingi ni Dola 129 bilioni za Marekani,(Sh 212.85 bilioni), ambayo ni asilimia kumi ya matumizi ya dunia katika elimu,” inasema ripoti hiyo. Ripoti hiyo imelinukuu shirikali lisilo la Serikali la Uwezo, linaloeleza kuwa asilimia 26 ya wanafunzi wa darasa la tatu ndiyo wanaoweza kusoma vizuri hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili.

JUSTIN BIEBER HATORUDISHWA CANADA

Sorry, America — we’ll have to deal with Justin Bieber a bit longer. The White House on Friday finally officially responded to a petition signed by more than 273,000 people to have Bieber deported to Canada after a string of boozy antics and arrests. “Sorry to disappoint, but we won’t be commenting on this one,” read a statement on petitions.whitehouse.gov. “We’ll leave it to others to comment on Mr. Bieber’s case, but we’re glad you care about immigration issues.” The White House argued immigration reform will shrink our deficits by almost $1 trillion in the next 20 years. Handily, it added, “For those of you counting at home, that’s 12.5 billion concert tickets — or 100 billion copies of Mr. Bieber’s debut album.”

MRISHO MPOTO AELEZEA SABABU ZA KUTOVAA VIATU HATA ANAPOKUWA KATIKA ZIARANI KIMATAIFA

Msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto amedai kuwa ajisikii vizuri pindi anapo vaa viatu kutokana kudai kuvaa viatu kuna athiri utendaji wa kazi zake. Mpoto alilionga na bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika. “Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika nakuwa na amani”Alisema Mpoto Mrisho anaendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu “Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa Thiong’o alisema huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka mimi ninapoigia kwenye technolojia siwezi badilishwa kwasababu nimeshajijua mimi ni nani”Alimalizia Mpoto

UGOMVI KATI YA PETER NA PAUL 'P SQUARE' KAKA YAO NA MKE WA PETER WAHUSISHWA

Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri. Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana. Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao. Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao. Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao. “After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.”ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache. After over 10yrs of hard work, it's over. Am done. — IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014 Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri. Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya. Source: Bongo5

NUKUU ZA LEO/QUOTES OF THE DAY 19/04/2014

1. Let us dream of tomorrow where we can truly love from the soul, and know love as the ultimate truth at the heart of all creation. - Michael Jackson

2. Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant. -Robert Louis Stevenson

3. Find a place inside where there's joy, and the joy will burn out the pain. -Joseph Campbell

4. Health is the greatest gift, contentment the greatest wealth, faithfulness the best relationship. - Buddha

5. Even if I knew that tomorrow the world would go to pieces, I would still plant my apple tree. -Martin Luther

 6. Hope is a waking dream. - Aristotle

 7. Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present. - Jim Rohn

 8. I hated every minute of training, but I said, 'Don't quit. Suffer now and live the rest of your life as a champion.' -Muhammad Ali

9. Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared. -Buddha

10. Your present circumstances don't determine where you can go; they merely determine where you start. Nido Qubein

 11. If you accept the expectations of others, especially negative ones, then you never will change the outcome. - Michael Jordan

12. We can't help everyone, but everyone can help someone. -Ronald Reagan

13. Put your heart, mind, and soul into even your smallest acts. This is the secret of success. - Swami Sivananda

14. Start where you are. Use what you have. Do what you can. -Arthur Ashe

15. You must do the things you think you cannot do. -Eleanor Roosevelt

16. Don't limit yourself. Many people limit themselves to what they think they can do. You can go as far as your mind lets you. What you believe, remember, you can achieve. - Mary Kay Ash

17. You are always free to change your mind and choose a different future, or a different past. - Richard Bach

18. It is in your moments of decision that your destiny is shaped. - Tony Robbins

19. In oneself lies the whole world and if you know how to look and learn, the door is there and the key is in your hand. Nobody on earth can give you either the key or the door to open, except yourself. - Jiddu Krishnamurti

20. It is during our darkest moments that we must focus to see the light. -Aristotle Onassis

WAKOREA KASKAZINI WAAGIZWA KUNYOA KIDUKU

Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao. Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un. Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa. Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo. Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.