IDADI YA WATU WALIOFARIKI UGANDA YAFIKIA 33
Moto mkubwa uliowaka baada yaajali mbaya ya barabarani iliohusisha lori la mafuta, umewauwa takriban watu 33 mjini kampala Uganda.
Watu wengine 30 wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia tukiohilo.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa kati ya waliofariki ni raia waliokuwa wanakimbilia eneo hilo la mkasa kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka kwa lori hilo.
maafisa wa serikali walikuwa katika harakati za kutambua mili ya waliofariki baada ya wengi wao kuchomeka vibaya.
Idara ya polisi imesema kuwa waliofariki waliteketea kiasi cha kutotambulika na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua miili ya waliokufa.
Comments
Post a Comment