FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA

tanzania flagLeo nakufahamisha baadhi ya mambo ambayo huenda hukuyafahamu ama ulichukulia kawaida tu. Mambo hayo ni hapahapa Tanzania.  Tanzania ina eneo la kilomita za mraba 945,087. Ina jumla mikoa 31 kote bara na visiwani. Mpaka kufikia mwaka 2017 idadi ya watu nchini ilikadiriwa kuwa milioni 52.554 kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya takwimu. Twende sasa tuanze kuhesabu moja baada ya jingine


#1. Wimbo wa taifa "Mungu Ibariki Tanzania" ni wimbo unaofanana na nyimbo za mataifa ya Afrika Kusini na Zambia. Wimbo huu ulitungwa na Enock Sontonga kwa lugha ya Xhosa "Nkosi Sikelel iAfrika". Wimbo huu pia uliwahi kutumiwa na nchi za Zimbabwe na Namibia.
Image result for enoch sontonga
Enock Sontonga mtunzi wa wimbo Mungu Ibariki Afrika


#2. Ni Tanzania pakee ambako kunapatikana Simba wenye uwezo wa kupanda juu ya miti. Simba hawa wanapatikana katika hifadhi ya taifa ya Ziwa Manyara.
bwindi-and-serengeti-safari_18889423181_o
Simba wenye uwezo wa kupanda miti hifadhi ya Ziwa Manyara.


#3. Tanzania ni nchi ambako fuvu la mtu wa kale zaidi liligunguliwa. Fuvu hili liligunguliwa katika bonde la Olduvai mwaka 1959 na Dr. Louis Leakey.
Olduvai Gorge


#4. Tanzania in Mlima Kilimanjaro ambao ni Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huu una urefu wa mita 5895.
Related image



#5. Pamoja na kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa, Tanzania inayo makabila 120 ambayo yana mila, desturi na tamaduni tofauti tofauti. Makabila haya yanaishi vyema na kuelewana chini ya mwamvuli wa Utanzania na lugha ya taifa ya Kiswahili.
Related image
Ramani ya Tanzania ikionesha Makabila

#6. Uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo ni ziwa lenye kina kirefu kuliko yote barani Afrika. Ziwa hili lina kina cha futi 4823 ambazo ni sawa na mita 1470. Ziwa hili pia lipo katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na Zambia. Ziwa hili pia ni la pili duniani kwa kuwa na kina kirefu zaidi baada ya ziwa Baikal likifuatiwa na Caspian.
Related image
Ziwa Tanganyika

#7. Tanzania ina zaidi ya wanyama pori milioni 4 ambao wamegawanyia katika makundi 430 tofauti ya wanyama.



#8. Hifadhi ya taifa ya Serengeti ni hifadhi maarufu kwa kuwa na mimea na wanyama wa aina tofauti tofauti. Pia ni mbuga inayoongoza kwa kuwa na makundi makubwa ya wanyama wanaohama kila mwaka kundi kubwa likiwa ni kundi la nyumbu. Mwaka 1981 hifadhi hii ilitajwa na UNESCO kama sehemu ya urithi wa kujivunia duniani.
Image result for ngorongoro
Hifadhi ya Serengeti.


#9. Tanznaia ina hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambayo ni maarufu kwa kuwa na ziwa ambalo limetokana na mlipuko wa Volkano; Ziwa Magadi ziwa hili lina kilomita za mraba 264 na maarufu kwa kuwa na ndege wengi aina ya flamingo. Eneo hili la Ngorongoro lina aina mbalimbali za wanyama kama vile tembo, faru, kiboko, pundamilia, nyati n.k. Katika eneo hili jamii ya Wamasai hufanya shughuli zao za ufugaji. Hifadhi hii ilitajwa kama eneo la urithi wa kujivunia wa dunia mwaka 1979.
ngorongoro conservation area
Hifadhi ya Ngorongoro

Ngorongoro-Crater
Ziwa Magadi linalopatikana hifadhi ya Ngorongoro


#10. Tanzania ina mji eneo maarufu kwa kivutio cha utalii ambacho huitwa mji mongwe. Eneo hili lipo Unguja-Zanzibar. Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya “Urithi wa Dunia” (World Heritage). Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
Image result for mji mkongwe wa zanzibar
Mji Mkongwe uliojengwa tokea enzi za utawala wa Waarabu wa Omani

#11. Uwepo wa daraja la Nyerere linalounganisha wilaya ya Kigamboni kupitia Kurasini. Ujenzi wa daraja hili ulianza Februari 2012 na kukamilika April 2016. Daraja hili lina urefu wa mita 680.
Image result for kigamboni bridge
Daraja la Nyerere linalounganisha wilaya ya Kigamboni na kata ya Kurasini kupitia mkondo bahari wa Kurasini


#12. Ziwa kubwa kulio yote Afrika na Ziwa la tatu kwa ukubwa duniani; Ziwa Victoria lipo Tanzania kwa kiasi kikubwa likipakana na nchi za Uganda na Kenya. Ziwa hili lina ukubwa wa eneo la mraba 68,870 likiwa na urefu wa kilomita 332 na kina cha mita 84 sawa na futi 276.
Related image
Ziwa Victoria

#13. Pengine kuna hili hukulifahamu. Tanzania ina majiji 6 kwa sasa Dar es Salaam likiwa ni jiji kubwa kuliko yote, likifuatia jiji la Mwanza, Arusha na majiji ya Mbeya, Tanga na jiji pipya la Dodoma ambalo limepata hadhi ya jiji April 26, 2018 siku ya kumbukumbu ya maandhimisho Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 19964.
Ramani ya Tanzania ikionesha mikoa yake (mikoa michache haijaoneshwa katika ramani hii)


#14. Kuna fukwe (beach) nzuri na za kuvutia pindi unapohitaji sehemu ya kupunga upepo baharini. Coco beach, Landmark, Ocean view, Lamada, Nungwi, Sea cliff, Zanzi Resort, Tanga beach, Mbezi beach, Malaika Beach Resort n.k. ni baadhi ya fukwe maarufu nchini
tanzania beach



#15. Tanzania inapakana na nchi 8 ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia na Msumbiji.
Image result for tanzania map with lakes



#16. Tanzania ilisaidia nchi nyingi za Kusini mwa Afrika kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni; nchi hizo ni Jamhuri za Afrika ya Kusini, Angola, Namibia, Msumbiji na Zimbabwe. Mwalimu Nyerere aliwasaidia wapigani uhuru wa vyama vya ANC, MPLA, SWAPO, FRELIMO na ZANU. 
Related image


#17. Tanzania ina kisiwa kikubwa katika visiwa vyote vilivyo ndani ya maziwa ya bara la Afrika; Kisiwa cha Ukerewe ambacho kina eneo la kilomita za mraba 530. Kisiwa hiki kinapatikana ndani ya Ziwa Victoria. Huenda hukuifahamu hii, basi nimekufahamisha.
Image result for ukerewe map
Kisiwa cha Ukerewe kama jinsi ramani inavyoonekana kwa juu.
Image result for ukerewe map
Kisiwa cha Ukerewe (rangi nyekundu)
#18. Tanzania kuna mawe ambayo ni kuvutio kikubwa cha utalii nchini. Mawe haya yamebebana bila kudondoka kwa miaka mingi sasa. Ni maarufu kama Bismarck rock. Yapo jijini Mwanza na yamewekwa katika noti ya Tsh. 1,000/=
Image result for bismarck rock
Mawe ya Bismarck ambayo ni maarufu sana nchini

#19. Uwepo wa banadari ya Dar es Salaam ambayo inakuza uchumi na pato la taifa kwa kuingiza na kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi. Bandari hii inasaidia pia nchi za Congo DR, Rwanda, Zambia, Burundi na Malawi.
An aerial view of a section of the port. Credit: Tanzania Ports Authority
Picha ya Bandari ya Dar es Salaam kama ilivyopigwa kutoka juu.

#20. Tanzania ina maeneno 7 ambayo yalitangazwa kuwa ni maeneo ya urithi wa kujivunia duniani. Maamuzi hayo yalitajwa kwa nyakati miaka tofauti na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO). Maeneo hayo ni haya yafuatavyo:
  • Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
  • Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro
  • Mlima Kilimanjaro
  • Magofu ya kale ya Kilwa na Songa Mnara
  • Michoro ya Mapangoni ya Kondoa
  • Hifadhi ya Wanyama ya Selous
  • Mji Mkongwe Unguja.


Picha zote kwa msaada wa mtandao. Picha hizi si miliki ya blogu hii, kila picha ina mmliki wake.
Unaweza kuacha maoni yako chini ya chapisho hili ama kutuma barua pepe kupitia venancegilbert@gmail.com kama una lolote la kusema ama kuwasiliana nami kwa WhatsApp namba +255712586027 ama kunipigia kwa namba +255753400208.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER

BAISKELI YA DHAHABU YATENGENEZWA BEI YAKE INASHINDA FERARI