ASILILIA 25 YA WALIMU HUFUNDISHA MAMBO YASIYO YA MSINGI

Wakati Serikali ikiahidi kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha, imebainika kuwa asilimia 25 ya walimu huwafundisha wanafunzi mambo yasiyo ya msingi. Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), iliyozinduliwa Dar es Salaam hivi karibuni, imebainisha kuwa wakati wananchi wakilalamika kuwa elimu inayotolewa haimsaidii mwanafunzi kupata ajira nzuri, wanafunzi hawajifunzi mambo ya msingi yatakayowasaidia kupambana na changamoto za maisha. Akizindua ripoti hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa ripoti hiyo imeweka wazi ukubwa wa tatizo la ufundishaji, akieleza kwamba jumla ya watoto milioni 250, duniani wanakosa mafunzo ya msingi ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ingawa wanaingia darasani. “Tanzania kama sehemu ya dunia, haijakwepa tatizo hilo. Baadhi ya watoto wetu wamekuwa wakimaliza shule za misingi bila ya kuwa na ujuzi huo. Hii ni hali ya kushtua, inayohitaji nguvu za pamoja za wadau wote wa elimu duniani,” alisema Kawambwa. Alibainisha kwamba ripoti hiyo imependekeza mpango wa elimu mwaka 2015, uzingatie ubora utakaotokana na mipango sahihi inayotekelezeka akitaka tatizo la walimu lipatiwe ufumbuzi wa kudumu kwa lazima ili kuwanusuru wanafunzi. “Kama suala la walimu halitapatiwa ufumbuzi sasa, tofauti kwenye ufundishaji itakuwepo kwa vizazi vingi huku ikitoa tafsiri mbaya dhidi ya jitihada za kuondoa umaskini duniani na kufikiwa kwa maendeleo endelevu,” alisema Dk Kawambwa. Aliongeza kuwa kwa namna hali ilivyo sasa, Serikali inalazimika kuhakikisha inaajiri walimu wenye dhamira ya kweli ya kufundisha na kutoa elimu bora. Ripoti ya Unesco inaeleza kuwa licha ya kuwepo kwa mafanikio ya kuridhisha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, wananchi masikini ndiyo walioathirika zaidi na tatizo la utoaji elimu mbaya sababu ikiwa kutokuwepo kwa walimu wenye mafunzo ya kutosha. Unesco ilisema kuwa kutokana na matatizo ya walimu, wanafunzi 130 milioni wanaosoma shule za msingi duniani, hawana uwezo wa kusoma hata sentensi moja, jambo linalowafanya washindwe kujiunga na sekondari. “Matatizo ya elimu siyo tu yanaathiri malengo ya watoto ya baadaye, lakini pia uchumi wa Serikali hizo. Gharama ya watoto 250 milioni kutosoma elimu ya msingi ni Dola 129 bilioni za Marekani,(Sh 212.85 bilioni), ambayo ni asilimia kumi ya matumizi ya dunia katika elimu,” inasema ripoti hiyo. Ripoti hiyo imelinukuu shirikali lisilo la Serikali la Uwezo, linaloeleza kuwa asilimia 26 ya wanafunzi wa darasa la tatu ndiyo wanaoweza kusoma vizuri hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU