Venance Blog:
Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa mamlakani rais aliyechaguliwa naraia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi.
Viongozi duniani wamepokea kwa tahadhari matukio yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amewaambia waandishi kwambaanaangalia kwa umakini hatua iliyochukuliwa na jeshi la Misri.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza , William Hague, amesema Uingereza haiungi mkono uvamizi huo wa kijeshi lakini haina budi kuitambua hatua hiyo na kusogea mbele. Hata hivyo alikataa kulishutumu jeshi kwa kumpindua Morsi akisema ni uvamizi ulioungwa mkono na watu wengi.
Mfalme Abdalla wa Saudia ametuma ujumbe wa hongera kwa kaimu rais wa Misri akisema kwamba uteuzi wake unajiri katika wakati muhimu.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjiniCairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
IDADI YA WATU WALIOFARIKI UGANDA YAFIKIA 33
Moto mkubwa uliowaka baada yaajali mbaya ya barabarani iliohusisha lori la mafuta, umewauwa takriban watu 33 mjini kampala Uganda.
Watu wengine 30 wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia tukiohilo.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa kati ya waliofariki ni raia waliokuwa wanakimbilia eneo hilo la mkasa kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka kwa lori hilo.
maafisa wa serikali walikuwa katika harakati za kutambua mili ya waliofariki baada ya wengi wao kuchomeka vibaya.
Idara ya polisi imesema kuwa waliofariki waliteketea kiasi cha kutotambulika na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua miili ya waliokufa.
RAIS OBAMA AWASIRI TANZANIA
Rais wa Marekani Mh. Barack Obama amewasili leo hii nchini katika uwanja wa kimataifa Mwalimu Nyerere majira ya saa 8 akitokea katika nchi ya Afrika Kusini.
Rais Obama amewasiri yeye pamoja na familia yake huku akiambatana na msafara wa watu 700 kutoka Marekani wakiwemo Wafanyabiashara na Waandishi wa habari.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
KIONGOZI WA AL SHABAAB AJISALIMISHA
Mmoja wa viongozi wakuu wa zamani wa kundi la wapiganaji wa Al-shabaab, Hassa Dahir Aweyes amewasili mjini Mogadishu chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya serikali.
Hata hivyo haijulikani iwapo kiongozi huyo amesalimu amri auameamua kujiunga na vikosi hivyo vya serikali.
Ijumaa iliopita, umoja wa mataifaulitangaza kuwa Bwana Hassa Dahir alikuwa amejisalimisha kwavikosi vya serikali ya Somali lakinimadai hayo yakapingwa na wazee wa koo za taifa hilo.
Kiongozi huyo alikuwa amechukua hifadhi katika mji wa Kazkazini wa Adado baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya kambi tofauti za wapiganaji wa Al Shabaab juma lililopita.
Kiongozi huyo ametajwa kama gaidi na umoja wa mataifa pamoja na serikali ya marekani.
©2013 Venance
MAANDAMANO DHIDI YA RAIS MORSI WA MISRI YAANZA
Raia wa Misri wamefanya maandamano makubwa kote nchini kumshinikiza rais wa taifa hilo Mohammed Morsi, kujiuzulu wakati wa maadhimisho yake ya kwanza tangu achukue hatamu ya taifa hilo.
Ijapokuwa barabara za mji wa Cairo zina utulivu kufikia sasa, maafisa wa polisi wamewekwa katika kila sehemu ili kuzuia ghasia.
Wapinzani wa rais huyo wanamkashifu kwa kushindwa kutatua maswala ya kimsingi kama vile uchumi pamoja na usalama na kudai kuwa zaidi ya raia millioni 22 wametia sahihi yakutaka uchaguzi mpya kufanyika mara moja.
Aidha wanadai kuwa rais Morsi, ameweka ajenda ya Kiislamu ya chama chake cha Muslim brotherhood mbele kushinda mahitaji ya raia wa taifa hilo.
Wafuasi wa rais huyo pia wameapa kufanya mikutano ya hadhara kumuunga mkono kiongozi wao
©2013 Venance
RAIA WA AFRIKA KUSINI WAKESHA WAKIMUOMBEA RAIS NELSON MANDELA
Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabariwanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safariyake ya Msumbiji ili kumtembeleaMandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.
ZIARA YA RAIS OBAMA KATIKA NCHI TATU ZA AFRIKA YAANZA
Rais wa Marekani, Mh. Barack Obama ,jana ameanza ziara yake katika ule mpango wake wa kuzitembelea nchi za bara la Afrika. Nchi zilizopata fursa ya kutembelewa na kiongozi huyo kutoka taifa kubwa ulimwenguni ni 1. Tanzania 2. Senegal 3. Afrika Kusini Katika kuitembelea nchi ya Afrika Kusini ilikuwa Rais Obama aonane na Rais wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Mandela ambaye yuko hospitali kwa siku ya 20 lakini sasa atafanya hivyo endapo ataruhusiwa na familia ya Nelson Mandela. Akiwa nchini humu rais Obama atapokelewa na mwenyeji wake Rais Kikwete.
Copyright © 2013
SOMA HAPA JINSI YA KUWEKA USALAMA WA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK
KWA USALAMA WA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK NENDA SEHEMU YA CHINI INAITWA "SETTINGS & PRIVACY" KISHA BOFYA "SECURITY" CHAGUA "SECURITY QUESTION" THEN USOME MASWALI YATAKAYOONESHWA HAPO CHINI CHAGUA SWALI AMBALO UNAONA NI RAHISI KWAKO KISHA LICHAGUESWALI HILO KWA KULIBONYEZA NA KISHA TOA JIBU LA SWALI HILOKWA USAHIHI KISHA WEKA NAMBAZAKO ZA SIRI ZA FACEBOOK (PASSWORD) KISHA HIFADHI (SAVE) KUMBUKA USIMWAMBIE MTU YEYOTE SWALI HILI KWA SABABU LINATUMIKA KURUDISHA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK PINDI UNAPOZUIWA (BLOCKED) AUKUBADILISHWA BAADHI YA TAARIFA (HACKING) HAYA SASA FUATA MLOLONGO HUU KWENYE AKAUNTI YAKO:
"SETTINGS & PRIVACY >SECURITY >SECURITY QUESTION"
Asante!!!
© 2013 Venance
© 2013 Venance
SOMA KISA CHA KIPOFU HAPA (NI BURUDANI TU HAKUNA UKWELI)
Kipofu alimpiga mtu mmoja hadi akamuua.
Akapelekwa mahakamani, Hakimu akamuuliza kwa nini umeua na wakati huoni?
Kipofu akajibu, marehemu aliniambia mwenyewe nipige uone, kwa vile mi nilikuwa na hamu kubwa ya kuona nikampiga kwa nguvu zangu zote bahati mbaya akafariki!!... Hakimu akaduwaa!!!
"KWA MUJIBU WA MAELEZO YA KIPOFU, KAMA WE UNGEKUWA HAKIMU UNGEAMUA NINI HAPO???!!"
Udaku Specially: SHOW YA MWANA FA AMEAMBULIA PATUPU.... WAJITOKEZA ...
Udaku Specially: SHOW YA MWANA FA AMEAMBULIA PATUPU.... WAJITOKEZA ...: Nilikua narudi mjini nikitokea Kigamboni kupumzisha akili. Sasa nikapita pale opposite na iFM kucheki kama Mwana FA kala shavu. FA katia ...
Venance Blog
Venance Blog
AFARIKI URAMBO TABORA KWA KUNYWA VIROBA 12 VYA KONYAGI KATIKA MASHINDANO
Tukio hilo lilitokea juzi tarehe 12 Juni 2013 katika wilaya ya Urambo mkoani Tabora akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Kaimu Kamanda, Edward Lukombe amemtaja marehemu kuwa ni Juvenali Wambura mwenye umri wa miaka 42, inadaiwa kuwa siku ya tukio baadhi ya wanywaji katika glosari moja waliandaa shindano ambalo si rasmi kuwa mnywaji atakayekunywa viroba 12 ataondoka na zawadi ya pesa taslimu ambapo inadaiwa marehemu alijigamba kuwa angekunywa viroba vyote na hivyo kuibuka mshindi inadaiwa kuwa marehemu alianza kunywa viroba hivyo kwa kasi ya ajabu ambapo alipomaliza kunywa kiroba cha mwisho cha 12 aliishiwa nguvu na hivyo wenzake kulazimika kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya urambo kwa matibabu lakini bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi.
Kaimu kamanda huyo amesema kuwa licha ya marehemu kunywa viroba vyote hivyo inaelekea hakuwa amepata lishe ya kutosha siku hiyo.
Kaimu kamanda huyo ametahadharisha wanywaji mkoani humo kunywa kwa wastani na kuwa wamekula na sio kunywa kwa mashindano ili kuepuka madhara kama hayo.
Venance ©Juni, 2013
MISHE MISHE ZA MWAFRIKA: BREAKING NEWS; MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AL...
MISHE MISHE ZA MWAFRIKA: BREAKING NEWS; MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AL...: Msanii huyo amekamatiliwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliyopo manispaa ya Son...
Venance Blog
Venance Blog
SAFARI YA MWISHO YA ALBERT MANGWEA
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya mwanamuziki Albert Mangwea almaarufu kama Ngwair hapa duniani leo Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amina
Jeneza lililobeba mwili wa Ngwair
BAADHI YA NYIMBO ZILIZOMUWEKA JUU SANA NGWAIR NI:
1. She got a gwan
2. CNN
3. Demu wangu
4.Nipeni dili
5. Mikasi
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI
AMINA!!..
Picha na DJ FETTY WA CLOUDS FM
TAMKO LA BALOZI WA TANZANIA WA AFRICA YA KUSINI KUHUSU KUCHELEWA MWILI WA MAREHEMU NGAIR
AnnaPeter: TAMKO LA BALOZI WA TANZANIA WA AFRICA YA KUSINI KU...: Balozi wa Tanzania Africa ya Kusini Radhia Msuya. Balozi wa Tanzania Africa ya Kusini kwenye picha hapo juu ametoa pole kwa familia,w...